Watumishi wa umma na wasomi, ninyi sio Watanzania pekee

Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
2,344
4,167
Aliyeishia darasa la nne ni Mtanzania
Aliyekataa kusoma ni Mtanzania pia
Machinga ni Mtanzania
Wauza Azam lambalamba ni Watanzania
Sandia fundi ni Mtanzania
Makahaba pia ni Watanzania
Ombaomba ni Watanzania

Hayo makundi yote yanahitaji kuangaliwa sawia kama vile nyie mnavyolilia ongezeko la mishahara na marupupu, kama vile wasomi mnavyolazimisha muajiriwe serikalini ndivyo vivyo hivyo hayo makundi yanatarajia ustawi bora toka serikalini.

Mfano:

Bwawa la Nyerere likikamilika ni viwanda vingapi vitajengwa nchini na kupunguza lundo la vijana wasio na elimu wala ajira serikalini kuajiriwa?

Acheni ubinafsi nchi ni ya kila Mtanzania, vumilieni ili wenzenu nao waje kunufaika na hii nchi

Nao pia sana haki kula mema ya ardhi yao!
 
Wanyonge tulieni hamjaridhika miaka yote mitano mmekula bata. Tulieni watumishi nao wale bata miaka mitano iliyobakia.

Huwezi endesha nchi bila watumishi wa umma hilo lazima ulitambue hata kama hulitaki.

Watumishi wa umma utawakuta tanesco, tbc, hospitalini, shuleni, tcra, posta, mahakamani, polisi, nk hao wote wanakuhudumia wewe mnyonge mwenye roho mbaya.
 
Asili ya binaadam ni ubinafsi.

Pamoja na kwamba mimi ni mtumishi, sijawahi kuwaza mstakabali wa taifa hili kwa kutumia mshahara wangu.

Watu wanataka umeme, matibabau bora, usafiri wa uhakika,nk.
 
Wanyonge wengine bwana, miaka yote 5 baba yenu aliwabeba, ngoja na sisi watumishi tulipwe stahiki zenu, halafu asilimia kubwa ya wanyonge walikimbia umande au walicheza pool mnachotakiwa kujua wanyonge ni kwamba mtumishi akilipwa vizuri atakuwa na nguvu ya kukubeba mfano kukutuma shambani au kusafisha nyumba,acha chuki kwa watumishi wa umma hao ndo wanaokoa maisha yenu na kufundisha watoto wenu.
 
Wanyonge tulieni hamjaridhika miaka yote mitano mmekula bata. Tulieni watumishi nao wale bata miaka mitano iliyobakia.

Huwezi endesha nchi bila watumishi wa umma hilo lazima ulitambue hata kama hulitaki.

Watumishi wa umma utawakuta tanesco, tbc, hospitalini, shuleni, tcra, posta, mahakamani, polisi, nk hao wote wanakuhudumia wewe mnyonge mwenye roho mbaya.
Tutaona hilo hata mnalongoja.
 
Usilete ujinga kwenye maisha ya watu, watu wanarisk maisha yao kwa kuhudumia watu wenye covid n.k wewe unapigana miti na mkeo? nani alikuzuia kusoma? wakati wa mwendazake machinga, mamalishe n.k wote walikuwa wanashangilia.
Kutokusoma kwangu kuna umuhimu kwako ndo maana Leo wewe ni mtumwa wa serikali chini ya kivuli cha utumishi
 
asili ya binaadam ni ubinafsi.

pamoja na kwamba mimi ni mtumishi,sijawahi kuwaza mstakabali wa taifa hili kwa kutumia mshahara wangu.

watu wanataka umeme,matibabau bora,usafiri wa uhakika,nk.
Kila kitu kinafanywa kwa mikakati na taratibu.
 
wanyonge wengine bwana,miaka yote 5 baba yenu aliwabeba,ngoja na sisi watumishi tulipwe stahiki zenu,halafu asilimia kubwa ya wanyonge walikimbia umande au wakicjeza pool mnachotakiwa kujua wanyonge ni kwamba mtumishi akilipwa vizuri atakuwa na nguvu ya kukubeba mfano kukutuma shambani au kusafisha nyumba,acha chuki kwa watumishi wa umma hao ndo wanaokoa maisha yenu na kufundisha watoto wenu
Acha chuki na dharau kwa wanyonge hao ndo walofanya uajiriwe hao ndo wataofanya upandishiwe mshahara.
 
Watumishi ni kati ya watu wenye maisha bora hapa nchini na wengine wameshafika uchumi wa kati wa juu. Wasubiri kidogo mkulima naye atolewe kwenye jembe la mkono.
 
Wanyonge tulieni hamjaridhika miaka yote mitano mmekula bata. Tulieni watumishi nao wale bata miaka mitano iliyobakia.

Huwezi endesha nchi bila watumishi wa umma hilo lazima ulitambue hata kama hulitaki.

Watumishi wa umma utawakuta tanesco, tbc, hospitalini, shuleni, tcra, posta, mahakamani, polisi, nk hao wote wanakuhudumia wewe mnyonge mwenye roho mbaya.
Hawo wadanganyanyika neno la wanyonge linawafaa sana maana walilifurahia sana huku wakapigwa
 
Nashauri badala ya kupandisha mishaharw serikali itumie pesa hizo kufungua vitu kama irrigation schemes ili vijana wakajiajiri.
 
Watumishi ni kati ya watu wenye maisha bora hapa nchini na wengine wameshafika uchumi wa kati wa juu. Wasubiri kidogo mkulima naye atolewe kwenye jembe la mkono.
Hao watu ni wa hovyo sana sijui wanawachukiliaje watu ambao hawana ajira serikalini.
 
Hawo wadanganyanyika neno la wanyonge linawafaa sana maana walilifurahia sana huku wakapigwa
Wakati sie tukipigwa pekeetu enzi ya kikwete mlikuwa wapi?
Acha tupigwe kama kupigwa ni kuanzishwa kwa miradi inayoonekana
 
Back
Top Bottom