Watumish wa umma tuige mawaziri kupanda kwenye majukwaa ya siasa na kuhutubia

TEMILUGODA

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
1,381
1,500
Hakuna aliye juu ya sheria,ili muafaka ufikie ni muda mwafaka sasa watumishi wa umma kuiga tabia ya mawaziri ya kupanda majukwani na kuhutubia mikutano ya vyama vya siasa mpaka katibu mkuu kiongozi na katibu wa management na utumishi wa umma watakapo ona umuhimu wa ku-balance situation.
 
TUKUTUKU

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
11,775
2,000
Mkuu watumishi wa umma ni wataalamu mbalimbali ambao lengo lao kuu ni kutekeleza sera za serikali.Kinachofanywa na mawaziri ni sahihi kwa kuwa wao ni wanasiasa.Sasa unataka watumishi wa umma wawe wanasisa?
 
TEMILUGODA

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
1,381
1,500
Mkuu watumishi wa umma ni wataalamu mbalimbali ambao lengo lao kuu ni kutekeleza sera za serikali.Kinachofanywa na mawaziri ni sahihi kwa kuwa wao ni wanasiasa.Sasa unataka watumishi wa umma wawe wanasisa?

Wewe nawe ni mvivu wa kufikiri,katiba ya JMT inatambua mawaziri kama watumishi wa umma,sasa kuwaiga hawa tatizo lipo wapi?kwa taarifa yako lengo langu nataka mwafaka katika jambo hili ili tutimize malengo ya 2025 ya kuwa nchi iliyofikia viwango vya utawala bora[Good governance].ACHENI KUKURUPUKIA MAMBO YA GREAT THINKERS].
 
Nsiande

JF-Expert Member
Jul 27, 2009
1,649
1,195
Iongezwe kwenye JD , mpaka sasa watumishi wa umma wanasemewa na msemaji wa wizara, taasisi au shirika
 
TUKUTUKU

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
11,775
2,000
Wewe nawe ni mvivu wa kufikiri, [ACHENI KUKURUPUKIA MAMBO YA GREAT THINKERS].
Mkuu kwani wewe unakaa wapi?naona si mstaarabu hata kidogo,hapa tumezoea kujadiliana na kuelimishana bila kutumia lugha za kijinga jinga, hata kabla ya wewe kujiunga na JF tarehe 11th February 2012 ustaarabu kilikuwa kitu cha muhimu sana,mbona unataka kutualibia JF ulioikuta shwari?.Ni vema kama una hoja ya msingi kuiwakilisha jamvini kwa kutumia lugha za kistaarabu!!
 
Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,863
2,000
Wataambiwa hawapaswi kushiriki siasa hadi waachie ngazi wakati makatibu wakuu bado ni watumishi wa serikali na wanafanya siasa tena chafu. Tanzania ingeitwa Tangeugeu ingependeza.
 
nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
15,113
2,000
siungi mkono hoja..mawaziri wapo kwenye zile nafasi kutoka katika vyama vyao(magamba),hakuna mtendaji(mtaalamu)serikalini aliyeajiriwa kwa kupeleka kadi ya mafisadi(ccm)kwa muakiri,alipeleka vyeti vya shule
 
zema21

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
619
225
Mkuu kwani wewe unakaa wapi?naona si mstaarabu hata kidogo,hapa tumezoea kujadiliana na kuelimishana bila kutumia lugha za kijinga jinga, hata kabla ya wewe kujiunga na JF tarehe 11th February 2012 ustaarabu kilikuwa kitu cha muhimu sana,mbona unataka kutualibia JF ulioikuta shwari?.Ni vema kama una hoja ya msingi kuiwakilisha jamvini kwa kutumia lugha za kistaarabu!!
Unajua unapokuwa waziri unaingia kuwatumikia wananchi wote wa JMT, wenye vyama na wasio na vyama, wa chama Tawala na wasio wa chama tawala! Ni kitu cha ajabu mno kusikia eti mawaziri wako katika ziara za chama cha mapinduzi wakijibu hoja katika mkutano ili hali wale ni watumishi wa umma
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom