Watumishi katika Jeshi la Polisi mnahitaji mjitafakari

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,944
18,653
Nimekuwa nikikutana na watu mabalimbali ambao wameajiriwa katika jeshi ya police. Maana yao wengi na maasikari.

Hawa watu tunapozungumza nao kiurafiki wanalalamikia hali za uchumi na mazingira yao ya kazi. Nimekutanaa na wengi wanaolalamiki uchumi, vyuma kukaza,, mishahara na mazingira mabovu ya kazi. Yani hata kabla hujamuuliza anaanza kukuambia mwenyewe kuwa hali ilivyo ngumu.

Sasa kinachonishangaza. Hawa hawa wanaolalamika hali ni ngumu, wapo tiyari kuwapiga kipigo cha mbwa koko wanaotetea maslahi yao huku wakitumia nguvu nyingi kuwalinda na kuwakingia kifua wanaomimya maslai yao.

Hii hata haihitaji elimu ya chuo kikuu kuelewa. Mnahitaji na nyie mjitafakari kama mnachofanya kinamanufaa katika jamii zenu, vizazi vyenu na nyinyi binafsi.

Nimeandika hii sababu nakereka kila napokutana na asikari tukipiga stori kidogo tu lazima alalamike vyuma vimekaza wakati alayevikaza wanamjua na wanamkingia kifua. Huu nao ni ujinga uliopitiliza.
 
Kuna Mmoja alikuwa Ni Mfuasi Lia Lia wa Mbowe na CDM
lakini ajabu siku Ambayo Mbowe Anaenda Lupango,Yeye ndiye alikuwa wa kwaza kumzingua na kuonesha ubabe.

Askri wa ki,Africa Ni Kama Mazombie wanaishi kwa kuendeshwa.

Ni Mara kuwa mtumwa ulaya kuliko kuwa Askari Africa
 
Askari tunaokutana nao ni wale wadogo (was chini) ambao wanatekeleza maagizo toka juu kwa wakubwa wao walio karibu na viongozi wa kisiasa ambao wanafaidi keki ya taiga hill LA wanyonge. Wakubwa wao wakati wote wako Ikulu au na wateule wakila bata. Wadogo wanamalizia hasira zao kwa wananchi kwa kuwapiga mpaka wachakae. Kuna Sikh watasema enough is enough.
 
Polisi Wana mshahara mzuri na posho ya laki tatu kila katikati ya mwezi. Maana ya kuwa mtumishi maana yake ni mtumwa. Mtumishi ni neno la kistaarabu kuficha neno mtumwa. Kwahiyo mtu ukitaka kupata hela au maisha unayoyahit Kwa mtumishi mahali pepote Dunia sio rahisi kihivyo kufanikiwa. Njia rahisi ni kujiunga kufanya shuguli binafsi mfano businesses, kilimo na ujasiliamali. Usitegemee mtumishi awe tajiri labda awe mwizi ambapo Kwa nchi zilizoendelea kuiba inakuwa ngumu Sana na ikigundulika unashtakiwa hata kama ukiwa Rais . Kumbuka Rais mstaafu wa Peru wa aliyejipa risasi kuepuka kuja kukamatwa.
 
Muulize kwanza ana cheo gani. Kuna ngaz hawez tamka hilo. Pia ujue askar anafata amri ya mkubwa wake. Ndio nature ya kiapo. Na hata uwe na haki kias gan bado utalazimika kuheshim sheria, kanun na taratib. Yan hakuna haki bila wajib.
 
wakigomea hizo amri sasa si watakua matatani?, alafu maisha yao yatakuwa magumu zaidi. wakulaumiwa ni viongozi waandamizi ya polisi IGP na timu yake, wao wanao uwezo wa kugomea ujinga lakini hawafanyi hivyo.
 
Hiyo inatokana na Mkuu wa nchi kuwa ndiye Amiri Jeshi Mkuu

Inapotokea nchi kwa Bahati mbaya inapata kiongozi ambaye "amefyatuka" ndiyo hali kama inayolikabili Taifa kwa hivi sasa
 
Muulize kwanza ana cheo gani. Kuna ngaz hawez tamka hilo. Pia ujue askar anafata amri ya mkubwa wake. Ndio nature ya kiapo. Na hata uwe na haki kias gan bado utalazimika kuheshim sheria, kanun na taratib. Yan hakuna haki bila wajib.
Hapa naongelea wenye vyeo vya chini au wasiokuwa na vyeo kabisa.
 
Zile hasira za kupihmga zinakuwa ni stress zao majumbani sio kazi inavyosema mm kuna mmoja nimemsikia akimwomba jamaa msamaha eti sory nilikuwa na mkuu ikabidi nifanye vile ili nisionekane laini laini oo broo yaishe bana yale yalikuwa mambo ya kazi
 
Polo mshahara wao ni laki 6

Nilidhani 1.5m kumbe ni laki 6? Hao polisi wenyewe ni nadra kuwa na familia ya watu chini ya watano@family, ukiigawa ni kama kila mtu anatumia laki kwa mwezi. Ingekuwaa wanalipwa 2m, hiyo kwenda kupiga watu si wangefanya mauji ya kimbari?
 
Hahaha eti mauaji ya kimbari
 
Nimekuwa nikikutana na watu mabalimbali ambao wameajiriwa katika jeshi ya police. Maana yao wengi na maasikari.

Hawa watu tunapozungumza nao kiurafiki wanalalamikia hali za uchumi na mazingira yao ya kazi. Nimekutanaa na wengi wanaolalamiki uchumi, vyuma kukaza,, mishahara na mazingira mabovu ya kazi. Yani hata kabla hujamuuliza anaanza kukuambia mwenyewe kuwa hali ilivyo ngumu.

Sasa kinachonishangaza. Hawa hawa wanaolalamika hali ni ngumu, wapo tiyari kuwapiga kipigo cha mbwa koko wanaotetea maslahi yao huku wakitumia nguvu nyingi kuwalinda na kuwakingia kifua wanaomimya maslai yao.

Hii hata haihitaji elimu ya chuo kikuu kuelewa. Mnahitaji na nyie mjitafakari kama mnachofanya kinamanufaa katika jamii zenu, vizazi vyenu na nyinyi binafsi.

Nimeandika hii sababu nakereka kila napokutana na asikari tukipiga stori kidogo tu lazima alalamike vyuma vimekaza wakati alayevikaza wanamjua na wanamkingia kifua. Huu nao ni ujinga uliopitiliza.
Hao ni wanafiki tu ,wanakudanganya ,mishahara wanapata na malupulupu yako vizuri sana, na kwa wakati.
Pesa wanayoikosa na kulalamika kwa baadhi ya hao askari ni ile waliokua wanaipata kwa kuvusha magendo,kubambika watu kesi ,kushiriki ujambazi,na kufanya biashara ya mihadarati.

Polisi ambao ni watiifu na wanaongozwa na maadili ya kazi wataendelea kutoa kipigo cha mbwa koko na kuchakaza kwa raia watakao kaidi na kutokutii sheria bila shuruti.
 
Back
Top Bottom