Watumishi wa serikali wapya 3000 waliofukuzwa kazi wapanga kufungua kesi mahakamani

nkanga chief

JF-Expert Member
May 31, 2016
2,084
1,620
Watumishi wapya walioajiriwa mwezi June 2016 kisha kusainishwa mikataba ya kazi na kuanza kufanya kazi baaadaye walifukuzwa kazi bila kufata utaratibu wanatarajia kufungua kesi kesho kuishitaki serikali kwa kitendo ilichowafanyia serikali imewafukuza kazi waajiriwa wapya wa mahakama ,Afya, mikoani ,wilayani nk akiongea mwenyekiti msaidizi wa wahanga hao deus mweseka ,amesema kuwa wamejipanga vya kutosha kukabiliana na kesi hiyo ili kutafuta haki yao maana wamefukuzwa kazi bila kuambia hata sababu ya kwanini wamefukuzwa kazi wakati wana mikataba ya kazi na barua za kuitwa vituoni kazini amesema tangu wafukuzwe kazi Leo huu ni mwezi wa sita wapo nyumbani amesema anashangazwa na serikali hii kushindwa kufuta sheria na taratibu za utumishi wa umma .

Mwenyekiti msaidizi huyo ameiomba Mahakama kuwatendea haki maana wameitafuta haki kwa njia ya mazungumzo imeshindikana kupatikana kabisa amesema wameonana na katibu mkuu utumishi wa umma juu ya kurudishwa kazini lakini naye hakuwa na majibu alisema hilo swala lipo juu ya uwezo wao lipo chini ya rais magufuli pia Waziri kairuki alisema nae kuwa hill zoezi la watu kurudishwa kazini lipo chini ya rais na wao utumishi wanategemea kibali ,mwenyekiti huyo alisema njia sasa ya kutafuta suruhu juu ya swala hilo ni Mahakama pekee.
 
BWANA YULE.


SWISSME
Si kweli, mimi nina wahusika wa karibu na wameambiwa wasubiri. Huwezi kusema umefukuzwa kazi bila kuambiwa. Kesi ya msingi ingekuwa kuajiriwa na kutokulipwa mshahara.
 
Wangejitahidi pia kupata barua yakufukuzwa ili wawe na base grounds za madai
 
Back
Top Bottom