Watumishi wa umma 125,000/-; wanafunzi 300,000/= per month!

Kichwa Ngumu

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
1,726
312
Wiki chache zilizopita tulisikia Wanachuo wa Mlimani wamegoma kuingia madarasani kwa sababu ya fedha wanayopewa meal na accomodation Tsh. 5,000/= haitoshi, sina shaka na hilo na pia naamini kuwa haitoshi kweli kwa sababu miaka miwili iliyopita nilikuwa pale na matatizo kama hayo yalinikuta.

Waligoma wakitaka hela hiyo iongezwe toka Tsh. 5,000 hadi 10,000

Nashindwa kuielewa serikali katika hili ilifikiria nini? Mwanachuo ambaye analipwa Tsh. 5000 ni kwa ajili yake yeye mwenyewe bila kujali kama anafamilia au hana na hata kama anayo serikali haitambui hilo; kwa mwanachuo kulipwa Tsh. 5000 kwa siku ni sawa na Tsh. 150,000.00 kwa mwezi kama ungekuwa ni mshahara tunaita TAKE HOME, wengine wanaita NET PAY.

NASHANGAZWA
Mtumishi wa Serikali ambaye Serikali inatambua kuwa anafamilia ya watu sita yaani yeye, mke/mme na watoto wanne analipwa kima cha chini cha Tsh. 135,000.00 (TGOS A) as gross pay ukitoa michango ya kijamii analipwa Tsh. sio zaidi 125,000.00 na huyo mtumishi anafanya kazi labda DSM ambapo ugumu wa maisha hauna tofauti kati ya mwanachuo na huyo mtumishi ambaye anafamilia ya watu sita.
Tena mwanachuo analipwa kwa ajili ya meal na accomodation tu lakini mtumishi ni kwa ajili ya matumizi yote ya binadamu, pia inaaminika mwanachuo anaweza kupata msaada kutoka kwa wazazi wake

NAAMINI
Mwaka ujao wa fedha Serikali itaongeza hela ya meal na accomodation kwa wanachuo ingawa inaweza isifike Tsh. 10,000.00

NAPENDEKEZA
Serikali imlipa Mwanachuo chini ya kima cha chini cha mshahara wa mtumishi yaani kama mwanachuo atalipwa Tsh. 7,500 kwa siku basi mtumishi alipwe Tsh. 12,500 kwa siku kama kima cha chini.

KAMA SERIKALI HAITA ZINGATIA PENDEKEZO LANGU NATABIRI
  1. Kutajitokeza mgomo wa wafanyakazi nchi nzima na utaivuruga serikali
  2. Kwa sasa molali ya wafanyakazi imeshuka na itazidi kushuka zaidi hivyo kazi zitafanyika bila kuwa na tija (mafanikio) uzembe mdogo mdogo ambao utasababisha majanga makubwa kama ya Gongo la Mboto utaongezeka na Serikali itatumia fedha nyingi kuurekebisha.
  3. Ufisadi mdogo mdogo maofisini kwa kila mfanyakazi utaongezeka ambao ukijumuishwa mfanyakazi na mfanyakazi utaleta hasara kubwa kwa Serikali
Nawasilisha
 
Mimi nasikitishwa sana na watumishi wa umma, wanapewa mshahara mdogo mno ambao haukidhi hata mahitaji msingi kwa wiki mbili tu. Hapa nazungumzia wale wa KCC, ambao naamini ndio wengi, lakini hata siku moja hutawasikia wakipaza sauti zao kuishinikiza serikali iongeze mshahara! Kutokana na ugumu wa maisha uliopo sasa, bado wapo kimya, Wanaishije?

Mi naamini huu ndo wakati muafaka wa watumishi wa umma kusimama kidete kudahi haki zao kwa vitendo na kwa sauti iliyo kuu, TUCTA sio watetezi tena!
 
Mnacheza na watumishi wa umma nyie... wana maganji kibao, maposho, vikao, semina, warsha, kongamano... vyote hivyo ukivijumuisha kwa mwezi ni mara mbili ya mshahara wake... kuna wengine hata mshahara hawautumii, tena na kujenga wanajenga...
 
acho uongo wewe,maposho kibao yanatoka wapi? mwalimu anamakongamano na semina za wapi, nesi, askari polisi magereza jwtz hizo semina wanafanyia wapi? na watumishi wengine wengi hizo posho wanazipata wapi?
 
Nani kasema TUCTA kipo kwa maslai ya Wafanyakazi, Tucta ni wakandamizaji wa wafanyakazi yako wapi maandamano waliosema wataandamana nchi nzima. Wakina Mgaya ni Wasaliti wa wafanyakazi wa Umma (Traitor)
 
mnacheza na watumishi wa umma nyie... Wana maganji kibao, maposho, vikao, semina, warsha, kongamano... Vyote hivyo ukivijumuisha kwa mwezi ni mara mbili ya mshahara wake... Kuna wengine hata mshahara hawautumii, tena na kujenga wanajenga...

porojo hizo mkuu!!
 
Tucta sio watetezi wa wafanya kazi kwani wao wenyewe wanawadhulumu haki zao wafanya kazi wao; nawafahamu wafanyakazi wengi wanaowadai mafao yao baada ya kustaafu na mpaka leo hawajalipwa!! Tucta haina moral authority ya kuwatetea wafanyakazi.
 
yaani umenena haswa mie nimefurahi kujua as nilidhani hiyo elfu 5 ilikuwa kwa sio siku moja.

