Watumishi wa Serikali tuige ya Wabunge wetu.

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Nimesika leo wabunge wakisema walikubali kutoa posho zao za siku moja ili kuchangia maafa ya tetemeko la ardhi Bukoba,Hongereni sana kwa hilo.

Naona ingekua vizuri pia watumishi wengine wa serikali kama vile police,drs,walimu...nk nao waige mfano wa wabunge na kukubali kuchangia/kukatwa fedha kutoka kwenye mishahara yao ili kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi Bukoba.
 
Hao walimu uliowataja wana posho kama wabunge?
Kumbuka wabunge wamechangia posho yao ya siku moja sio mshahara sasa hivi hao walimu wanaposho?
 
Eish! Sijisikii kusema vibaya leo, ngoja nijitahidi..... Watulipe posho on time kama wanavyo wapa wanasiasa ili tupate za kuchanga. nasema kwa upande wangu.
 
................ nashindwa kuandika maneno mazito hapa. ila hii post imenifanya nijiskie vibaya sana, ngoja niweke sawa vyeti vyangu kwa ajili ya kuhakikiwa kwa mara ya tatu.
Nimesika leo wabunge wakisema walikubali kutoa posho zao za siku moja ili kuchangia maafa ya tetemeko la ardhi Bukoba,Hongereni sana kwa hilo.

Naona ingekua vizuri pia watumishi wengine wa serikali kama vile police,drs,walimu...nk nao waige mfano wa wabunge na kukubali kuchangia/kukatwa fedha kutoka kwenye mishahara yao ili kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi Bukoba.
 
Hao watumishi wenyewe wamechoka wanadaiwa kila kona Majirani,ndugu,mabenki,wafanyakazi wenzao,waleta biashra majumbani na maduka yote mitaani halafu unataka wachangie? Sasa kile kitenge cha maafa kimefanya nini mpaka sasa? unaonaje Rais,Makamu,Waziri mkuu na mawaziri wote wakafanya hivyo manake mishahara yao minono kuliko hata hawa masikini mishahara yao haiwatoshi.
 
Back
Top Bottom