Watuhumiwa wa kesi za ugaidi Arusha walalamikia upelelezi wa kesi zao kuchelewa

buswelu moja

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
226
180
Baadhi ya watuhumiwa wa kesi za ugaidi wanaoshikiliwa katika gereza la KISONGO mkoani Arusha wanalalamikia upelelezi wa kesi zao kuchelewa hadi sasa.

Watuhumiwa hawa wanasema kwamba ni takribani miaka mitatu sasa inatimia lakini kila wakipelekwa mahakamani wanaambiwa upelelezi wa kesi zao unaendelea.

Wanaiomba serikali kupitia ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali kupitia upya majalada yao ili haki iweze kuonekana imetendeka.

Kesi yao italetwa ifikapo Mei 3 mwaka huu katika mahakama kuu kanda ya Arusha nitawajuza nini kitajiri mahakamani ,asanteni
 
Wanaiomba ....ofisi.. .kupitia upya majalada yao haki ..imetendeka.

Kila mwanadamu angetambua kuwa Haki ni kitu cha msingi maovu yasingekuweko: HAKI YA MWENZAKO KUISHI, KUABUDU, KUVAA ANAVYOPENDA na KULA ANACHOTAKA (Mf. Chura, Nyoka, senene, mbwa nk) ili mradi havunji sheria za nchi.
 
Baadhi ya watuhumiwa wa kesi za ugaidi wanaoshikiliwa katika gereza la KISONGO mkoani Arusha wanalalamikia upelelezi wa kesi zao kuchelewa hadi sasa.

Watuhumiwa hawa wanasema kwamba ni takribani miaka mitatu sasa inatimia lakini kila wakipelekwa mahakamani wanaambiwa upelelezi wa kesi zao unaendelea.

Wanaiomba serikali kupitia ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali kupitia upya majalada yao ili haki iweze kuonekana imetendeka.

Kesi yao italetwa ifikapo Mei 3 mwaka huu katika mahakama kuu kanda ya Arusha nitawajuza nini kitajiri mahakamani ,asanteni
Watulie, ugaidi haupelelezwi kwa haraka hivyo.
 
Back
Top Bottom