Inasikitisha I hope wahusika wataona ujumbe wako
 
acho uongo wewe,maposho kibao yanatoka wapi? mwalimu anamakongamano na semina za wapi, nesi, askari polisi magereza jwtz hizo semina wanafanyia wapi? na watumishi wengine wengi hizo posho wanazipata wapi?

Kweli lakini mzee!!:clap2::clap2:
 
Mnacheza na watumishi wa umma nyie... wana maganji kibao, maposho, vikao, semina, warsha, kongamano... vyote hivyo ukivijumuisha kwa mwezi ni mara mbili ya mshahara wake... kuna wengine hata mshahara hawautumii, tena na kujenga wanajenga...

Pole sana kwa kuangalia kundi dogo la watumishi wa umma.Unafahamu kuwa walimu,wauguzi,madaktari,watendaji wa vijiji/mitaa/kata nao ni watumishi wa umma?Hawa wana marupurupu gani?
 
Mnacheza na watumishi wa umma nyie... wana maganji kibao, maposho, vikao, semina, warsha, kongamano... vyote hivyo ukivijumuisha kwa mwezi ni mara mbili ya mshahara wake... kuna wengine hata mshahara hawautumii, tena na kujenga wanajenga...

Wewe tangu lini polisi na waalimu wanapewa posho ya aina hio? Hapa umedanganya nadhani. Safari na semina wapate kutoka wapi?
 
Mnacheza na watumishi wa umma nyie... wana maganji kibao, maposho, vikao, semina, warsha, kongamano... vyote hivyo ukivijumuisha kwa mwezi ni mara mbili ya mshahara wake... kuna wengine hata mshahara hawautumii, tena na kujenga wanajenga...

Mimi ni mtumishi wa umma na tena ni Mhasibu, hapa nazungumzia hasa wenye kima cha chini ambao ndio wengi na pia nakuakikishia posho yoyote wanayoipata. cashier wangu analipwa kiasi hicho na Meneja wangu analipwa posho ya simu ya mkononi Tsh.150,000 kwa mwezi.
Cashier huwa ananung'unika nanukuu "yaani posho yake moja tu ni zaidi ya net pay yangu bado posho nyingine sijui ni lini mimi niatendelea nchi hii sijui kama tutafika"
 
Wafute huu utaratibu wa posho/walipwe mishahara. Huu ni ubadhirifu. Hata hivyo, nadhani huu utaratibu wa matabaka wa kupeana posho kimsingi unalenga kuwagawa watumishi wa juu na wa chini kwa malengo ambayo ni dhahiri ...
 
Serikalini WENYE MBWA ndo wanamaposho ya kufa mtu.yani mpaka posho zingine huwa wanasahau kuziclaim mpaka wakumbushwe.lakini MBWA wenyenye (watendaji) wana hali mbaya kuliko.yani ukifuatilia magumashi wanayofanya ili kusurvive utachoka mwenyewe
 
Mimi nashauri wachangiaji muelewe, wanafunzi chuo waligoma na madai yao yameonekana, mnataka wawagomee wafanya kazi wa uma? Si wa gome nao sihiyo ni haki yao. Nchi imeoza kila mahali kwani mnafikiri pesa haipo. Swala nikila mtu aamke kudai haki yake na hapo ndipo nguvu ya uma itonekana!
 
Pamekuwa na habari kuwa hali inazidi kuwa si nzuri serikalini na hasa watumishi wenye mishahara midogo kwani serikali haina pesa nafasi za posho kuongeza kipato hakuna.

Hatari ninayoiona na inabidi kuchangia mawazo ni kurudi enzi za mwinyi yaani walioko serikalini kuanza kurudi kwa kasi private sector na maana yake private sector wataanza kutoa ujira mdogo kwani ukilenga maslah mazuri wapo watu kama wewe watafanya kazi hizo na maana yake thaman ya elimu itashuka kuliko sasa.

Tatizo la ajira litakuwa kubwa kuliko sasa hiyo shift of labour ikianza.

Kuna hatari naiona inakuja wakuu.
 
Mnacheza na watumishi wa umma nyie... wana maganji kibao, maposho, vikao, semina, warsha, kongamano... vyote hivyo ukivijumuisha kwa mwezi ni mara mbili ya mshahara wake... kuna wengine hata mshahara hawautumii, tena na kujenga wanajenga...

Wewe!! We lazima utakuwa mtoto wa fisadi wewe!!!! Au la we mwenyewe ni fisadi wewe!!!

Ungekuwa ni mwalimu wa sekondari ya kata usingeandika uliyoyaandika hapa jamvini!!!

We unaangalia maisha ya `shemeji` yako anayefanya kazi ikulu unaleta kwa waliochoka?
 
wengi wanaishi kwa magumashi...na ndio maana huwa nasema nchii hii haiwezi kufanya mambo waliyofanya wamisri...juzi tukta wakatangaza mgomo wa kupinga ongezeko la umeme....badae wakasogeza mbele...imeenda weeee mwisho wakaahirisha kabisa.....

hiki kilichotokea g'mboto na wahanga kuwekwa pale uwanja wa uhuru ndipo palikuwa mahali pa kutokea wote tungejaa pale ...kwanza kushinikiza waziri wa ulinzi aachie ngazi , mwamunyange na mwisho kumtaka kikwete aondoke madarakani...badala yake watu wanalilia nyjma ya kii bodi zao......
leo huwezi kuwakusanya eti waandamane...hakika hakuna atakayejitokeza.....
 
Back
Top Bottom