Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,797
- 71,216
Kuna usemi katika vitabu vitakatifu usemao: Mna macho lakini hamuoni na mna masikio lakini hamsikii.
Hivi watumishi wa umma, yaani serikali, na mashirika yote mnafahamu kuwa leo mpo kazini na kesho hampo? Aidha kwa kustaafu, ulemavu, kufukuzwa au kuacha mwenyewe?
Siku zote mnaweka akiba kupitia mifuko ya jamii kama NSSF, GEPF, PPF nk ambayo sasa imeunganishwa kiubabaishaji.
Lengo la akiba hiyo ni kukufaa uzeeni au wakati utakapohitaji. Lakini sasa ni zaidi ya miaka miwili watu wamestaafu na wengine mikataba imeisha na hakuna mafao yalipwayo zaidi ya danadana, kwa nini?
Jibu ni fedha zao hazipo, serikali ya CCM imezikopa (au tuite kupora) na ndio maana inashindwa kulipa.
Je, wewe uliye kazini sasa, unakubali hali hiyo ije ikutokee wakati wako wa kutoka kazini ukifika?
Hakuna anayetaka hilo. Dawa ni moja tu, kuhakikisha CCM hairudi ofisini kuendelea na hadaa zake na kushindwa kuinua uchumi.
Kama mfanyakazi ambaye unayo nafasi ya kuikataa CCM, pia unayo nafasi ya kuwaelimisha wale wote waliokuzunguka kuikataa CCM na hata wazazi wako kama wako kijijini.
Vinginevyo ujue CCM ikiendelea kuwepo ndio kifo chako cha mapema wakati hao walio humo na familia zao wanazidi kuneemeka.
Sent using Jamii Forums mobile app