Watumishi wa Halmashauri ambao bado hawajahamia makazi mapya watakiwa kuondoka mara moja

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameagiza Watumishi wa Halmashauri ambao wametakiwa kuhamia makazi mapya na hawajafanya hivyo kuondoka mara moja.

Amesema "Kipindi cha kuondoka kilishatamkwa na Rais kwahiyo hatuna sababu ya kuwapa muda tena. Endapo hawatafanya hivyo, Mkuu wa Mkoa husika achukue hatua mara moja dhidi ya Watumishi hao".

Kauli ya Majaliwa inakuja baada ya Mbunge Joseph Kasheku kuhoji kauli ya Serikali kuhusu Halmashauri ambazo zimehamisha Ofisi Vijijini lakini Watumishi bado wanarudi kulala Mjini hata kama walipohamia kuna nyumba, hali inayoleta mzigo wa kugharamia mafuta kila siku.

Amesema, Novemba 2019 Rais Magufuli aliagiza Halmashauri za Vijijini zinazokaa Mjini kurejea maeneo husika ndani ya siku 30 ili kuhudumia Wananchi kwa karibu.
 
Hiki kikijamaa kinaangalia sana maslahi yake
Nasikia huko halimashaur "vijijin" amejenga huko vinyumba vya kupangisha ndio maana anakomaa watumish wakakae huko..

Kama mtumish anaripoti kazini kama sheria inavotaka shida ipo wap

Mtu utoke Geita mjini ukapange kwa msukuma

Jitu binafsi sijawah ona..
 
Back
Top Bottom