Watumishi wa umma hawaruhusiwi kumiliki biashara, mali na vitega uchumi kupitia taaluma zao?

Mr Emmy

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
1,219
550
Napenda watumishi wa Umma wa wawajibike na kutekeleza majukumu yao ipasavyo lakini kwa hali inayoendekea sasa wanasiasa wanataka kuwafanya watumishi wa umma kama watumwa na makabwela wasioruhusiwa kumiliki mali, biashara na vitega uchumi.

Kitendo cha Waziri wa Afya MH Ummy Mwalimu kuwataka watumishi katika sekta ya afya kujieleza kwa maandishi umiliki wa biashara zao katika fani zao. Kitendo cha kuwataka Madakatari, waaguzi, wafamasia, maabara kukiri na kujieleza why wanamiliki hospitali, clinic, maduka ya dawa, maabara ni kitu tu cha kisichofaa kwani ni wapi katiba inawakataza kufungua ama kutumia vyeti vyao kuanzisha biashara na vitega uchumi kupitia taaluma zao.

Ili kutowanyanyapaa watmishi katika sekta ya Afyan vyema watumishi wote wa umma wajieleze na kukiri kumiliki biashara zao; mfano Afisa Kilimo ambaye ana mashamba yake binafsi ajieleze, afisa Mifugo anayefuga ajieleze, mwalimu mwenye shule ama tution centre ajieleze, afisa biashara anayefanya biashara ajieleze, afisa ardhi anayepima aridhi bnafc ajieleze, Engineer mwenye kampuni ajieeze.

NI VYEMA IKATOLEWA SHERIA AMA WARAKA MAALUM WA KUWAZUIA WATUISHI WA UMMA KUFANYA BIASHARA AMA SHUGHULI NYINGINE INAYOMUINGIZIA KIPATO ZAIDI YA AJIRA YAKE SERIKALIN

Mwisho wewe Mh Waziri toka umezaliwa na kufanya kazi serikalini hauna biashara yeyote unayofanya kukungizia kipato zaid ya mshahara unaolipwa? kama ipo nawe jieleze tu
 
as much as tunataka accountability basi hili jambo la kujieleza mali ulizonazo liwe universal, watumishi wote wa umma wanatakiwa wajieleze mali walizo nazo!!!
 
what is the effect hata ukijeleza una majumba 75? Au unaendesha nar? Au una semi trela? Ukiona hivyo ujue wivu umeanza kuwasakama. Kama sheria inasema wafanyakazi wa Umma wasifanye biashara iwekwe wazi ili waweze kuamua kuendelea kufanya kazi au kusepa.
 
what is the effect hata ukijeleza una majumba 75? Au unaendesha nar? Au una semi trela? Ukiona hivyo ujue wivu umeanza kuwasakama. Kama sheria inasema wafanyakazi wa Umma wasifanye biashara iwekwe wazi ili waweze kuamua kuendelea kufanya kazi au kusepa.[/QUOTE

YAAAH thats true, mambo yawekwe wazi tujue
 
inabidi wanasiasa wasiwachukulie poa watumishi wa umma kila mara na kwa kila kitu...siku waki-react back--heshima itakuwepo.
 
Tatizo umeona mkurugenzi katumbuliwa ukaamua uje juu, utumishi wa umma kumiliki vitu si tatizo, tatizo ni wqngapi wana uaminifu wa kutokujiingiza katika mgongano wa masrahi ili kuneemesha biashara zao? ni waaminifu?
 
Tatizo linaonekana kwa Watumishi wa Umma tu, Wanasiasa ni watakatifu katika hili!
 
Nakumbuka ni Raisi Mkapa aliyeruhusu watu waanzishe biashara zao hizo baada ya kuona serikali haiwezi kuwalipa lakini msimamizi lazima asiwe mfanyakazi wa serikali ndipo baadhi ya madaktari wakaondoka kwa mfano Tumaini hospital ni hospitali ya madaktari wazalendo ambao wamekataa kukimbia nchi ili wasaidie wananchi wao hivi Magufuli na timu yake ya mawaziri waliochanganyikiwa wanadhani wanaweza kuendesha nchi bila watumishi wa umma huu ni upuuzi ulio pitiliza
 
Tatizo umeona mkurugenzi katumbuliwa ukaamua uje juu, utumishi wa umma kumiliki vitu si tatizo, tatizo ni wqngapi wana uaminifu wa kutokujiingiza katika mgongano wa masrahi ili kuneemesha biashara zao? ni waaminifu?
Hivi ummy anawe uwezo wa kumsimamisha mkurugenzi wa ocean road ile si ni tassisi inayojitegemea si ina maana ni presidential posts wanawachezea madaktari wauguzi na wafamasia na watu wa maabara wanaofanya kazi kubwa kwa mishahara kiduchu wanawadharau kwa sababu ni wanasiasa tusubili tuone
 
ukitumikia mabwana wawili moja atalalamika, Waziri yuko sahihi, waliomba kazi ya kutumikia jamii kwa moyo wote sio waliomba kazi na kijibiashara, mbona manesi hawaji na vitumbua kuwauuzia wagonjwa? manesi hawana haki? wafagizi je, acha kutetea uvundo hata ulaya haya hayapo ila umwambie hawaboreshehe mishahara waache kutanga tanga, hata hivyo ile ya kumwona daktari tshs 5 mpaka 10 inawatosha ila ulafi tu kwa kuwa wameendekezwa kwa kuwa wanatibu watu, kama ni suala la biashara hata rubani wamruhusu awe anatembea na watu wa kufundisha kuendesha ndege basi KHa!
 
