Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,397
Watu zaidi ya 150 kwenye vijiji vya Mpwapwa na Jangwani katika tarafa ya Mpui, wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, hawana mahali pa kuishi kufuatia nyumba zaidi ya hamsini kubomolewa na mvua kubwa iliyokuwa imeambatana na upepo mkali, huku ikimuacha mtoto mmoja wa miaka sita akijeruhiwa kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba.
Baadhi ya waathirika wa Kimbunga hicho pamoja na mashuhuda, wakiongea kwenye kijiji cha Mpwapwa ambako nyumba 25 zimebomolewa, wamesema kuwa mvua hiyo ilianza kunyesha mnamo usiku wa manane, na wakimshukuru mungu kwa uweza wake kwani nyumba moja iliyokuwa na watu zaidi ya wanane ilibomolewa kabisa hadi chini lakini wote walitoka salama kabisa, na hivi sasa wote wamejibanza kwa ndugu, jamaa ikiwa ni pamoja na majirani.
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa zahanati ya kijiji cha Mpwapwa Bi. Upendo Lwinga, amesema alfajiri ya siku ya tukio walimpokea mtoto Edson Konstebo akiwa hana fahamu kabisa baada ya kujeruhiwa kichwani, na baada ya kumhudumia waliamua kumhamishia kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa mjini Sumbawanga, huku diwani wa kata ya Mpwapwa Bw. Abeli Msumbachika akiomba msaada kwa ajili ya waathirika waliopoteza mahali pa kuishi vyombo mbalimbali pamoja na chakula.