Watumishi hewa Arusha waongezeka, wafikia 300

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda amesema idadi ya watumishi hewa mkoani humo imeongezeka baada ya uchunguzi wa awali huku baadhi ya waliokuwa wakifuja fedha za serikali kwa kudanganya wakiomba kuzirejesha.

Aidha, amesema mkoa umepoteza Sh bilioni 1.8 kwa mwaka jana kutokana na kulipa watumishi hewa. Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Ntibenda alisema hivi sasa mkoa huo unafuatilia akaunti za watumishi hao hewa ili fedha hizo zirudishwe serikalini huku watumishi wengine baadhi waliokuwa wakifuja fedha za serikali kwa kudanganya wakiomba kuzirejesha.

Alisema awali wakati timu ya uchunguzi aliyoiunda kuchunguza watumishi hewa ilibaini mkoa huo kuwa na watumishi hewa 270, lakini hadi jana idadi hiyo imeongezeka na kufikia zaidi ya 300.

Alisema wilaya mbili za Karatu na Arumeru ndizo ambazo watumishi hewa wameongezeka. “Bado tunaendelea na uchunguzi na naamini wataongezeka lakini hivi sasa hao watumishi hewa wanahaha kurudisha fedha za serikali lakini hata kama wakirudisha watapelekwa mahakamani,” alisema Ntibenda.

Alisema hata kama fedha hizo watazirudisha, lakini watawafikisha mahakamani na pia wanafuatilia kujua ni kwa nini wakuu wa idara zao walifahamu udhaifu huo, lakini walikaa kimya na kuwalipa mishahara huku wakijua kuwa wanaihujumu serikali.

Alisisitiza ni vyema watu wakaacha tabia ya kujipatia fedha nyingi kwa njia isiyo halali kwani watumishi hewa wanasababisha fedha za serikali kushindwa kufanya shughuli nyingine badala yake kupata hasara.

Katikati ya mwezi uliopita, wakati akiwaapisha wakuu wa mikoa wapya, Rais John Magufuli aliagiza waende kufuatilia watumishi hewa katika mikoa yao na hadi sasa wamegundulika watumishi hewa zaidi ya 4,000.
 
kwa mwaka mmoja ni 1.8 b kwa miaka kumi ni 10.8 b hao wapo miaka mingi sio mwaka mmoja pekee...
 
Mmmh hawa ni multiple talents. Hvi unawezaje kujilipa mishahara kadhaa ukadhani utakuwa salama?
Ndio maana kada nyingine tukisema mishahara midogo hawa jamaa walikuwa hawatuelewi ila sasa naona tutaongea lugha moja.
Tumelalamika sana kodi kubwa posho hamna mazingira ya magumu ila who cares?
 
Safi sana Mkuu wa mkoa. Lakini nashauri tusiishie hapo. Kuna watu wako nyuma ya uozo huu. Nikuibie tu siri: Kuna maafisa utumishi/tawala ambao wanakagua payroll na kuidhinisha kila mwezi kabla ya mishahara kulipwa. Hawa wanapaswa kufukuzwa kazi. Huwezi kuendelea kuidhinisha mhahara wa mtumishi ambaye hayupo kazini na kuruhusu mshahara wake kuendelea kulipwa kwa zaidi ya mwaka! Hii haiwezi kuwa bahati mbaya. Pili, fedha hizo zilikuwa zinalipwa kwenye akaunti za watu (kwa mfumo wa ulipaji serikalini kwa sasa), je ni nani hao? Watafutwe na kushitakiwa mahakamani. Tatu, wafuatilie pia wakuu wa Idara zinazohusika. Kwa nini waliruhusu hali hii kuwepo? kazi yao ni nini? Ninavyofahamu, katika sehemu yoyote ya kazi, 50% au zaidi ya budget huwa ni kwa ajili ya personnel. Inashangaza kwamba unakuwa na mtu anaitwa DAP au RAS au DAS lakini hajui na hawezi kuthibiti 50% ya bajeti katika idara yake. Kwangu, mtu wa namna hii hapaswi hata kuwa na cheo hicho in the first place.
 
Ndugu yangu hii kitu imekuwa na mlolongo mpaka Utumishi. Kuna mbea aliwahi nidokeza kuwa mtandao umekuwepo kwa muda mrefu mpaka kwa ngazi za juu za OR Utumishi na Menejimenti ya Umma tangu enzi za kina Kombani na Ghasia.

Ushauri alioutoa Mbunge Ruth Mollel (CHADEMA ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu Utumishi ndiyo unatakiwa kufanyiwa kazi. Kubwa ni kutumia mifumo ya TEHAMA na ikihusisha idara kama NIDA, RITA na Benki.

Kwa kuanzia, serikali itoe vitambulisho vya Uraia kwa Watumishi wote wa serikali. Kisha kuwe na mfumo wa kuoanisha taarifa za mtu na ajira na malipo na namba yake ya uraia. Hilo ndiyi litakuwa suluhisho la kudumu.
 
Hiyo aya ya mwisho ndiyo ufumbuzi tu. Mengine ni kupoteza muda bure.
Hapo hata wenye kazi zaidi ya moja unawaona kirahisi tu.
 
Kwa mwendo huu tunakwenda kuwa na serikali yenye adabu kabisa hasa kwa watumishi wa umma kazeni kama wakuu wa mikoa na wilaya tujenge taifa lenye nidhamu.
 
Ndugu yangu hii kitu imekuwa na mlolongo mpaka Utumishi. Kuna mbea aliwahi nidokeza kuwa mtandao umekuwepo kwa muda mrefu mpaka kwa ngazi za juu za OR Utumishi na Menejimenti ya Umma tangu enzi za kina Kombani na Ghasia.

Ushauri alioutoa Mbunge Ruth Mollel (CHADEMA ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu Utumishi ndiyo unatakiwa kufanyiwa kazi. Kubwa ni kutumia mifumo ya TEHAMA na ikihusisha idara kama NIDA, RITA na Benki.

Kwa kuanzia, serikali itoe vitambulisho vya Uraia kwa Watumishi wote wa serikali. Kisha kuwe na mfumo wa kuoanisha taarifa za mtu na ajira na malipo na namba yake ya uraia. Hilo ndiyi litakuwa suluhisho la kudumu.

Yes, nakubaliana na wewe kuhusu hatua za kuchukua ili kurekebisha mambo. lakini, bila kuwachukulia hatua kali wanaofanya mchezo huu mambo hayawezi kukaa sawa. Tunaleana mno kwenye serikali yetu ndiyo maana uchafu hauishi. Hata ukileta mifumo mipya kama hakuna kuwajibishana, wajinga wachache wataichezea tu. Kwenye sekta binafsi kuna 0-tolerance, ukiruhusu mtumishi hewa tu kwa mwezi mmoja, you lose your job. Ndiyo maana hakuna uchafu huu. lakini kwenye Govt, kila siku ni story, story tu.... kama vile wanaofanya michezo hii hawajulikani.
 
kwa style hii ni dhahiri serikali yetu ilikuwa dhaifu sana,kulipwa bure wakati kuna watu wafuja jasho malipo kidogo
 
Back
Top Bottom