Watumiaji wa Mtandao wa Simu ya Kampuni ya Voda kuweni makini

Enzi na Enzi

JF-Expert Member
May 29, 2020
888
821
WanaJF mnaotumia mtandao wa simu wa kampuni ya Vodacom kuweni makini kufuatilia makato ya fedha kwenye vifurushi mnavyojiunga.

Kuna kukatwa pesa bila mteja kujua hasa unapokuwa unajiunga ukiwa na fedha kwenye account yako.

Jioni hii nimepigwa, nanilipowafatilia wananipa majibu ambayo wao wenyewe wanashindwa kuyathibitisha na baadae kupotea kabisa bila kunijibu chochote.

Mwisho, nawaomba uongozi wa Vodacom fatilieni hili, kama siyo kampuni inafanya hivyo basi kunawafanyakazi wanafanya mchezo huu mbaya ambao kiukweli umeniuzi sana.
 
Nishawahama kitambo tangia niwe naweka vocha alafu najiunga vifurushi naambiwa sina salio la kutosha kila mara. Na nikicheki salio nakuta washaramba kitambo

Zamani walikuwa wananipiga vifurushi, ukinunua GB1 unapewa G1, sasa jitahidi wakati unanunua uwe umezima data, then kaa dk hata5 bila kuwasha halafu washa uangalie salio la data utakuta wamekula mb baadhi ndo utajiuliza umezitumia wapi??
Ukiwauliza watakwambia umezitumia.

Sasa hivi wameanza kupiga pesa kabisa.
 
Asante mkuu ila makampuny ya simu siyo Tanesco kwamba LAZIMA awe yeye. Voda akizingua laini yao tupa huko chukua halotel, tigo, Airtel nk


Nimeshawaambia tayari, wasipoludisha hela yangu, kesho nasajiri line ya mtandao mwingine.

Nauzuli leo wamenipa hela ya mkopo, ndio itakuwa droo ngoma , halafu tutaona nani aliyepigwa sana.
 
Ndo mchezo wao Hawa jamaa Baada ya kuona huo upuuzi na kutokana na eneo nililopo kutosapoti mitandao mingine basi nimeamua pesa yangu ya vocha iwe kule upande wa mpesa Kwahyo nimepunguza kdogo huo ujinga wao
 
Duh! Kumbe!...

Juzi nimetoka kuamulia ugomvi mzee na wajukuu zake. Mzee kawapa vocha wajukuu waingize ikakatwa (ilikuwa vocha ya 1000 ikabaki 245) wajukuu wanasema Babu alikuwa ana mkopo, Babu anasema hana mkopo labda hawajaweka. Ikabidi niingilie kati tukapiga Customer care, kama ulivyosema kakapokea kadada kanasema system haiko sawa ko hakawezi ingia kwenye account ya ile laini ili kujua nini shida so tupige tena badae, kupiga badae simu hazipokelewi. Ko mpaka sasa Babu anajua madogo walimpita ile vocha
 
Huu ni mwaka wa 9 natumia Vodacom lakini sijawahi kupata hayo matatizo ambayo wengi wanayasema
 
Huu ni mwaka wa 9 natumia Vodacom lakini sijawahi kupata hayo matatizo ambayo wengi wanayasema

Miaka 9, we bado sana dada, watu tumo kwenye huu mtandao zaidi ya miaka 30 ila wewe yawezekana ukiweka vocha ya jero unapewa dh 25 za wiki, harafu unakuwa mzee wa kubip wenzako na kuwa miss call.
Sasa haya matatizo huwezi yajua hata ukiwa voda miaka40.

Kunawatu tunanunua vifurushi vya 30000/= vya mwezi kwa ajiri ya internet bado vifurushi vya kuongea hivyo wewe bado mchanga kwenye matumizi ya sim, nasimu labda yakuhongwa dada. Vocha mpk uwekewe utajuaje.
 
Walinifanyia huo ujinga nimeweka vocher ya buku ten nimezima kila kitu ili nijiumge, nikajaribu kujiunga nikakuta sauli zero, kuwapigia simu wanaongea blah blah, tangu siku hyo nikaacha kutumia voda. In short voda ni majizi wakubwa kwa raia
 
Back
Top Bottom