Watu zaidi ya 150 hawana mahali pa kuishi kufuatia nyumba zaidi ya hamsini kubomolewa na mvua kubwa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,551
2,000
Watu zaidi ya 150 kwenye vijiji vya Mpwapwa na Jangwani katika tarafa ya Mpui, wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, hawana mahali pa kuishi kufuatia nyumba zaidi ya hamsini kubomolewa na mvua kubwa iliyokuwa imeambatana na upepo mkali, huku ikimuacha mtoto mmoja wa miaka sita akijeruhiwa kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba.

Baadhi ya waathirika wa Kimbunga hicho pamoja na mashuhuda, wakiongea kwenye kijiji cha Mpwapwa ambako nyumba 25 zimebomolewa, wamesema kuwa mvua hiyo ilianza kunyesha mnamo usiku wa manane, na wakimshukuru mungu kwa uweza wake kwani nyumba moja iliyokuwa na watu zaidi ya wanane ilibomolewa kabisa hadi chini lakini wote walitoka salama kabisa, na hivi sasa wote wamejibanza kwa ndugu, jamaa ikiwa ni pamoja na majirani.

Kwa upande wake mganga mfawidhi wa zahanati ya kijiji cha Mpwapwa Bi. Upendo Lwinga, amesema alfajiri ya siku ya tukio walimpokea mtoto Edson Konstebo akiwa hana fahamu kabisa baada ya kujeruhiwa kichwani, na baada ya kumhudumia waliamua kumhamishia kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa mjini Sumbawanga, huku diwani wa kata ya Mpwapwa Bw. Abeli Msumbachika akiomba msaada kwa ajili ya waathirika waliopoteza mahali pa kuishi vyombo mbalimbali pamoja na chakula.
 

Simara

JF-Expert Member
Oct 1, 2014
5,036
2,000
Pole zao wajitahidi wajijengee tu hatutoi michango safari hii, tulilazimishwa hadi maofisini matokeo yake hela hazikufika zinapohitajika.
 

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,823
2,000
Haya wale wazee wa kupiga dili pesa za rambi Rambi na majanga kwa jina la "Saidia Wahanga", dili hilo hapo tena.
 

AGOLA

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,344
2,000
Hata tukichanga Magufuli hatakubali kuwapenimaskini!Atasema mvua haikuetwa na ccm,mwisho wa siku pesa zote mfukoni.Labda mtupenjia njia nyinginembadala.
 

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,304
2,000
Dah. Iyo mvua itakuwa yamiujiza. Haiwezekani kingine kuto ni ukame uko kunamvua ya kubomoa hadi nyumba.

Serikali itoe tena tangazo tuwachangie wahanga wa mafuriko
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,777
2,000
Hatutoi hata shilingi moja, maana kilichotupata kagera hatutaki kirudie tena, hela za kusaidia waathirika zikajenga miundo mbinu ya Serikali
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom