Watumishi 27 wafukuzwa kazi halmashauri ya wilaya ya Uyui

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
madiwani(4).jpg

Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Uyui mkoani Tabora kwa pamoja limeridhia kuwafukuza kazi watumishi 27 ambao walibainishwa kuwa walighushi vyeti ili wajipatie kazi pamoja na kuwasimamisha wengine 31 ambao walikuwa wameajiriwa mwaka 2004 wakiwa va vyeti vya darasa la saba.

Akisoma maamuzi hayo yamefikiwa katika baraza la madiwani, mwenyekiti wa halmashauri hiyo ya Uyui Bw.Saidi Shabani Ntahondi amesema kuwa, lengo la kutekeleza agizo la serikali la kuwaondoa watumishi wasiostahili huku wanaostahili wakiwa hawana kazi.

Aidha kufuatia maamuzi hayo ambayo yameacha pengo kubwa la watumishi 111, baraza hilo limeiomba serikali kuharakisha kuajili kwani, kata na vijiji havina watumishi ambapo linaweza kuwa pigo kwa halmashauri kuporomoka kiuchumi.

Aidha baraza hilo lililokuwa na jukumu la kumchagua makamu mwenyekiiti wa halmashauri pamoja pamoja na wenyeviti wa kamati za kudumu wamemchagua Abdalah Katarambula kuwa makamu mwenyekiti kwa awamu ya pili.

Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom