Watuhumiwa wa mauaji NMB Temeke wagoma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
202,924
2,000
Watuhumiwa wa mauaji NMB Temeke wagoma
Thursday, 16 December 2010 20:48

Tausi Ally
WASHTAKIWA zaidi ya 10 wanaokabiliwa na kesi ya mauaji katika benki ya NMB tawi la Temeke jijiji Dar es Salaam jana waligoma kushuka ndani ya gari lililowapeleka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Tukio hilo, lilitokea jana saa 3:15 asubuhi katika Mahakama ya Kisutu baada ya washtakiwa hao wanaotoka katika gereza la Keko na Segerea kufikishwa katika mahakama hiyo.

Kesi hiyo, jana katika mahakama hiyo, ilipangiwa tarehe nyingine kwa sababu upelelezi wa kesi hiyo, haujakamilika.
Baada ya gari kufika katika eneo la Mahakama ya Kisutu, washtakiwa hao, walianza kupiga kelele huku wakiimba kuwa ‘hatutoshuka hadi kieleweke’.

Washtakiwa hao, waliendelea kufanya hivyo hadi gari lilipofika katika eneo la kushushia mahabusu kwa ajili ya kuhifadhiwa wakati wakisubiri kuingia mahakamani kusikiliza kesi zao na askari wa jeshi la Magereza aliwaamrisha wateremke,lakini waligoma.
Washtakiwa hao, waligoma kushuka huku wakidai kuwa wamechoshwa na hawaoni maendeleo ya kesi yao kila wanapopelekwa katika mahakama hiyo, wanaelezwa kuwa upelelezi haujakamilika.

“Tunataka watufunge kama wanaona ni kweli tumetenda kosa, kila siku tunaambiwa upelelezi bado haujakamilika,” walilalamika washtakiwa hao.

Hata hivyo mmoja wa washtakiwa hao ambaye jina lake alikuweza kufahamika alikubali kushuka na kusomewa mashtaka yanayomkabili mbele ya Hakimu Mkazi, Liad Chamshama ambaye aliiahirisha kesi hiyo hadi Desemba 30, mwaka huu itakapotajwa tena.
Washtakiwa wengine waliogoma kushuka ndani ya gari walipelekewa tarehe ya kesi yao wakiwa kwenye gari na kurudishwa rumande.

Watuhumiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Boniface Joseph (34), Deogratius Masawe (30) mkazi wa Moshi, 55935 SGT Mathew Mwangunga (43) ambaye ni askari wa Jeshi la Wananchi na mkazi wa Kibaha, Antony Sokya (30).
Wengine ni Said Hamisi (30), Issack Abuu (23) mkazi wa Moshi, Jopo Salum (27), Richard Muhonza ambaye ni raia wa Burundi na Yusuph Rajab (34) .

Kwa pamoja wanadaiwa Julai 31, mwaka huu wakiwa katika Benki ya NMB Tawi la Temeke waliwaua marehemu Seif Mkweke na E 329 CPL Josephat.

Mbali ya mauaji hayo, washtakiwa hao pia wanadaiwa kupora fedha katika benki hiyo.
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
202,924
2,000
Washtakiwa hao, waligoma kushuka huku wakidai kuwa wamechoshwa na hawaoni maendeleo ya kesi yao kila wanapopelekwa katika mahakama hiyo, wanaelezwa kuwa upelelezi haujakamilika.

"Tunataka watufunge kama wanaona ni kweli tumetenda kosa, kila siku tunaambiwa upelelezi bado haujakamilika," walilalamika washtakiwa hao.

Moja ya matunda ya katiba Mpya ya Kenya ni kuwa watuhumiwa wa kesi za mauaji hupewa mdhamana..............na sisi hatuna budi kusema kuwa ni haki ya mshtakiwa kujulishwa makosa anayotuhumiwa katika kipndi kisichozidi masaa 48 tangia amekamatwa na kesi hiyo kuanza kusikilizwa katika kipindi maalumu kisichozidi miezi miwili hivi.......................

Kama ushidi haujakamilika polisi wanapaswa kuwaachia watuhumiwa na wala siyo kuzijaza lupango na watuhumiwa wenye kesi hewa...............

Ikumbukwe hata kwenye katiba iliyopo mtuhumiwa hana hatia hadi hapo mahakama itakapomtia hatiani...............
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom