Watumishi wa Umma (Seiekali) na dhamana mahakamani

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,799
30,724
Heshima wanajamvi,

Kumekuwa na tabia au utaratibu wa mahakama na wakati mwingine Polisi kuweka sharti la dhamana kwa watuhumiwa / washtakiwa kudhaminiwa na watumishi wa serekali.

Naomba kuulizwa watumishi wa umma wana sifa gani za ziada kushinda waTanzania wengine.Kuna waTanzania wengine wana uzito zaidi mahakamani ?.

ikiwa huna mtu anayefanyakazi serekalini basi haki ya dhamana inapotea ?.

Naomba kuwasilisha.
 
Kwa sababu MTU akiwa ameajiriwa serikalini kwanza Ajira ya kudumu.Na Ni nadra atoroke mana ana uhakika .
Wengi Sio wababaishaji(sio wote)
Ila kikubwa kwamba Huyu MTU Ni wa uhakika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni upumbavu uliopitiliza, kimsingi Tls ilipaswa kufunguwa kesi mahakama kuu kuhoji uhuni huu, kinachotakiwa kwa bailable case bond iwe ni pesa taslim au hao watumishi wa serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu wanawaita wakoloni ni mabeberu, ajabu yenyewe ule ujinga wote uliowekwa na wakoloni aka mabeberu kwa lengo la kutukoloni vizuri wao wameyakumbatia. Sheria/utaratibu huu na ule wa kujua makabila ya watu ni miongoni mwa ujinga wa kikoloni tunaoundekeza.
 
Kwa sababu MTU akiwa ameajiriwa serikalini kwanza Ajira ya kudumu.Na Ni nadra atoroke mana ana uhakika .
Wengi Sio wababaishaji(sio wote)
Ila kikubwa kwamba Huyu MTU Ni wa uhakika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ajira ya kudumu na mtu wa uhakika uhusiano wake upo wapi jielekeze kwenye huo mrengo wakati unajibu swali lililoulizwa tafadhali
 
Masharti hayo ya dhamana yana faida kwa pande zote. Kwa mtumishi wa umma inakiwa rahisi kwa sababu serikali ina nyaraka zake muhimu na hivyo kumfahamu. Kwa upande wa anayehitaji dhamana hupungizia muda wa kumtafuta mtu mwenye nyaraka zote zinazohitajika na anayefikika au kupatikana kirahisi.
 
Tatizo letu ni kwamba mara nyingi tunaangalia jambo au dhana au scenario bila kukamilisha dimensions zake.
 
Kwa hakika huu ni uhuni wa kupitiliza tena yafaa TLS yafaa watusaidie kwa kufungua kesi mahakama kuu au kesi ya kikatiba.
Ipo hoja dhaifu eti watumishi wa umma ni wahukakika zaidi kwasababu serekali ina taarifa zao muhimu.Katika ulimwengu wa sasa wa sayansi na technology serekali inakuwa na taarifa zote muhimu za wananchi wote hasa wakati wa kukata leseni TIN,Kitambulisho cha taifa na Passport yaani kule hakuna taarifa iliyoachwa sasa nashindwa kuelewa kwanini tunaendeleza utaratibu wa karne ya 20 ?.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom