chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,968
Marehemu Kinyongoli enzi za uhai wake
Mapya yameendelea kuibuka kuhusiana na kifo cha aliyekuwa askari wa usalama barabarani, Ally Kinyogoli baada ya Jeshi la Polisi kudai watuhumiwa wawili kati ya 15 wamekiri kutekeleza mauaji hayo kutokana na mgogoro wa kifamilia.
Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam, Simon Sirro alilieleza gazeti hili jana kuwa, baada ya mahojiano watuhumiwa hao walikiri kuhusika na kifo hicho na kuwataja wahalifu wengine wawili zaidi walioshirikiana nao.
Watuhumiwa hao wapya wanaendelea kusakwa na polisi ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria na kwamba, uchunguzi wa awali unaonyesha ugomvi wa familia ndicho chanzo kikuu cha kifo cha askari huyo.
Mei 18, wakati wa usiku watu waliokuwa wameziba nyuso walikwenda nyumbani kwa Kinyogoli na kumuita na alipotoka nje walimfyatulia risasi zilizosababisha kifo chake.
Taarifa zilizotolewa hivi karibuni na jeshi hilo zilisema lilikuwa linawashikilia watu hao, akiwamo mke wa marehemu huyo kwa kuwa ndiye aliyemuita Kinyogoli aende nyumbani kwake na mauti kumfika.
“Kifo cha askari Kinyogoli kimesababishwa na ugomvi wa familia na waliofanya mauaji haya walikuwa wanne, wawili tunaendelea kuwatafuta ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema Sirro.
Alisema baada ya kubaini watuhumiwa 13 hawahusiki na mauaji hayo waliachiwa kwa dhamana, huku upelelezi ukiwa unaendelea ili kujua mtandao wote uliohusika.
Wakati Sirro akieleza hayo, Polisi Mkoa wa Pwani imesema kuwa inaendelea kumshikilia mke wa marehemu huyo kwa ajili ya kusaidia zaidi katika upelelezi wa kesi hiyo.
Chanzo: Mwananchi