Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,813
- 4,545
Watumishi tisa wa Kitengo cha upimaji wa COVID - 19 kwa wasafiri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere (JNIA) wamesimamishwa kazi kwa kosa la kutokufika kazini kutoa huduma ya vipimo hivyo kwa wasafiri bila taarifa.
"Imeonekana hapa hili zoezi la baadhi ya watumishi kutokuja kazini limekuwepo, sasa hii imenisikitisha sana kwa baadhi ya viongozi kushindwa kuchukua hatua zinazostahili na kulindana kwa kuficha uozo"
Ni kauli ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi baada ya kuwasimamisha kazi Watumishi tisa wa afya katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa juzi alipofika katika uwanja huo akiwa ameambatana na Katibu mwenzake wa Wizara ya Uchukuzi.
Sambamba na hilo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi amewataka Watumishi wanaotoa huduma za Afya hususan katika maeneo ya mipaka ya nchi kavu, maji na ardhi kufanya kazi yao kwa uzalendo na kwa budii ili kuitunza taswira nzuri ya nchi.
Prof. Makubi amesisitiza hilo alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa juzi alipofika katika uwanja huo akiwa ameambatana na Katibu mwenzake wa Wizara ya Uchukuzi.