wankuru nyankuru
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 490
- 763
Watumishi wengi ukiachana na walimu wamekuwa wakitumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii wakichati na wengine wakirusha picha kwenye status za WhatsApp.
Wengine utawakuta Instagram, mara Facebook huo ni muda wa kazi .
Sasa unabaki kujiuliza hivi huyu mtumishi anafanya kazi muda gani?
Na hawa ndio ikifika may mosi wananyanyua mabango wakidai kuongezewa mishahara na kupandishwa madaraja na kudai allowance mbali mbali zikiwemo house allowance, communication allowance, electricity allowance n.k.
Namshauri yafuatayo Mzee wetu mzalendo nambari moja Dr Magufuli.
1. Tathimini ya kina ifanyike kwa watumishi wote wa umma kama kweli wanalipwa mshahara kulingana na majukumu yao.
2. OPRAS ya makaratasi iliyopo sasa ifanyiwe maboresho na iwe ya ki electronics ambayo mtumishi ataweza kujaza majukumu yake tarajiwa kwa mwaka wa fedha husika, utekelezaji wa majukumu kwa siku, kwa mwezi,kwa robo mwaka na hadi mwaka. ( hii itasaidia kujua uhaliasia wa mipango inayopangwa).
3.OPRAS iunganishwe na mifumo ya ya bajeti ya Serikali kuu na Serikali za mitaa ( mifumo iwasiliane).
4. Faida ya kuwa na electronic OPRAS itasaidia kutrack add hoc overtime vile vile kutrack extra duties zisizokuwa na uhalisia ambazo mara nyingi utakuta mtumishi anazidai kwa justification za uongo.
5. Kumekuwepo na tabia ya baadhi ya viongozi kupewa communication allowance kila mwezi lakini hawazitumii ipasavyo badala yake maafisa na watumishi wa kada za chini wasiopewa hizo fedha hutumia fedha zao kuwasiliana ( kuratibu) na watumishi wenzao pindi wanapohitaji kujua mambo kadhaa. Kuna haja ya Serikali kuweka system ya kutrack matumizi halisi ya hizi fedha za mawasiliano Kwa wakuu wa idara.
6. Na mwisho kabisa nimpongeze mh Rais wetu Dr Magufuli kwa maamuzi yake ya kishujaa aliyofanya kwa kutujengea sisi watanzania wa hali ya chini hospitali za wilaya zaidi ya 60 na vituo vya afya na zahanati nyingi ndani ya miaka 4. Tena kwa fedha za ndani. Fedha ambazo zilikuwa zikipotea kwa udanganyifu mbali mbali.
Karibu kwa machango wenu wa kujenga tu na sio matusi .