Watuhumiwa wa mauaji ya Mwanza, Tanga wauawa Dar

Wewe ukimuona nyoka chumbani kwako akataka kukugonga utamuua au utamrudisha porini??
hahahah, labda awe ng'ombe ndiyo utamrudisha zizini, otherwise itabidi umuue fasta. Ingawa kuna nchi zinasheria ambapo ni kosa kumuua mnyama awe mbwa, mbuzi, etc mpaka kwa utaratibu maalumu, hivyo hata ukimkuta nyoka chumbani unamrudisha porini, ila kwa bongo huo ustaraabu hatujafikia.
 
HIVI MTUHUMIWA HUWA ANAUAWA AU ANAFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA KUJIBU TUHUMA?

Rudia kusoma ili uelewe mkuu.
Ikiwa mtuhumiwa amekaidi amri ya kujisalimisha na kuamua kupambana na askari kwa siraha hatima yake ni nini?
 
Kama jambazi ameuwa watu Tanga na Mwanza then ukamkuta Darslum na katika harakati za kumkamata akataka kukimbia utamfanyeje kama ingekuwa ni wewe.
Ni majambazi au wanatuhumiwa? Halafu una uhakika kulitokea mapambano? Wakati mwingine polisi wanahalalisha walichofanya kwa maelezo kuwa kulikuwa na mpambano kumbe hamna kitu kama hicho,kumbuka ile issue ya Zombe
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema kuwa limefanikiwa kuwaua watuhumiwa wa mauaji yaliyotokea hivi karibuni katika mikoa ya Mwanza na Tanga.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amesema kuwa mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya watu 8 mkoani Tanga aliyefahamika kwa jina la Abuu Seif ameuawa juzi katika mapambano na askari maeneo ya Kimara, huku mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya Mwanza akiuawa maeneo ya Buguruni.

Chanzo: EATV

View attachment 360613
Kuua watuhumiwa siyo jambo la kujivunia
 
Ni majambazi au wanatuhumiwa? Halafu una uhakika kulitokea mapambano? Wakati mwingine polisi wanahalalisha walichofanya kwa maelezo kuwa kulikuwa na mpambano kumbe hamna kitu kama hicho,kumbuka ile issue ya Zombe
Wote hatujui kilichotokea huko na kamanda mwenyewe pia hajasema sababu za hao majambazi kuuawa,inawezekana kuna sababu za msingi ndiyo maana wakaamua kufanya hivyo,tusiwalaumu polisi haraka kwasababu kazi ya police si kuuwa bali kumkamata mhalifu.
 
Ilikuwaje kukawa na mapambano??? Je lengo kuu ilikuwa kuwaua au kuwakamata ili watuambie kwanini wanaua na tupate chain ya wauaji nchini!?
 
Wote hatujui kilichotokea huko na kamanda mwenyewe pia hajasema sababu za hao majambazi kuuawa,inawezekana kuna sababu za msingi ndiyo maana wakaamua kufanya hivyo,tusiwalaumu polisi haraka kwasababu kazi ya police si kuuwa bali kumkamata mhalifu.
Hawa wa kwetu ni kudhuru na ikibidi kuua haraka sana.
 
Ninafikiri walikuwa wanarushiana risasi ndiyo wakawahiwa vinginevyo wangekamata wasaidie kuwataja wasaidizi wao wakiashamaliza ndiyo wanamalizwa.
 
Ninafikiri walikuwa wanarushiana risasi ndiyo wakawahiwa vinginevyo wangekamata wasaidie kuwataja wasaidizi wao wakiashamaliza ndiyo wanamalizwa.
Je, walijua lini kama ndio wauaji wa tanga na mza? baada ya kuwaua au kabla?
 
Back
Top Bottom