Watumishi Manispaa ya IRINGA walazimishwa kuwa na kadi za CCM kama kigezo cha kupandishwa madaraja ya kazi....

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,632
2,413
Wadau huku kwetu Iringa tunazidi kuvurugwa kila siku tokea aletwe huyu kada wa CCM kama RC wa Iringa..Ukiachilia mbali bendera za CCM zililizozagaa kwa wingi kwa sasa hapa mjini katika baadhi ya nyumba zilizo pembezoni mwa barabara kuu za mji ama kwa wenye nyumba hizo kupenda au kulazimishwa hapo sijui lakini jambo linalosikitisha kwa sasa ni huu unyanyasaji unaowakumba kwa sasa wana Iringa katika hali ile hali ya kuwalazimisha kukiunga mkuno chama tawala.

1. Katika ofisi za Manispaa wafanyakazi woote wa vitengo muhimu wameambiwa kuwa kama hawana kadi za CCM hawatapanda madaraja ya kazi au kupata "promotion" yoyote kazini
2. Kuna mikopo mbali mbali inayotolewa sasa kwa wajasiriamali hasa wanawake na vijana..Kigezo kimojwapo kilichowekwa ni kwamba kipaumbele ni kwa wale wenye kadi ya CCM.

Hapa kazi tu!
 
acha uongo mm nipo hapa iringa napiga kazi na sina kadi ya chama chochote na naona watu wanapandishwa madaraja kila leo
Uliwahi wapi kusikia muumini mtiifu wa dini fulani akikana matendo maovu yanayofanywa na viongozi wa dini yake?
 
Ha ha haaa, mkuu yupo huko kazi maalumu tu ila kiwiliwi kipo chama Dola.
Bado ni mtumishi wa serikali analipwa stahiki na marupurupu kama sheria inavoeleza.
Hivyo bado Ukiwa CCM mambo yako yanaenda vyema.

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah! Hii ndio dosari kubwa sana katika mfumo wetu wa kiutawala na kisiasa. Mtu akiwa analipwa mshahara na dola(baada ya kustaafu utumishi wa umma) lazima awe na mafungamano na chama tawala. Bahati mbaya sana vyama vya upinzani havielewi hilo
 
acha uongo mm nipo hapa iringa napiga kazi na sina kadi ya chama chochote na naona watu wanapandishwa madaraja kila leo

Kwenye suala la vitambulisho upo Moshi na kwenye halmashauri upo Iringa. Naamini ccm usipokuwa muongo unafukuzwa uwanachama; otherwise kwa nini kila kimtokacho mlumumba laziwe kiwe na elements za uongo? Na hii ni kuanzia mwenyekiti wa taifa down to the last person.
 
Dah! Hii ndio dosari kubwa sana katika mfumo wetu wa kiutawala na kisiasa. Mtu akiwa analipwa mshahara na dola(baada ya kustaafu utumishi wa umma) lazima awe na mafungamano na chama tawala. Bahati mbaya sana vyama vya upinzani havielewi hilo
Mi siamini eti mtu kama yule ni mpinzani wa ukweli.
Siku wakianza kuwekwa ndani nao miezi miwili ntaanza kuona upinzani wao halisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kuku mmoja wa Lumumba alisema polepole kawaambia watoe kadi za uana chama baada ya kuwapiga semina.
 
Wadau huku kwetu Iringa tunazidi kuvurugwa kila siku tokea aletwe huyu kada wa CCM kama RC wa Iringa..Ukiachilia mbali bendera za CCM zililizozagaa kwa wingi kwa sasa hapa mjini katika baadhi ya nyumba zilizo pembezoni mwa barabara kuu za mji ama kwa wenye nyumba hizo kupenda au kulazimishwa hapo sijui lakini jambo linalosikitisha kwa sasa ni huu unyanyasaji unaowakumba kwa sasa wana Iringa katika hali ile hali ya kuwalazimisha kukiunga mkuno chama tawala.

1. Katika ofisi za Manispaa wafanyakazi woote wa vitengo muhimu wameambiwa kuwa kama hawana kadi za CCM hawatapanda madaraja ya kazi au kupata "promotion" yoyote kazini
2. Kuna mikopo mbali mbali inayotolewa sasa kwa wajasiriamali hasa wanawake na vijana..Kigezo kimojwapo kilichowekwa ni kwamba kipaumbele ni kwa wale wenye kadi ya CCM.

Hapa kazi tu!
Sio mpya zamani ilikuwa huwezi kuendelea kusoma au kupata ajira popote kama huna kadi ya ccm, historia hujirudiaaaa
 
Back
Top Bottom