Watumiaji wa Windows XP ambayo ni "Genuine" bado wanaweza kuendelea kuitumia wakizingatia yafuatayo.

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,398
Maicrosoft waliacha kutoa msaada wa viraka vya usalama au "security patches" mwaka 2014, na kusema kwamba hawatoendelea na uratatibu huo.kwa Windows XP.

Microsoft wakaendelea kusema kwamba bado watumiaji wa Windows XP wangeweza kuendelea kupakua sasishi au "updates" na kuziingiza katika kompyuta zao lakini ikiwa watagundua kasoro au udukuzi wenye lengo la kuharibu au "security flaws" wao wasingeweza kutoa kiraka chochote ili kuzuia hali hiyo.

Hii ilikuwa ikimaanisha wazi kwamba endapo kutatokea kasoro ya kiusalama na ikamsaidia mdukuzi yoyote yule na akatuma virusi kushambulia mfumo huo wa Windows XP basi wenye kompyuta hizo watashambuliwa kwa kompyuta zao kuambukizwa kwa kasi ya ajabu.

Hali hii inatisha kwa mmiliki yoyote wa kompyuta na hiyo si tu kwamba ni Windows XP pekee ambayo ina uwezo wa kushambuliwa, wadukuzi wana uwezo wa kushambulia mifumo zingine katika kompyuta yako.

Programu hizo ni kama zile za Adobe Reader na Java ni mfano tu wa programs ambazo licha ya Windows kutoa sasishi kila mara watengenezaji wa programu hizo wanaweza wakawa nao hawatenenezi sasishi kwa muda ulio muafaka hivyo kutoa mwanya kwa wadukuzi na matapeli kuingilia programu hizo na kueneza program hasidi au Malware kama hii ya Ranson ware na WannaCry.

Lakini Windows XP ni moja tu ya chemsha bongo nyingi ambazo wenye kumiliki kopyuta wanakutana nazo katika suala la ulinzi na usalama wa kompyuta yako.

Ntaeleza kidogo namna ya kuweza kuendelea kutumia Windows Xp na zingine kama vile Windows Vista, Windows 7 na 8 bila kuanza kutahayari na kuanza kupiga hesabu ya kutaka kununua kompyuta mpya.

Hii ni muhimu, unapoingiza upya Windows XP chukulia kama unafanya "Reformatting" yaani unairudisha kompyuta yako katika upya ilokuwa nayo huko nyuma na kwa kuzingatia kwamba unayo CD original na halali kutoka dukani, basi unahakikisha unaingiza kila kitu kwa kuicha CD yako izunguke.

Pia ni lazima utakuwa umepata sasishi za "Windows XP with service pack 1, " Windows XP with service park 2" na "Windows XP with service pack 3" hizi zote zilikuwa zikitolewa na Microsoft katika muda wote wa uhai wa Windows XP hivyo ni lazima uwe na CD ambayo pia imebeba mafaili ya "service pack 3" amabyo ilikuwa ni package ya mwisho kabla ya kusitisha kutoa sasihi zao mwezi April mwaka 2014.

Hivyo mmiliki yoyote mwenye kompyuta nyumbani au ofisini mbae anayo original pack ya CD ambayo ina mzigo mzima au "bundle", yaani inatakiwa iwe imeandikwa "Windows XP with service pack 3" basi unaingiza CD yako katika kompyuta yako na unakaa chini ya kahawa au chai na unafuata maelekezo ya ungizaji wa programu zote zilizomo katika CD yako.

Microsoft bado wanaendelea kutoa msaada kwa wale watumiaji wa Windows Embedded POPS Ready na hii ni kwasababu program hii inatumiwa na makampuni, wafanyabiashara na khasa mashine za kotolea fedha au ATM, mashine za kufanyia manunuzi au "cash tills", hivyo kwa kuwa wanasaidia hiyo basi kwa wale wenye home edition unaweza kabisa kufanya updates kupitia katika registry yako katika kompyuta yaani "run registry back to enable Windows Updates".

Kufanya hivi, unagonga start halafu unaingia katika option ya run na unaandika regedit kisha unatafuta mahali panaposema "enable Windows Updates".

