Watumishi wa umma mje hapa tubadilishane mawazo kuhusu harakati za kimaisha

maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,774
2,297
Kwanza nawapa pole kwa yanayoendelea nikiwepo mimi mwenyewe.

Lengo la uzi huu ni kutafuta namna mbadala nje ya kazi zetu. Mimi nimekuwa na kabiashara kangu na huko ndo nguvu zangu iliko kwa wingi maana ndiyo kazi inayoniweka mjini naonekana mtu.

Pili nawaomba tusiwaze sana kwamba sijui ataongeza lini au daraja itapanda lini kubwa tupambane nje ya kazi zetu kuna lipa sana na utapata hata ziada ya kusomesha watoto shule za hadhi ili wajikomboe maana awamu hii imeamua laivu kwamba wewe mtumishi kwanza unapata mshahara huwezi kuwa sawa na bibi na babu kule kijijini ndivyo mawazo yao yalivyo.

Tatu awamu hii haina mpango na watumishi kwa hiyo tukae tukijua hilo na wao wanajua hili. sasa tufanyaje? Kila moja akili kichwani mwako kama unakaa kijijini lima maestate ya kufa mtu ukishakopa fanya jambo litakalokutoa kwenye umaskini kama uko mjini cheki fursa inayopatikana fanya kitu unaweza nunua boda boda tano ikawa inakuletea kiasi fulani kila siku nao ni mradi tosha tu.

Ugumu wa maisha hufanya watu wafikiri sana na lengo la uzi huu ni kutafuta mbadala kuliko kulalamika maana hawana mpango na sisi.

Tupeane location za maana mtu akitaka kufanya biashara kwa bidhaa za madukani aina zote mimi nauza duka la nguo za akina mama wapi napata bidhaa bei nafuu kwa Dodoma, Arusha na Dar.

Maana tumeandaliwa circle ya poverty na wanaona tunafaidi sana lakini wanasahau mtumishi ambaye hajatulia akili yake hawezi kutoa kile kilichokusudiwa kwake afanye.

Karibuni wadau
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom