Watumishi Mliosema upinzani wa kazi gani Tanzania natumai mmeona wabunge wa CCM wanavyowapigania Bungeni.

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Kuna mtumishi mmoja analalamika kwanini upandishaji mishahara umekuwa wa hisani ya Mhe. Rais nikamwambia akamuulize Mbunge wake aliyempeleka Bungeni. Nimemjibu hivyo Kwa sababu awali enzi ya JK alikuwa anawaona wapinzani Bungeni kama watu wasio na uchungu na nchi hii na wasiofaa kuwepo.

Baada ya wapinzani kuondolewa kama alivyokuwa anaombea amebadilika anajiuliza wabunge wa CCM wanafanya kazi gani Bungeni? Nadhani Kila anayeona kwamba mazingira ya haki nchini siyo ya wazi na hisani zimekuwa nyingi anapaswa kuelewa nchi inahitaji katiba Bora na siasa safi. Hakuna nchi Duniani inaweza mpata Rais Bora, mfumo sahihi wa maishi unatoka KWENYE katiba yenye kumpa mamlaka mwananchi. Kenya Mhe. Rais awezi kushindana na katiba, alijaribu kuibadilisha akakataliwa maana yake yeye yupo chini ya Katiba. South Afrika hakuna ujanja ujanja, Mhe Rais akitoa ahadi zisizokidhi anahojiwa na wanachi kupitia maandamano nk.

Tukubali Watumishi wa Umma mnatakiwa kwenda kumlilia mliyempa kula, Siku mkutofautisha Kati ya kula la kura mtashiriki kutafuta mfumo sahihi wakuwapatia watu wakuwapigia kura kura siyo watu wakupewa Nafasi ya kula

Mhe. Rais wa Sasa anaeleza facts, anaeleza ukweli kwamba amepokea nchi ikiwa hoi kiuchumi, inahitaji miujiza au kujitoa ufahamu Kwa Rais kuwapendelea wafanyakazi akawaacha Wananchi walio wengi bila Huduma. Endeleeni kuisifia hotuba ya Kenya ila mtaendelea kulipwa kulingana na uwezo wa kiuchumi . Hongera mama, walipokosea 2015 wakaweka mfumo wakuuwa uchumi walidhani wanawakomesha wapinzani kumbe wanajikomoa.
 
Tukubali Watumishi wa Umma mnatakiwa kwenda kumlilia mliyempa kula, Siku mkutofautisha Kati ya kula la kura mtashiriki kutafuta mfumo sahihi wakuwapatia watu wakuwapigia kura kura siyo watu wakupewa Nafasi ya kula
Elimu... Elimu... Elimu!

ccm imebemenda elimu na uwezo wa common wananchi. Pamoja na kwamba hawaelewi kilichozungumzwa lakini bado watapiga makofi, vifijo na nderemo!
Screenshot_20220502-003402.png
 
Back
Top Bottom