WATUHUMIWA katika mauaji ya Swetu Fundikira wahukumiwa kifo!

mtwana

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
428
140
WATUHUMIWA katika mauaji ya Swetu Fundikira, MTM 1900 Sajenti Roda Robert (42) wa kikosi cha JKT - Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ-Kunduchi leo wamehukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam. HABARI NA PICHA ZAIDI KUWAJIA HIVI PUNDE!
 

Attachments

  • Untitled.jpg
    Untitled.jpg
    15.7 KB · Views: 1,318
  • Wauaji.jpg
    Wauaji.jpg
    29.5 KB · Views: 1,454
Mkuu tafadhali ongeza maneno katika habari yako ili watu tupate picha halisi ya tukio zima la mauaji
 
Hawa jamaa sasa wanaishi kwa majuto kwa mambo ya kipuuzi kabisa kutafuta sifa tu. Kumuua kijana wa watu kwa mzozo wa barabarani kisa wao wababe....loh!

Haya, japo hawatanyongwa hawa. Wanaenda kukaa na wenzao gizani
 
Hivi hukumu ya Kifo Tanzania ipo? na katika historia ya nchi hii ni wangapi waliohukumiwaga kifo??
 
auwae kwa upanga na yeye atauwawa kwa upanga
Haya yataendelea kutanua huko gerezani kwani aliyehukumiwa kifo hafanyi kazi yoyote gerezani. Adhabu yao ya kifo haitatekelezwa kisa rais hajakubali. Ni vema katiba mpya ikaondoa huu mwingiliano wa rais kuingilia mihimili mingine. Jaji akihukumu kinachofuata iwe utekelezaji wa hukumu, unless an appeal to the higher court is lodged.
 
Hivi bado tu ni watuhumiwa? Si tayari wana hatia? Kwanini msibadirishe title na kuwa Wauaji Wa Swetu wahukumiwa hukumu ya kifo! Samahani lakini.
 
tatizo hawa jamaa huwa wanajiona special sana hasa barabarani sasa ubabe wao umewacost
 
Hivi hukumu ya Kifo Tanzania ipo? na katika historia ya nchi hii ni wangapi waliohukumiwaga kifo??

Hukumu ipo ila hakuna rais anayesign hyo issue wengi hawataki kuna prezdent nadhani nkapa ashawahi sign ila brotherman ajasign hata moja nahisi watakula mvua za maisha tu!
 
WATUHUMIWA katika mauaji ya Swetu Fundikira, MTM 1900 Sajenti Roda Robert (42) wa kikosi cha JKT - Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ-Kunduchi leo wamehukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam. HABARI NA PICHA ZAIDI KUWAJIA HIVI PUNDE!

Katika kesi hii inasemekana kulikuwa na kihoja cha aina yake; Inabidi mfumo wetu wa sheria uangalie upya suala zima la kuwatumia wazee wa baraza kama hawa, ambao hali zao tu zinaonyesha wako katika mazingira rahisi mno ya kuhongwa na kupindisha ukweli.

Na ikiwa hakimu mwishowe hazingatii ushauri wao, kuna haja gani ya kuwa na wazee wa baraza?

Jana katika mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam wazee wa baraza katika kesi ya Swetu Fundikira waliushangaza umma uliohudhuria kesi hiyo (nafikiri hata na ndugu wa washtakiwa hawakutegemea kile walichosikia) baada ya wote watatu kudai kuwa washtakiwa waachiwe huru kwa kuwa hakuna ushahidi kuwa wao walimuua Swetu Fundikira. Aliyetoa kali kabisa ni Mzee Raha Saidi aliyedai polisi wamewabambikia kesi washtakiwa ki ujanja ujanja. Mzee mwingine Ali Kampea alidai kifo cha marehemu ni ajali tu kwani alianguka ndipo akaumia kichwani na kupeleka kifo chake. Bibi Johari yeye alidai kuwa yeye haoni kama washtakiwa walikuwa na nia mbaya na hatimaye kumuua Swetu Fundikira bali washtakiwa ni watu wazuri na nia yao ilikuwa ni kumpeleka polisi tu na si vinginevyo hivyo yeye anaona hawana hatia.
SAM_3574.JPG

 
Hi kuna aliye na wasifu wa Swetu Fundikira? Niliwahi cheza mpira na Swetu Fundikira huko Tabora miaka ya 80, akiwa anasoma Kazima kama sikosei, na sijui kama huyu ndiye huyo niliyemfahamu. Naona wanafanana.
 
Back
Top Bottom