Watumishi wa umma ipo siku mtakumbuka maneno ya Lissu kuhusu kikokotoo

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,944
2,000
Katika mkutano mmoja wa kampeni hivi karibuni, Lissu alionya juu ya sheria ya kikokotoo ambayo kwa sasa imewekwa pending mpaka 2021, sheria ambayo kwa mujibu wa Lissu itafyeka nusu ya mafao ambavyo mstaafu anastahili kulipwa.

Lissu kawaonya Polisi na watumishi wengine wa umma ambao kwa nafasi zao, wanaweza kutumika kusaidia watu au mtu fulani kusalia madarakani. Kawaeleza kuwa, wakifanya hivyo, wajue siku wakistaafu,nusu ya mafao yao imekwenda na maji.

Mimi naomba niongeze na lile kundi lingine la wasaka vyeo na wasiotazama mbele kuwa hata wao ama watoto wao wanaweza kuja kuwa wahanga wa sheria hii.

Tusitake kuwa kama Wayahudi ambao hawakuelewa lengo la Mungu kuwaletea mwanae Yesu Kristo ili wakombolewe kama ambavyo na sisi tumeletwa huyu Lissu leo hii ili atuongoze katika kujikomboa na ndio maana hata Mungu alimnusuru baada ya shambulio lile.

Tukipuuza maneno haya ya Lissu,ipo siku tutakumbana na ukweli huu kama ambavyo Wayahudi walikumbwa na giza baada ya kumsulubisha Yesu msalabani.
 

Abdul Mganyizi

JF-Expert Member
Oct 28, 2019
434
1,000
Mkuuu unachokisema kipo sahihi ,mm ni mtumishi kila nikilifikilia hilo ninapata ganzi kweli kweli ,tunajiuliza maswali mengi tutapambana vipi kujinusuru.Watumishi wanalitambua hilo lakini kumbuka tupo watu milioni moja tu ,unaddani tunafanyaje hapo mkuu na elimu ndogo ya watanzania?
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,944
2,000
Mkuuu unachokisema kipo sahihi ,mm ni mtumishi kila nikilifikilia hilo ninapata ganzi kweli kweli ,tunajiuliza maswali mengi tutapambana vipi kujinusuru.Watumishi wanalitambua hilo lakini kumbuka tupo watu milioni moja tu ,unaddani tunafanyaje hapo mkuu na elimu ndogo ya watanzania?
Uzuri huu utawala umegusa lila mtu.
 

Nakukunda

JF-Expert Member
Jul 10, 2017
654
1,000
Mkuuu unachokisema kipo sahihi ,mm ni mtumishi kila nikilifikilia hilo ninapata ganzi kweli kweli ,tunajiuliza maswali mengi tutapambana vipi kujinusuru.Watumishi wanalitambua hilo lakini kumbuka tupo watu milioni moja tu ,unaddani tunafanyaje hapo mkuu na elimu ndogo ya watanzania?
Magu hafai kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi..Kikwete please tuonee huruma
 

Abdul Mganyizi

JF-Expert Member
Oct 28, 2019
434
1,000
Tatizo watumishi wetu akili zao walishazipark tucuta
Saivi unakuta wengi wao wanamshangilia jiwe kwa kuongeza elfu 12 kwa mwezi moja baada ya miezi 72
Inawezekana unachokisema lakini mm naona tunapokutana watumishi wengi wanaomba jamaa aanguke ila ndoo hivyo tunatishiwa huko juu kuwa ukigundulika unashabikia upinzani ajira ndoo utaisahau na utafanyiwa visa vya kutosha.

Juzi wamekuja na kutwambia kuwa usimamizi watahusishwa watumishi tu ndoo wenye kuokoa hii serikali irudi madarakani ,tukawasikiliza wanavyojishaua kutuona leo ndoo tunafaa kuirudisha serikali madarakani.
 

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
14,022
2,000
Inawezekana unachokisema lakini mm naona tunapokutana watumishi wengi wanaomba jamaa aanguke ila ndoo hivyo tunatishiwa huko juu kuwa ukigundulika unashabikia upinzani ajira ndoo utaisahau na utafanyiwa visa vya kutosha.Juzi wamekuja na kutwambia kuwa usimamizi watahusishwa watumishi tu ndoo wenye kuokoa hii serikali irudi madarakani ,tukawasikiliza wanavyojishaua kutuona leo ndoo tunafaa kuirudisha serikali madarakani.
Wewe kaa kimya,subiri siku ya uchaguzi mkamfyekelee mbali.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,586
2,000
Chakushangaza Wabunge kila baada ya miaka 5 wanachukua mzigo wao wa kutosha, baada ya miezi mitatu wanarudi tena mjengoni!

Hawana fao la kujitoa wala kikokotoo!! Wanasiasa hawana tofauti yoyote ile na mnyama aina ya nguruwe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom