Watumishi ardhi Jiji Mwanza linawaliza wananchi viwanja

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
Watumishi ardhi Jiji Mwanza linawaliza wananchi viwanja

JIJI la Mwanza linatuhumiwa kudhurumu viwanja vya familia ya Marehemu Hassan Seif, Mkazi wa Nera wilayani Nyamagana mkoani Mwanza vilivyomilikiwa na familia hiuo tangu mwaka 1984.

Viwanja vilivyochukuliwa na Jiji na kuviuza kwa watu wengine ambavyo ni mali ya familia Marehemu Hassan Seif ni namba 195 - 201 vilivyopo Miembeni Isamilo jijini Mwanza.

Mtoto wa marehemu Hassan Seif, Abbakar Seif ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa Nera, amesema anasikitishwa kuona tangu mwaka 1984 familia yao ikishindwa kupata haki yao licha ya kupewa haki Mahakama.

Amesema Mwaka 1987 mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mwanza ilitoa hukumu iliyowapa haki ya kumiliki eneo hilo lenye viwanja 10.

Amesema licha ya hukumu hiyo ya mahakama kutoa agizo la wao kumilikishwa viwanja hivyo lakini mpaka leo jiji la Mwanza limeshindwa kutekeleza hukumu hiyo.

Amesema viwanja hivyo, vyote vimeuzwa na mtu mmoja aliyefahamika kwa jinaa Ally Salehe aliyeshirikiana na baadhi ya watendaji wa jiji la Mwanza.

Baadhi ya watumishi walioshirikiana na Salehe kuuza viwanja hivyo ni watumishi wa idara ya ardhi wakiongozwa na aliyekuwa afisa ardhi jiji ambaye kwa sasa amehamishiwa Magu Mwanza Salvatory na afisa ardhi jiji la Mwanza Halima Yahaya.

Watumishi hao wa idara ya ardhi wanatuhumiwa kushirikiana na Salehe na kuuza eneo hilo kwa zaidi ya Milioni 100.

"Mheshimiwa Rais John Magufuli naomba uingilie kati suala hili, sisi wananchi wa kawaida tunaonewa na kudhurumiwa maeneo yetu.

"Miaka 40 tunadai haki yetu lakini mpaka leo hatujaipata licha ya mahakama kutupatia haki yetu lakini Jiji tukienda ili tumililishwe imekuwa ni changamoto kubwa kwetu," Seif amenukuliwa akisema.

Seif amenukuliwa akiendelea kueleza kwamba, barua zote kutoka kwa wakuu wa mikoa na mawaziri wa ardhi waliyopita kwenda kwa Jiji la Mwanza lakini wamekuwa wakichelewesha kuwamilikisha eneo lao.

Seif amesema, ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza imekuwa ikitoa maelekezo kupitia Makatibu tawala wa mkoa wa Mwanza.

Pia aliyewahi kuwa waziri wa ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi mjini, Edward Lowassa amewahi kuiandikia barua ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza kuielekeza kuchukua hatua kwa kuwapa haki yao familia ya Hassan Seif.

Barua ya Lowassa iliandikwa Aprili 25 mwaka 1995 kwenda kwa mbunge wa wakati huo Dk. William Shija na kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza wa enzi hizo kwa ajili ya kumaliza tatizo hilo.

Familia ya marehemu hassan Seif, ilimteua bi. Amina Mchaki kama msamizi wa mali ya familia (mirathi) ambao tangu miaka hiyo ya 84 hawajapata haki yao.

Hata hivyo, baada ya Amina ambaye alikuwa msimamizi, alipofariki dunia familia ilimteua Abbakar Seif kuwa msimazi wa mali za familia yao ambaye alianza harakati za kufuatilia viwanja hivyo.
 

Attachments

  • IMG20200826163257.jpg
    IMG20200826163257.jpg
    81.2 KB · Views: 1
  • IMG20200826165202.jpg
    IMG20200826165202.jpg
    100.5 KB · Views: 1
  • IMG20200826152700.jpg
    IMG20200826152700.jpg
    213.7 KB · Views: 1
  • IMG20200826152647.jpg
    IMG20200826152647.jpg
    269.2 KB · Views: 1
Back
Top Bottom