Watuhumiwa wa mauaji ya Mwenyekiti wa CDM USA River watajwa

Kama ni kweli ni wao, na kama ni kweli walitumwa basi watapotea kabla hawajawataja waliowatuma! Kazi ipo,tusali sana ili ukweli ubainike.

Ooh Mungu ibariki Tz.
 
Hawa ni watuhumiwa. Uliyeanzisha thread hii umeandika as if hawa watu wameshathibitishwa kuwa ni wauwaji. Hiyo siyo sahihi na inafanya jukwaa letu lionekana kama kijiwe cha wahuni.
Vilevile polisi wameshikilia watu saba (7) mbona majini yaliyotajwa ni matatu tu?
 
baada ya kikwete kuambiwa hata kanyaga Meru wameanza kuwakamata bado walio wakatakata mapanga wabunge wetu na waliomuua wakala wetu kule Igunga...Wenje mpinge marufuku Kikwete kukanyaga Mwanza uone polisi watakavyo haha kuwatafuta waliowakatakata wabunge wetu...
 
Nalipongeza jeshi la polisi kwa kukamata watuhumiwa, wakuu suala la uhalifu si la kufumbumbiwa macho na kufanywa la kisiasa. mauaji ya aina yoyote yasifanyiwe mzaha na kuingiziwa siasa bali sheria ichukue mkondo wake masuala ya itikadi za kisiasa za watuhumiwa hayana maana yoyote maana siamini kama kuna chama chochote chenye sera ya kuua raia wema kwa kisingizio chochote kile.
 
Hawa ni watuhumiwa. Uliyeanzisha thread hii umeandika as if hawa watu wameshathibitishwa kuwa ni wauwaji. Hiyo siyo sahihi na inafanya jukwaa letu lionekana kama kijiwe cha wahuni.
Vilevile polisi wameshikilia watu saba (7) mbona majini yaliyotajwa ni matatu tu?

walikamatwa 12 na wengine waliachiwa huru na hao wanne ni watuhumiwa wa mauaji mengine ya uvamizi wa mashaba..
 
Polisi mkoani Arusha imewatia mbaroni wauaji watatu waliomuua kwa kumchinja mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Usa River wilayani Arumeru, Msafiri Mbwambo na tayari wamefikishwa mahakamani.

Kamishna wa polisi nchini, Isaya Mngulu amewataja:

1. DAUD LEZILE MKUBA
2. MATHIAS NATHAN KURWA
3. SAID PHLORIN MKWELA


Hawa ni wale janjawed waliokodiwa na Chama kimoja ...kwenda kuleta vurugu Arumeru....toka maeneo mengine ya nchi...
 
kama ni kweli sheria isimame ili wanyongwe kabisa maana ni aibu na uhaini wa maisha nafamilia kwa ujumla
 
Polisi mkoani Arusha imewatia mbaroni wauaji watatu waliomuua kwa kumchinja mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Usa River wilayani Arumeru, Msafiri Mbwambo na tayari wamefikishwa mahakamani.

Kamishna wa polisi nchini, Isaya Mngulu amewataja:

1. DAUD LEZILE MKUBA
2. MATHIAS NATHAN KURWA
3. SAID PHLORIN MKWELA

Hawajabanwa korodani wataje aliye watuma?
 
Najua wote tuna hasira sana na watu kama hawa ila naomba tuvute subira kwa sasa badio ni watuhumiwa till proven guilt ndio tutasema ni wauji. Na ninaomba mungu wawe ndio hao kweli kwani wanataka kuharibu maana halisi ya demokrasia na vyma vingi na kama ni wao waseme bila kuficha nani kawatuma.
 
Jeshi la polisi lipo mathubuti ni haki yao kuonja mauti kama watapatikana na hatia....big up police
 
Pia mwandishi alipaswa kusema watuhumiwa wa mauaji ya mwentekiti wa cdm usariver majina yao haya hapa, lakini ukisema watuhumiwa hawa hapa means tayari there is no reasonable doubt kuwa ndio hao na umeshawahukumu! Pamoja na ubovu wake tuheshimu mahakama zetu pia watuhumiwa wote ni innocent hadi mahakama iweze ku prove otherwise!

Mkuu,
You are wrong.Unajua maana ya Mtuhumiwa? Neno mtuhumiwa pekeyake linasimama kama not proven guilty.Mtu aliyekuwa proven guilty haitwi mtuhumiwa tena
 
Ni hatua nzuri, Marehemu alikufa kifo cha kinyama, maana kile hakikua kisu nadhani lilikua panga, mpk kukata ile shingo mpk kufa,haikua kazi ndogo na Kamanda alikufa kifo cha mateso,nawaombea Polisi wafanye kazi yao vizuri, na mtoa hukumu huyo,namuombea awe na uchungu kama nilioupata mimi ili atoe hukumu sawia na kosa lenyewe, though it will take time mpaka conviction.
 
Back
Top Bottom