WATUMISHI WA UMMA TUSIBABAISHWE, KINANA na NAPE na wenzao CCM hawana mamlaka kutukoromea sisi

NYAMKANG'ILI

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
223
112
WAKUU naona KINANA na wenzake wanazunguka na kukoromea watumishi wa umma na kutoa ahadi kemu2 kwamba "...wanaiagiza serikali itekeleze, watawachukulia hatua watumishi..." WAKIDAI NI CCM KUISIMAMIA SERIKALI YAKE...

Hapa naona kuna kutokuelewa maana ya "... Chama tawala CCM kuisimamia serikali yake...". Katibu mkuu CCM KINANA hana mamlaka ya kuiagiza serikali, kwa kisingizio cha chama kusimamia serikali. CCM kuisimaia serikali siyo kupitia mtu mmoja mmoja, bali vikao:mkutano mkuu, NEC & CC. Hivi vikao vina mamlaka ya kuisimamia serikali, siyo KINANA. Tunapaswa kuelewa hili. Jambo hili ni sawa na BUNGE kusimamia serikali: MBUNGE mmoja mmoja hana mamlaka ya kutoa maagizo kwa serikali, bali MBUNGE (SOMA IBARA 63 ya KATIBA TZ 1977).

NAKUMBUKA alipoingia Sec Gen MKAMA naye alizunguka nchi nzima na kutoa ahadi "mpya kabisa" na kukoromea serikali, aliitwa na kuambiwa anakosea na akapotelea kusikojulikana. MOJA ya ahadi za MKAMA ni kujenga hospitali ya RUFAA eneo la Kwangwa MUSOMA , yenye pia na chuo kikuu cha afya kama MUHIMBILI, MJINI MUSOMA, na akasema isipojengwa hadi 2015 basi CCM isichaguliwe ... TUNASUBILIA TUONE.

AHADI NYINGIZE za EX-SEC GEN MKAMA, wadau mtanisaidia...

KINANA naye anapita mle2, haya bwana: naona hawajajua kuwa CHAMA KUSHIKA HATAMU ILISHAKWISHA ZAMAAAAAAAAAAAAANI ... wanawadanganya wananchi
 
Wamechanganyikiwa na ufisad na kusahau majukumu yao.wanataka kufanya kama cdm wacjue kwamba cdm ni speed kubwa kaz yake kuishitaki serkal kwa wananchi pale wanaposhindwa kuwajbika kwa wananchi,wao ccm hawajielei mpaka sasa wafanye nn ili wapendwe kama cdm.
 
wameanza!!,eti WATOKE VIPI,sasa wanakuja na SINGLE hii(kuwatishia watumishi).Wanasahau kwamba wafanya kazi hawatakiwa kuingizwa katika siasa.!!

Boss wao alikosea kuwatishia wafanyakazi,MATOKEO YA UCHAGUZI uliopita,inaonyesha maeneo ya mjini ndipo walipo wafanyakazi wengi na ndipo CCM ilipoangushwa na WAPINZANI,(Arusha,Mwanza,Dar,Mbeya,n.K).

Wanatengeneza njia ya kushindwa kwao tena.!!!
 
Tatizo baada ya kuchaguliwa wenzao wameamini kuwa wao ni muarobani wa marehemu chama chao. Wametoka wakijua kwa imani hiyo watakachokiongea kitabadili imani ya wananchi kwa hilo genge lao la wezi
 
...himijitu inaweweseka tu hata haijui inafanya nini sasa,wamekumbuka shuka kumekucha...kila wakipiga hesabu wanaona hawajafanya kitu,ahadi za dhaifu nazo hazitekerezeki na muda nao umeisha,wanachofanya sasa ni juhudi za mfa maji....2015 lazima tuwatembeze uchi mji mzima...
 
Natambua kwamba hawa wanasiasa wazee wamekua hawapendezwi na jinsi Kikwete amejitahidi kuachia demokrasia ya vyama vingi ichukue nafasi yake. Sishangazwi kusikia kauli zilizopitwa na wakati toka kwa Kinana. Wazee baada ya mabadiliko ya katiba ya CCM wameondolewa ktk vikao vya maamuzi,wamebaki washauri,sasa naona waliamua kulazimisha watu aina ya Kinana na Mangula wawe viongozi wa juu kulinda maslahi yao wala siyo maslahi mapana ya chama. Bado wanaishi na mawazo ya chama kushika hatamu.
 
wamechanganyikiwa na
ufisad na kusahau majukumu yao.wanataka kufanya kama cdm wacjue kwamba
cdm ni speed kubwa kaz yake kuishitaki serkal kwa wananchi pale
wanaposhindwa kuwajbika kwa wananchi,wao ccm hawajielei mpaka sasa
wafanye nn ili wapendwe kama cdm.

cdm kwisney wanaweweseka kutokana na ccm kuisimamia serikali kutekeleza ahadi
 
Jamani mi sio CCM ni Mpinzani ila kwa hili mmemnukuu vibaya. Mimi juzi nilisikia ITV alivyokuwa mtwara akisema kwamba anapita kila eneo kuangalia maendeleo na kukusanya maoni ili ayafikishe kwenye vikao vyao waandae taarifa ya kuwasilisha mapendekezo Serikalini.

Mnyonge mnyongeni jaman.
 
Kweli kazi ipo hadi Mtumishi wa umma kufanyia kazi amri za watendaji wa chama haya ni mapya sasa anyways siye tushajitambua
 
Wautoe wapi ubavu huo...? Waitishe CC na NEC, hao ndo wenye mamlaka ya kuisimamia serikali! Akili ndogo kweli, yaani wanataka katibu mkuu atoe amri kwa mkurugenzi wa wilaya!
 
NYAMKANG'ILI

Mkuu hawana lolote hawa!! wanakula Per diem tu!!! Yaani wanatafuna kurejesha madeni ya rushwa za uchaguzi!!! Kwani safari si ni hela? Si ajabu kwa siku anakunja milion?
 
Last edited by a moderator:
siku akijuwa kutofautisha kati ya serikali na watendaji wa serikali basi tutampa uraia.

Serikali ni wananchi.
Hao mawaziri wake ni watendaji wa serikali, na ndio maana wananchi wakifika kikomo cha uvumilivu basi hao watendaji wanakuwa hawana chao.
 
Hata mimi nilikuwa najiuliza maswali mengi kichwani. Lakini ilipofika kipengele cha kutekeleza ilani ya chama kwa serikali iliyoko madarakani, basi nilitulia. Ila kinana atakuwa mpole soon
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom