Watumishi hawa wa serikali ndiyo wameipotezea mvuto CCM

DT125

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
378
571
Baadhi ya viongozi wa juu wa CCM kwa kutoelewa au kwa makusudi na chuki binafsi waliendesha zengwe la kuwashambulia na kuwabatiza wenzao Mapacha watatu na kuwafanya kuonekana kama ndio wamefanya CCM kupoteza mvuto kwa wananchi. Viongozi wanaoipotezea mvuto CCM ni hawa wafuatao;
  1. Watendaji wa vijijini na kata ,mahakimu wa mwanzo, waganga na manesi wa zahanati, walimu wa shule za msingi na sekondari wasotimiza wajibu wao kwa haki, kwa wakati na bila choyo, chuki, upendeleo na kupenda rushwa. Hawa ndio huhudumia kundi kubwa la watanzania.
  2. Idara mbalimbali za serikali zinazotoa huduma kwa wananchi kama TRA, Shirika la Reli, watumishi wa hospitali za wilaya na mikoa, mahakama nchini, Bandari, watumishi wa Halmashauri za serikali za mitaa, polisi, magereza n.k
Kama makundi ya watumishi hawa hayawajibiki ipasavyo kwa, mfano unakuta utaratibu wa kupata huduma umebadikwa katika kuta za ofisi na umetimiza masharti yote lakini huduma hakuna aidha mtoa huduma yahupo siku nzima au wiki, yupo lakini hakuhudumii mpaka umpe rushwa, huduma zinatolewa kwa upendeleo hata mkifukuzana wanachama bila kurekebisha hali hizi hakuweze kurudisha mvuto kwa CCM.

Ni lazima CCM kama wanataka kurejesha mvuto wake wa kukubalika kwa wananchi ni lazima serikali yake iweke mfumo utakaoboresha utoaji huduma mzuri kwa watanzania. Sio dhana ya kujivua gamba.
 
Umesahau na wanachama. Wanalamba rushwa kama hawaelewi. Wameshawajulia Takuruku.
 
kwa hiyo kipindi cha mkapa,mwinyi na nyerere walikuwa wanawajibika au?si ndio hawa hawa waliitwa mbayuwayu!!!
kama hawapewi maslahi yao kwa wakati unategemea nini?

chama kimepoteza mvuto kwa kukumbatia wafanyabiashara na mafisadi na kuwaacha wakulima na wafanyakazi.acha kupotosha umma kama wewe ni gamba lazima uvuke.mkishindwa kuvuana mtavuliwa na wananchi ebo!!
 
Kwa hiyo tatizo ni CCM kwa ujumla na wanatakiwa wakabidhi nchi kwa wenye uwezo wa kusimamia haya yote!
 
Kwani hao watumishi wa serikali wamekuwepo leo? wapo tokea enzi za mwalimu. Tatizo wao hufanya kazi kwa kutekeleza maamuzi ya wanasiasa. kama chama hakina sera nzuri basi watapoteza mvuo. kikiingia madarakani chama chenye sera safi zitatekelezwa na hao hao watumishi. sioni kosa kwa hao watumishi tena muwatake radhia hapaapa jamvini.
 
Ndugu yangu kuna wafanyakazi wanalipwa vizuri kama hawa wa TRA lakini utoaji wao huduma ni mbovu ajabu, nimefatilia leseni wamenizungusha kuliko hata polisi traffic wanaolipwa kiduchu. Wakulima wanatakiwa kukumbatiwa kwa kupatiwa huduma bora na kwa wakati na watumishi hawa wa serikali hii ya CCM. Lakini Naheshimu mawazo yako Meningitis, mie sio Gamba ndugu yangu.[o
kwa hiyo kipindi cha mkapa,mwinyi na nyerere walikuwa wanawajibika au?si ndio hawa hawa waliitwa mbayuwayu!!!
kama hawapewi maslahi yao kwa wakati unategemea nini?

chama kimepoteza mvuto kwa kukumbatia wafanyabiashara na mafisadi na kuwaacha wakulima na wafanyakazi.acha kupotosha umma kama wewe ni gamba lazima uvuke.mkishindwa kuvuana mtavuliwa na wananchi ebo!!
 
labda wamepoteza mvuto kwa kikwete, tena kutokana na mahubiri haya xmass na pasaka. Lkn akimaliza jk tu, ccm itakuja kwa kasi ya ajabu na cahadema itakufa ziiiiiiii
Huwa ni nn kinawasukuma kutabiri? yaani nn kinawasaidia kufanya utabiri?
 
Kwani wakati wa mkapa hawa wafanyakazi na mashirika unayoyasema hayakuwepo? Hapa ni mtu mmoja tu jk ndiye aliyekiponza chama.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom