Watumishi wa serikali wanasababisha serikali ichukiwe na Wananchi

ungonella wa ukweli

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
4,210
555
Wakuu habarini zenu, kuna Walimu wanaosubiri kulipwa madirishani hapa wilayani Mbinga, walimu hao hawakuingiziwa mishahara yao kwenye Akaunti zao, kwa vile ni wapya. Tangu leo asubuhi mpaka sasa wanazungushwa tu na maafisa masuhuri hapa wilayani, mara wanaambiwa wasubiri hakuna kinachoeleweka! Wadau nimegundua maafisa waandamizi wengi serikalini ndio maadui wakubwa wa serikali na ndo wanaosababisha wananchi waichukie serikali yao! Naona wengi hawawajali wananchi kwenye sekta zao za utumishi.

Mytake:
Kama serikali inapenda iendelee kuheshimiwa ni vema ikawadhibiti wafanyakazi wa serikali wanaotumia ofisi kama mali yao binafsi! Vinginevyo serikali ya CCM siku zake zinahesabiwa!
 
Taswila ya chama lazima ionekane kwa serikali, serikali nayo taswila yake huaksi wafanyakazi kwenye ofisi zake. Mtoto wa nyoka nae nyoka!wafanyakazi kwenye ofisi ya fisadi nao watakuwa na tabia ya ufisadi,kama chama katili, serikali itakuwa katili na wafanyakazi pia, The whole system looks like that and moves in a so parabolic way, impotent gvt...
 
That is true.
 
Serikali ni kweli isipokuwa makini itachukiwa sana kwa sababu ya ulevi wa watumishi katika idara mbalimbali, ccm nadhani inabidi iondoke madarakani haraka kwa sababu za kushindwa kuisimamia serikali yake!
 
Kaka hilo ni tatizo la halmashaur zote, na hiyo ndiyo dalil ya kushindwa kwa serikal yetu. Maofisin saa tano ndio mwisho, baada ya hapo maofisa wanakuwa wapo bar wanakula walivyovuna kwa rushwa. La msingi km ataweza kupatikana mwandish wa habar mpen hzo taarifa ili watanzia wajuie nch inavyopotea. Zaid sn jaribun kumwona DED au DC km wataweza kutoa msaada. Wakishindwa toeni uamuz mgum
 
ni kweli mkuu umemshauri vema,kama vipi nendeni kwa Ded ama mkuu wa wilaya, serikali hii ni corrupt!
 
Hakuna shaka yoyote katika halmashauri nyingi viongozi waandamizi wamekuwa wakishirikiana na wahasibu kunyanyasa sana watumishi wa kada za chini yao,na hasa walimu na watumishi wa idara ya afya.Ni kawaida kukuta mtumishi anadai haki yake hadi analazimika kutoa chochote kitu kwa mhasibu ili tu apatiwe haki yake.Tena unakuta hazina wameshatuma fedha siku nyingi lakini fedha hizo kutoka kwenda kwa muhusika inakuwa usumbufu ajabu.Halafu akija mtu kama Mwanry anafoka utadhani leo ndo leo!Lol;kumbe wapi bhana,jamaa ni mkwara mdomoni tu vitendo ziro!Matokeo yake ndo hayo tunaamini hawa wakubwa huko serikalini wanahusika kuwapa kiburi watendaji wilayani.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
"Hii ndo Tanzania wagonjwa wanafia mapokezi kisa wanataka rushwa", kwanini serikali isilaumiwe maana serikali ndo ina mamlaka yote ya nchi na watumishi ni zao la serikali.
 
Wakuu habarini zenu, kuna Walimu wanaosubiri kulipwa madirishani hapa wilayani Mbinga, walimu hao hawakuingiziwa mishahara yao kwenye Akaunti zao, kwa vile ni wapya. Tangu leo asubuhi mpaka sasa wanazungushwa tu na maafisa masuhuri hapa wilayani, mara wanaambiwa wasubiri hakuna kinachoeleweka! Wadau nimegundua maafisa waandamizi wengi serikalini ndio maadui wakubwa wa serikali na ndo wanaosababisha wananchi waichukie serikali yao! Naona wengi hawawajali wananchi kwenye sekta zao za utumishi.

Mytake:
Kama serikali inapenda iendelee kuheshimiwa ni vema ikawadhibiti wafanyakazi wa serikali wanaotumia ofisi kama mali yao binafsi! Vinginevyo serikali ya CCM siku zake zinahesabiwa!

Kwenye ukweri hakuna budi kuukubali uo ukweri,ukifanya tofauti na ukweri ulivyo subiri hukumu ya ukweri kwakuwa utabaki kama ulivyo ni ukweri.ulichosema ni ukweri mtupu.
 
Back
Top Bottom