Watumishi hewa 46 wabainika mkoani Katavi, waisababishia serikali hasara ya zaidi ya Milioni 200

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481
Serikali mkoani Katavi imebaini uwepo wa wafanyakazi hewa 46 ambao wameisababishia serikali hasara ya zaidi ya shilingi milioni mia mbili.
Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari mkoani hapa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mhuga amesema wamebaini uwepo wa wafanyakazi hewa katika Halmashauri zote nne za mkoa huu.

Kufuatia uwepo wa watumishi hewa, Mkuu huyo wa Mkoa wa Katavi amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri hizo kuhakikisha fedha zote zilizolipwa katika mishahara ya watumishi hewa zinarejeshwa ndani ya siku 21 sanjari na kuwawajibisha maafisa utumishi.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ametoa wito kwa watumishi wa umma kufanya kazi kwa uadilifu na kufuata kanuni taratibu na sheria za utumishi wa umma.

Chanzo: IPP Media
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Back
Top Bottom