• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Elections 2020 Watumishi wa umma, chagua CCM 2020 yakukute ya wastaafu wa leo

Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
33,824
Points
2,000
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
33,824 2,000
Kuna usemi katika vitabu vitakatifu usemao: Mna macho lakini hamuoni na mna masikio lakini hamsikii.

Hivi watumishi wa umma, yaani serikali, na mashirika yote mnafahamu kuwa leo mpo kazini na kesho hampo? Aidha kwa kustaafu, ulemavu, kufukuzwa au kuacha mwenyewe?

Siku zote mnaweka akiba kupitia mifuko ya jamii kama NSSF, GEPF, PPF nk ambayo sasa imeunganishwa kiubabaishaji.

Lengo la akiba hiyo ni kukufaa uzeeni au wakati utakapohitaji. Lakini sasa ni zaidi ya miaka miwili watu wamestaafu na wengine mikataba imeisha na hakuna mafao yalipwayo zaidi ya danadana, kwa nini?

Jibu ni fedha zao hazipo, serikali ya CCM imezikopa (au tuite kupora) na ndio maana inashindwa kulipa.

Je, wewe uliye kazini sasa, unakubali hali hiyo ije ikutokee wakati wako wa kutoka kazini ukifika?

Hakuna anayetaka hilo. Dawa ni moja tu, kuhakikisha CCM hairudi ofisini kuendelea na hadaa zake na kushindwa kuinua uchumi.

Kama mfanyakazi ambaye unayo nafasi ya kuikataa CCM, pia unayo nafasi ya kuwaelimisha wale wote waliokuzunguka kuikataa CCM na hata wazazi wako kama wako kijijini.

Vinginevyo ujue CCM ikiendelea kuwepo ndio kifo chako cha mapema wakati hao walio humo na familia zao wanazidi kuneemeka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Emmanuel Robinson

Emmanuel Robinson

Verified Member
Joined
May 29, 2013
Messages
1,084
Points
1,500
Emmanuel Robinson

Emmanuel Robinson

Verified Member
Joined May 29, 2013
1,084 1,500
Watu wanachaguliwa wananunuliwa bora tu tuchague ccm
 
simplemind

simplemind

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2009
Messages
14,436
Points
2,000
simplemind

simplemind

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2009
14,436 2,000
Mwalimu Mdoe amekufa kwa njaa akisotea mafao yake kwa miaka mitatu mfululizo bila mafanikio .

Namuomba Mwenyezi Mungu aipokee roho yake
Kumbuka dana dana waliopigwa waastafu wa EAC kuhusu mafao baada ya kuvunjika jumuiya ya mwanzo. Siyo binaadamu hawa.
 
mwarobaini_

mwarobaini_

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2020
Messages
228
Points
1,000
mwarobaini_

mwarobaini_

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2020
228 1,000
Hii ndio nafasi ya watumishi kuudhahibu huu utawala dhalimu, rais akiwa ana 'brag' kuhusu kununua madege anasema hela zipo za kutosha, likija suala la maslahi ya watumishi ghafla kauli inabadilika kuwa hela hakuna. Sasa tumwondoe maana kazi imemshinda. Amebakia kufanya shopping ya madege tu.
 
The coolest jw

The coolest jw

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2016
Messages
500
Points
1,000
The coolest jw

The coolest jw

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2016
500 1,000
Hakuna mfanyakazi atakaye ichaguwa ccm kama anaakili timamu maana amenyonywa sana awamu hii hakuna annual increment wala kupandishwa madaraja yani mtu anawanyonya kama ni vitu vinavyotolewa kihisani wakati viko kisheria
 
K

kitimtim

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2010
Messages
428
Points
250
K

kitimtim

JF-Expert Member
Joined Nov 24, 2010
428 250
Lowasa wakimtumia atawashauri ana plans nyingi za kweli na udhoefu ni tofauti na wengi walivyoaminishwa
 
K

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Messages
1,391
Points
2,000
K

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2019
1,391 2,000
Hakuna anayewaza kukata mguu kwa kuwa kuna kidonda kwenye unyayo ili atembelee mguu wa bandia. Naamini umenielewa kama hujaelewa subiri nikueleze.

Inawezekana CCM ni kidonda kwenye mguu na kidonda hicho kinamfanya mtu ashindwe kutembea lakini baada ya muda kidonda hicho kitapona kwa sababu tiba imepatikana. Hivyo si vema kuwaza kukata mguu kwa kidonda cha muda ili utembelee mguu bandia ambao utakutesa. Bila kumung'unya hapa mguu bandia ni upinzani
 
K

katitu

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2010
Messages
531
Points
500
K

katitu

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2010
531 500
Unaumwa wewe kwa lipi yaani,kutopandishwa mishahara,vyeo,hakuna semina,kwenda nje nk. Huyo mtumishi atakayechagua ccm atakuwa mwehu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,406,193
Members 532,237
Posts 34,508,034
Top