Watumiaji WhatsApp: Hii inawezekana inakuhusu


S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Messages
33,734
Points
2,000
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2012
33,734 2,000
MTANDAO wa kijamii wa WhatsApp ambao mpaka sasa una watumiaji bilioni moja duniani kote, mapema mwezi huu umetangaza habari ambazo huenda zisiwe njema kwa baadhi ya watumiaji wa huduma hiyo ambao vifaa vyao vitakuwa nje ya mfumo wa kisasa unaohitajika.

WhatsApp ambao umejizolea umaarufu mkubwa duniani nakuchukuliwa kama njia ya haraka zaidi ya kupashana taarifa kwa ujumbe wa picha, sauti na hata video mbalimbali umetangaza kufikia uamuzi huo ambao unaweza usifurahiwe na wengi kwa kile ulichoeleza kuwa ni kuboresha zaidi huduma zake.

Mtandao huo umesema kuwa umefikia uamuzi huo wa kusitisha kutoa huduma kwa baadhi ya simu zinazotumia mifumo endeshi (OS) ambayo imepitwa na wakati ili kuweza kuendana na kasi ya ukuaji wa soko la simu duniani na teknolojia kwa ujumla.

Hivyo kwa taarifa hiyo ina maana kuwa kuna baadhi ya watumiaji wa mtandao huo ambao mwisho wao wa kutumia huduma hiyo itakuwa ni mwaka huu.

Mabadiliko haya hayajawakumba watumiaji wa simu za Android pekee bali hata wale wanaotumia simu za iPhone ambazo zinatumia mfumo wa uendeshaji wa iOs.

Watumiaji ambao watakosa huduma hii ya WhatsApp ni pamoja na wale wanaotumia simu zinazotumia mfumo huu wa uendeshaji.

Kwa upande wa watumiaji simu za Android watakaoathirika ni wale wanaotumia Version zaAndroid 2.1 na Android 2.2.

Upande wa watumiaji wa simu za Window ni zile zenye mfumo wa Window Phone 7 huku upande wa watumiaji wa simu za iPhone watakaoathiriwa ni wale wenye simu zenye mfumo wa 3GS/iOS6.

Mtandao wa WhatsApp ambao ulianza kupatikana rasmi mwaka 2009 haujaishia hapo, pia umetoa taadhari kwa watumiaji wa simu za Blackberry OS 10 running on BBOS na Nokia S40 running on Symbian S40 ambapo mwisho wa simu hizo kutumia huduma hiyo itakuwa ni Juni 2017.

Kama unakumbuka wakati mtandao huu unaanza kutumika ulianzia kwenye aina mbili za simu za Blackberry na Nokia lakini hicho hakijawa kigezo cha watumiaji wa simu hizo kuendelea kutesa.

“Tunajua kuwa uamuzi huu ni mgumu sana kuuchukua japo tunaamini una tija kubwa kwani utawezesha kuwapatia watu njia bora zaidi ya kuwasiliana na ndugu, jamaa, marafiki,” wamesema WhatsApp.

Chanzo:Mtanzania

Mjumbe hauwawi.
 
adna yuzo

adna yuzo

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Messages
1,040
Points
2,000
adna yuzo

adna yuzo

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2014
1,040 2,000
ahsante mkuu waototo wa ndalichako ndo watalia zaidi kwani huwa wanatumia kudiscuss,wattoto wa kikwete wanatumia kuchat na kutumiana sex video ilimradi wapoteze muda mtu saa 5 asubuh mpk usiku kuchat,waototo wa magufuli majungu tu


KAZI TUNAYo.
 
issac77

issac77

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2013
Messages
2,125
Points
2,000
issac77

issac77

JF-Expert Member
Joined Apr 26, 2013
2,125 2,000
kwahiyo wewe umelijua leo?
 
Snipes

Snipes

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2013
Messages
8,081
Points
2,000
Age
25
Snipes

Snipes

JF-Expert Member
Joined Jul 2, 2013
8,081 2,000
watumiaji watapungua kiasi
 
M

Mwanapropaganda

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2014
Messages
4,266
Points
2,000
M

Mwanapropaganda

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2014
4,266 2,000
Osama Gharib yupo.
 
Lancanshire

Lancanshire

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2014
Messages
14,037
Points
2,000
Lancanshire

Lancanshire

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2014
14,037 2,000
Kwanza sioni faida ya watsap wafunge tu haina shida.
 

Forum statistics

Threads 1,283,910
Members 493,869
Posts 30,805,795
Top