Uchaguzi 2020 Watumishi wa umma, chagua CCM 2020 yakukute ya wastaafu wa leo

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,758
71,139
Kuna usemi katika vitabu vitakatifu usemao: Mna macho lakini hamuoni na mna masikio lakini hamsikii.

Hivi watumishi wa umma, yaani serikali, na mashirika yote mnafahamu kuwa leo mpo kazini na kesho hampo? Aidha kwa kustaafu, ulemavu, kufukuzwa au kuacha mwenyewe?

Siku zote mnaweka akiba kupitia mifuko ya jamii kama NSSF, GEPF, PPF nk ambayo sasa imeunganishwa kiubabaishaji.

Lengo la akiba hiyo ni kukufaa uzeeni au wakati utakapohitaji. Lakini sasa ni zaidi ya miaka miwili watu wamestaafu na wengine mikataba imeisha na hakuna mafao yalipwayo zaidi ya danadana, kwa nini?

Jibu ni fedha zao hazipo, serikali ya CCM imezikopa (au tuite kupora) na ndio maana inashindwa kulipa.

Je, wewe uliye kazini sasa, unakubali hali hiyo ije ikutokee wakati wako wa kutoka kazini ukifika?

Hakuna anayetaka hilo. Dawa ni moja tu, kuhakikisha CCM hairudi ofisini kuendelea na hadaa zake na kushindwa kuinua uchumi.

Kama mfanyakazi ambaye unayo nafasi ya kuikataa CCM, pia unayo nafasi ya kuwaelimisha wale wote waliokuzunguka kuikataa CCM na hata wazazi wako kama wako kijijini.

Vinginevyo ujue CCM ikiendelea kuwepo ndio kifo chako cha mapema wakati hao walio humo na familia zao wanazidi kuneemeka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ndio nafasi ya watumishi kuudhahibu huu utawala dhalimu, rais akiwa ana 'brag' kuhusu kununua madege anasema hela zipo za kutosha, likija suala la maslahi ya watumishi ghafla kauli inabadilika kuwa hela hakuna. Sasa tumwondoe maana kazi imemshinda. Amebakia kufanya shopping ya madege tu.
 
Hakuna mfanyakazi atakaye ichaguwa ccm kama anaakili timamu maana amenyonywa sana awamu hii hakuna annual increment wala kupandishwa madaraja yani mtu anawanyonya kama ni vitu vinavyotolewa kihisani wakati viko kisheria
 
Lowasa wakimtumia atawashauri ana plans nyingi za kweli na udhoefu ni tofauti na wengi walivyoaminishwa
 
Hakuna anayewaza kukata mguu kwa kuwa kuna kidonda kwenye unyayo ili atembelee mguu wa bandia. Naamini umenielewa kama hujaelewa subiri nikueleze.

Inawezekana CCM ni kidonda kwenye mguu na kidonda hicho kinamfanya mtu ashindwe kutembea lakini baada ya muda kidonda hicho kitapona kwa sababu tiba imepatikana. Hivyo si vema kuwaza kukata mguu kwa kidonda cha muda ili utembelee mguu bandia ambao utakutesa. Bila kumung'unya hapa mguu bandia ni upinzani
 
Back
Top Bottom