Watumishi wa Umma waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa kukatwa mshahara wa mwezi Julai

Mtoa mada ulipata kura ngap maana umeandika kwa uchungu sana
 
Kuna tangazo linazunguka juu ya kutolipwa mishahara kwa wafanyakazi wa umma ambao walichukua fomu za kuomba kupata ridhaa kutokak chama cha mapinduzi ili wapeperushe bendera ya kuwania nafasi za ubunge.

Binafsi naunga mkono katazo la kutolipwa mshahara wa mwezi huu wa julai, ila kwa mtazamo wangu hawa wangefukuzwa na kufutwa kabisa katika utumishi wa umma...
Kweli wewe ni tahira, watu hufanya kazi kwa kufuata sheria za nchi,sheria za utumushi zimetoa ruhusa kwa mtumishi yoyote kuomba ruhusa isiyokuwa na malipo kwa majiri wake kwenda kugombea kama atahitaji na ikitokea ameteuliwa na chama inambidi mtumishi huyo kuacha kazi.

Sasa ww hilo la kutaka waachishwe kazi sijui umefata sheria ipi,acha wivu wa kimama dunia sasa watu huishi katika ulimwengu wa ushindani, wewe asira zako za kutokuwa na kazi au nduguzo kutokuwa na kazi unataka kuzimalizia kwa wenzako wanao tafuta green pasture.hao watumishi hawakuletewa hizo kazi wakiwa wamekinha 4 angaika na ww na uoache wivu wa kike.
 
CCM oyeeeeee CCM safiiiiiiii CCM juuuuuuuuu.

Na bado mtaisoma namba wote si mmeamua kujazana huko Sasa wanafanya Mambo kwa Uhuru maana wote mlishajipeleka huko. CCM wangekua na hofu ya kuanguka uchaguzi Mkuu kwa sababu upinzani nao Wana watu Wala msingefanyiwa hivyo.
 
Maana yake..
Top 3 pale juu nao wasilipwe..
Prezdaa/makamu wake pamoja na ka nae..au hiyo haiwahusu.wao....????
 
Kuna tangazo linazunguka juu ya kutolipwa mishahara kwa wafanyakazi wa umma ambao walichukua fomu za kuomba kupata ridhaa kutokak chama cha mapinduzi ili wapeperushe bendera ya kuwania nafasi za ubunge.

Binafsi naunga mkono katazo la kutolipwa mshahara wa mwezi huu wa julai, ila kwa mtazamo wangu hawa wangefukuzwa na kufutwa kabisa katika utumishi wa umma...

Utakuwa huna ajira wewe

Sasa unafikiri wakifukuzwa utapata wewe!!

Wivu unakusumbua.

Yaani kwkauwa mi nimeajiriwa Kama mtunza kumbukumbu basi niridhike na utunza kumbukumbu.....nyooo

Mbona ye Magu aligombea miaka mingi sana jimboni na amekuwa waziri miaka mingi akataka urais....

Sijapenda sana anapozuia watu kuwaza makubwa eti kwakuwa amewateua au wamegombea....
 
Kuna tangazo linazunguka juu ya kutolipwa mishahara kwa wafanyakazi wa umma ambao walichukua fomu za kuomba kupata ridhaa kutokak chama cha mapinduzi ili wapeperushe bendera ya kuwania nafasi za ubunge.

Binafsi naunga mkono katazo la kutolipwa mshahara wa mwezi huu wa julai, ila kwa mtazamo wangu hawa wangefukuzwa na kufutwa kabisa katika utumishi wa umma...
Du, hili povu ni la Nini hivi? Unapata shida gani Kama wakigombea na bado ni waajiriwa na mishahara yao! Au ndio unataka kumuingizaza mtegoni mkuu wetu wa nchi ili wafanyakazi na watia Nia wamchukie eeh!

Uzuri wa Magu yupo objective na hafanyi maamuzi kwa mihemko! Mungu azidi muongoza, kumlinda, na kumbariki rais wetu mpendwa Dr. JJP Magufuli na nchi yetu, amen!
 
