Watumishi 23 MOI wachunguzwa madai ya wizi wa Dawa na Vifaa Tiba

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Watumishi 23 wa Idara ya Famasia katika Taasisi ya Mifupa (Moi) wanachunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa madai ya wizi wa dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya Tsh1.2 bilioni.

Hayo yameelezwa leo Jumatano Januari 13, 2021 na mkurugenzi mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Mbungo amesema watumishi hao wanadaiwa kufanya udanganyifu huo kati ya mwaka 2018 hadi 2020.

Akielezea namna ubadhirifu huo ulivyofanyika, Mbungo amesema, watuhumiwa hao walikuwa wanaandika taarifa za uongo katika mfumo unaofahamika kama MEDPRO4 kwa kuweka idadi kubwa ya vifaa vilivyotolewa tofauti na idadi halisi iliyotolewa na madaktari kwa wagonjwa na wateja.

1610541377556.png
 
Matokeo ya kutatua tatizo kwa njia ya mkato huku ukitengeneza tatizo jingine kubwa
Watumishi mishahara yenu haitoshi ndio maana mnaiba kila kinachokatiza mbele yenu. Paza sauti zenu, TALGWU, TUGHE nk vinaongzwa na makada wa chama ambao wanajikomba ili wapewe teuzi za ubunge, nk

Ujumbe kwa serikali sikivu ya CCM: pitisha sheria ya kila mtumishi anayetaka kuacha kazi kwa hiari atapewa mafao yake yote bila kujali ana umri wa kustaafu au la, watumishi wengi wamechoka na kazi ila hawana jinsi wameamua kuonyesha "nidhamu" ili siku zao za utumishi ziishe!
 
.
Screenshot_20210113-163829.jpg


Dar es Salaam. Watumishi 23 wa Idara ya Famasia katika Taasisi ya Mifupa (Moi) wanachunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa madai ya wizi wa dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya Sh1.2 bilioni.

Hayo yameelezwa leo Jumatano Januari 13, 2021 na mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Mbungo amesema watumishi hao wanadaiwa kufanya udanganyifu huo kati ya mwaka 2018 hadi 2020.

Akielezea namna ubadhirifu huo ulivyofanyika, Mbungo amesema, watuhumiwa hao walikuwa wanaandika taarifa za uongo katika mfumo unaofahamika kama MEDPRO4 kwa kuweka idadi kubwa ya vifaa vilivyotolewa tofauti na idadi halisi iliyotolewa na madaktari kwa wagonjwa na wateja.
 
You can not treat diarrhea by sealing the anus.
(A Nigerian saying)
(Kiswahili chake kina ugwadu hakiwezi kuandikwa hapa)
 
Watumishi mishahara midogo sana isipokua waalimu ambao nasikia ndio wanalipwa mishahara mikubwa hapa Afrika mashariki na kati hakuna mfano wake.

Watumishi wote ingependeza kama wangelipwa kama waalimu.
 
Back
Top Bottom