Watu zaidi ya 200 Nchini Uganda hawajulikani walipo baada ya ghasia za Uchaguzi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Chama cha National Unity Platform (NUP) kimesema kwamba takriban raia 243 wa Uganda hawajulikani walipo wala hakuna taarifa zozote zinazofahamika kuwahusu.

Awali, spika wa Uganda Rebecca Kadaga amesema kuwa serikali imechukua muda mrefu kujibu agizo la bunge la kutaka iweke wazi majina ya watu wasiojulikana walipo.

Bi. Kadaga alisema serikali itawajibishwa kuhusiana na taarifa za watu waliopotea kwasababu imeshindwa kuweka wazi orodha yao mbele ya umma, kulingana na gazeti la Daily Monitor.

“Tangu kikao cha kwanza cha bunge kilichohudhuriwa na kila moja, kumekuwa na malalamiko juu ya madai ya watu wasiojulikana walipo. Rais aliagiza walio na majina ya watu hao kuyachapisha,” Spika huyo alisema.

Kulingana na gazeti la Daily Monitor, spika aliongeza kuwa: “Kwa kuwa orodha hiyo bado haipo, natoa wito kwa walio na orodha hiyo yenye majina ya watu wasiojulikana walipo kuitoa hapa ili serikali iweze kuwajibishwa.”

Uamuzi wake unafuatia ombi la mbunge wa Kalungu Magharibi Joseph Ssewungu aruhusiwe kuweka wazi orodha ya watu wasiojulikana walipo na taarifaza zao.

Idadi kubwa ya walisiojulikana walipo inadaiwa kwamba “walitekwa nyara” na maafisa wa usalama waliokuwa wanashika doria mara mingi kwa kutumia magari aina ya Toyata Hiace, ambayo ni maarufu kwa wenyeji kama magari yasio na rubani yaani drones.

Chama cha NUP nacho kimesema kwamba kilianza kusajili watu waliopotea wengi wao wakiwa wafuasi wao Novemba mwaka jana baada ya familia kuwasilisha malalamishi yao kufuatia maandamano ya siku mbili katika mwezi ambao vikosi vya usalama viliwapiga risasi na kuwaua raia 54.

Wakati huo huo, Rais Museveni amekiri kutokea kwa mauaji yaliyochochewa na kukamatwa kwa aliyekuwa mgombea urais Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, kupitia televisheni kwamba wengi wa waliofariki dunia walikuwa “waporaji” na “magaidi”.

Bongo5
 
Back
Top Bottom