kwakeli ni jambo linalochanganya sana,kama tunataka kujenga maadili,ni vyema,kama Taifa,sote tukamulikana na kusiwe na ndimi mbili katika hili,maana watumishi wa umma wanaonekana kama ndio stage ya wanasiasa kupashia misuli na kutolea matamko na vitun kama hivyo,ikumbukwe,matatizo makubwa ya nchi yetu hayaanzishwi na wafanyakazi wa umma ...utaratibu wa kushuhghulikia watumishi wa umma,sidhani kama una tija,naamini hili ni wimbi,litapita,kama yalivyopita mawimbi mengine...wanasiasa,wao ni kama malaika,wanalipana mishahara mikubwa na miposho kedekede sambamba na wimbi la vikao,warsha,kongamano na masemina,hakuna anaewajali,ila wataalam wanaohudumia jamii ndio wananyanyaswa na kuteseka kwa mishahara kiduchu na mazingira magumu ya kazi,kumbukeni kuna KARMA
 
inabidi wanasiasa wasiwachukulie poa watumishi wa umma kila mara na kwa kila kitu...siku waki-react back--heshima itakuwepo.

Endeleeni kujidanganya. Unajua maana ya neno "Mtumishi wa Umma"!? Utareact back kwa nani!? Mlizoea kufanya kazi kwa mazoea na kugeuza ofisi za umma Mali yenu. Mwisho wenu umefika.
 
Endeleeni kujidanganya. Unajua maana ya neno "Mtumishi wa Umma"!? Utareact back kwa nani!? Mlizoea kufanya kazi kwa mazoea na kugeuza ofisi za umma Mali yenu. Mwisho wenu umefika.

Husiwe poyoyo unafikiri kila mtu mtumishi wa umma? Husifikiri kila mtu ana negativity kiasi hicho. Jibu hoja acha kupayuka
 
Napenda watumishi wa Umma wa wawajibike na kutekeleza majukumu yao ipasavyo lakini kwa hali inayoendekea sasa wanasiasa wanataka kuwafanya watumishi wa umma kama watumwa na makabwela wasioruhusiwa kumiliki mali, biashara na vitega uchumi.

Kitendo cha Waziri wa Afya MH Ummy Mwalimu kuwataka watumishi katika sekta ya afya kujieleza kwa maandishi umiliki wa biashara zao katika fani zao. Kitendo cha kuwataka Madakatari, waaguzi, wafamasia, maabara kukiri na kujieleza why wanamiliki hospitali, clinic, maduka ya dawa, maabara ni kitu tu cha kipuuzi kwani ni wapi katiba inawakataza kufungua ama kutumia vyeti vyao kuanzisha biashara na vitega uchumi kupitia taaluma zao.

Ili kutowanyanyapaa watmishi katika sekta ya Afyan vyema watumishi wote wa umma wajieleze na kukiri kumiliki biashara zao; mfano Afisa Kilimo ambaye ana mashamba yake binafsi ajieleze, afisa Mifugo anayefuga ajieleze, mwalimu mwenye shule ama tution centre ajieleze, afisa biashara anayefanya biashara ajieleze, afisa ardhi anayepima aridhi bnafc ajieleze, Engineer mwenye kampuni ajieeze.

NI VYEMA IKATOLEWA SHERIA AMA WARAKA MAALUM WA KUWAZUIA WATUISHI WA UMMA KUFANYA BIASHARA AMA SHUGHULI NYINGINE INAYOMUINGIZIA KIPATO ZAIDI YA AJIRA YAKE SERIKALIN

Mwisho wewe Mh Waziri toka umezaliwa na kufanya kazi serikalini hauna biashara yeyote unayofanya kukungizia kipato zaid ya mshahara unaolipwa? kama ipo nawe jieleze tu

Thanks sana mkuu kwa kuhoji,

KUna namna ya kumanage hii issue; I think sio vibaya mtu kuwekeza kwa kutumia taaluma au kipaji chake, ila declaration ya hiyo investment ni muhimu na pia kujitahidi kuonyesha kwamba hakuna conflict of interest... Kingine kinachonitisha kidogo ni jinsi ilivyokua rahisi kusimamisha watu kabla ya kujiridhisha kwamba kuna shida

I cant wait kuona tunafika wapi na hii issue kwasababu naona kama inakua mismanaged
 
Husiwe poyoyo unafikiri kila mtu mtumishi wa umma? Husifikiri kila mtu ana negativity kiasi hicho. Jibu hoja acha kupayuka
usiwashwe namna hiyo waziri ana akili acha afanye kazi yake, kuna upotevu wa madawa wanaambiwa wakanunue mahari furani kwa vimemo, hii haikubaliki kabisa.
 
Waziri yuko sahihi 100%, kutokana na malalamiko yanayotolewa na wagonjwa kuwa mkuu anataka uwende hospital kwake ndo utapata

huduma nzuri, hafu we umekaa nyuma ya keyboard unatetea upumbavu kisa ulitaka chadema wapewe nchi, uchaguzi ushaisha, wote

tutetee maslai ya watanzania. Kiukweli huwezi kuwatumikia mabwana wawili
 
Back
Top Bottom