Yaani mtu umeenda kugombea, umeomba ruhusa ya siku 3, kufika jimboni unaambiwa chama hakina fedha za kusafirisha wapiga kura, umechangia mshahara wako laki 9, ili wapiga kura wale, wanywe, halafu unapata kura moja , tena huku unasikia mshahara wa julai hamna. CCM Mungu anawaona.
Kwa kiasi kikubwa uchaguzi huu umesaidiwa na watumishi
Magufuli anapenda pesa yako,watia nia elfu kumi wameingizia chama billion mmoja .

Zaidi ya watia nia elfu 7 ni watumishi wa umma ataokwepa au ataokoa hazina sh 7000 x wastani 800,000=5,600,000,000 (wastani wa bilioni 5.6)
Huyo ndio mjomba Magu achezi mbali na pesa.
 
Binafsi naunga mkono katazo la kutolipwa mshahara wa mwezi huu wa julai, ila kwa mtazamo wangu hawa wangefukuzwa na kufutwa kabisa katika utumishi wa umma. Hawafai na walafi. Nchi imejaa vijana wengi waliohitimu vyuo wakihaha kutafuta kazi. Jitu limepewa kazi linatamaa ya kutaka Ubunge, hawa hawafai kbs ni bora wafukuzwe kazi wakalime. Ni ujinga wa hali ya juu kucheza na kazi.
Bahati mbaya kwako ni kwamba Utumishi wa Umma hauongozwi kwa mawazo au matamanio binafsi ya mtu mmoja mmoja, bali kwa sheria na kanuni zake. Kuna hatua za uchaguzi ambazo mtumishi wa umma anaruhusiwa kufika bila ajira yake kuathirika, na pia zipo ambazo akifikia basi ajira yake huathirika. Vyote hivyo vipo katika sheria, kanuni na miongozo ya utumishi
 
Akiingia kwenye website ya utumishi atapata Waraka wa Utaratibu kwa Watumishi wa Umma Wanaogombea Nyadhifa za Kisiasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zipo taarifa za kuzuia mishahara ya watumishi waliogombea nafasi mbalimbali katika mwezi huu wa Julai, aliyetoa ushauri huu ana nia ya kutaka kumuharibia Rais Magufuli 2020, Oktoba 28.

Rais Magufuli nikuombe uingilie kati hili, si jambo la afya na ukingazatia watia nia hao wataombwa kwenda kusaidia kuweka umoja katika majimbo waliogombea, nani atakubali kwenda kusaidia chama wakati mshahara wake ulikatwa...
Serikali haiongozwi kwa huruma ya mtu mmoja,hilo swala lipo kwenye taratibu/kanuni/sheria za utumishi wa umma ,hakuna mtia nia ambaye alikuwa hajui consequences zake!

Nasema wasilipwe mishahara ya july na wale watakaoteuliwa waondolewe kabisa kwenye system ambao hawatachaguliwa watalipwa mshahara wa mwezi wa nane ila wa july BABA JANE BYE BYE!

Nchi inaongozwa na sheria na si swala la kumuomba mtu!! Sheria zipo wazi unataka kuniambia kama ukiua unaweza kumuomba rais usishitakiwe?
 
Bahati mbaya kwako ni kwamba Utumishi wa Umma hauongozwi kwa mawazo au matamanio binafsi ya mtu mmoja mmoja, bali kwa sheria na kanuni zake. Kuna hatua za uchaguzi ambazo mtumishi wa umma anaruhusiwa kufika bila ajira yake kuathirika, na pia zipo ambazo akifikia basi ajira yake huathirika. Vyote hivyo vipo katika sheria, kanuni na miongozo ya utumishi
Huyu mbaba anavunja sana sheria.
 
Aliyewatuma nani, hata msipotoa ushirikiano hamna madhara- wengi wenu mliambulia kura 0 na 1 sasa ukitoa na ya mkeo kuna hasara gani?
 
Back
Top Bottom