Mwisho ingiza Anti Virus katika Kompyuta yako kama anavyoshauri Mwalimu Mndeme kwamba Microsoft wanatoa Anti-Virus ya bure iitwayo Microsoft Security Essential ambayo inakuja kama mzigo wa bure kabisa bila malipo.

Hii Security Essential iliacha kutoa sasishi kwa Windows XP mwezi Julai mwaka 2015 hivyo kwa sasa imebakia kusaidia Windows zingine za 7, 8 na 10.

Zipo Anti-Virus za bure lakini ni Anti-Virus moja tu ambayo inaitwa Avast ya mwaka 2014 ambayo ndiyo angalau inaweza kusidia kwani haisumbuia sana kwenye kutaka ununue ikiwa bidhaa kamili.

Anti -Virus kamili ambayo unaweza kununua dukani ni ile ya Kaspersky ambayo ndiyo inatawala soko kwa sasa.

Kaspersky ina uwezo wa kutambua udhaifu wowote ule uwapo mtandaoni na kuzuia jitihada zozote ile zinazofanywa na wadukuzi popote pale walipo duniani.

Tafuta sasishi kwa programu zingine katika kompyuta yako kama nilivyosema hapo juu programu kama za Java na Adobe unaweza kuzitafutia sasishi pale unapokuwa unatumia mtandao.

Pia unaweza kuweka programu shirika za kutafuta sasishi kama moja ambayo yaitwa Update notifier au secunia PSI ambazo zinakutafutia sasishi bila shida na kuweka kila programu sawa.



Notifier inapatikana kwa kuipakua hapa: Update Notifier - All your software updates in one place! ... Easy, Fast & FREE na Secunia PSI unaweza kuipakua hapa :

Personal Software Inspector

Tafuta sasishi za Device Drivers kwa kompyuta yako:

Komyputa yako inaweza ikawa na kadi mbalimbali au graphics kama Nvidia au AMD ambayo ndiyo mama wa kompyuta yako na zingine ambazo zinasaidia mambo kama muziki, na muonekano wa picha. Una njia mbili kwanza unaweza kwenda katika option ya "Device Manager" na unatafuta sasishi kwa kila driver ya chombo husika.

Njia ingine ni kwenda moja kwa moja kwa watengezaji wa vifaa hivyo katika tovuti zao na kusajili kompyuta yako hivyo kuwa unapata sasishi kila mara zinapotolewa. unachofanya ni kuingiza taarifa za kompyuta yako ikiwemo namba ya pekee yaani Unique Number ambayo itaitambua server ya mtengenezaji.

Badilisha kivinjari au Browser

Ni vizuri pia wakati mwingine mtumiaji wa kompyuta akawa anabadilisha kivinjari ambapo kivinjari kilicho salama zaid ni kile cha Explorer 09 ambacho ndiyo salama zaidi. Pia Gogle Chrome na Firefox zimekuwa zinapata sasishi kila mara hivyo kuwa na uwezo wa kuisaidia Windows XP.

Isimamishe Java kutumia kivinjari.

Programu ya Java katika miaka ya hivi karibuni imekuwa ikileta matatizo yanayotokana na usalama wake. Unachoweza kufanya ni kusimamisha Java -"disable" hivyo kutokuwa ikifanya kazi nyuma ya pazia ukiwa mtandanoni lakini ukawaweza ktumia programs zinazotumia Java bila wasiwasi wowote.

Kufanya hivi nenda katika control panel na uchague Java kisha chagua Security na uondoe alama ya tiki kwenye chaguo lisemalo 'Enable Java content in the browser' kisha funga kwa kugonga neon OK chini mwisho.

Angalia picha ifuatayo.




Hivyo basi bado watumiaji wa "Original Windows XP" wanaweza kuendelea kutumia hii program kwa kuzingatia kuwa sasishi za programu shiriki zote zinakuwa zinafanyiwa Updates mpaka pale untakaoona Microsoft na watengenezaji wa vifaa vingine vilivyomo katika Komyuta yako wanaacha kutoa sasishi.
 
Back
Top Bottom