Watu zaidi ya 15 wafariki kwa ugonjwa usiofahamika, Chunya

Status
Not open for further replies.
Tanzania inatakiwa kuwepo na kikosi maalumu kwa ajili ya magonjwa ya milipuko na ikiwezekana wanakua na chopa yao kabisaa ya emergency bila kutegemea usafiri wa magari hapo tutakua tumeweza maana hii ya watu kutoa taarifa mpaka kwenye kikao cha madiwani na ishu ya kuzima Moto Mungu atusaidie kwa kweli...
Dsm ipo mikoani sidhani
 
Dsm ipo mikoani sidhani
Dsm ipo nini Mkuu,sijakuelewa Kama chopa inaweza kuwepo mji wowote na wataamu wanapiga kazi zao ikitokea tatizo lolote wanatoka haraka ili kwenda kukagua matatizo yaliyopo na si kutegemea vikao vya makatibu watendaji tunarudi zama za mawe za kati...
 
Hapo ndipo utajua faida za mabeberu ,hapo mabeberu wakichukua sample tu wanatupa details za huo ugonjwa fasta na transmission methods..Poleni sana wakazi wa chunya.
 
Kwa namna nilivyofatilia mahojiano youtube ni kwamba Vifo havijatokea kwa wakati mmoja (mkupuo) kama wengi ilivyotushtua baada ya kuona vichwa vyaa habari hasa kwa millard ayo.

Mimi nilishtuka nikajua ni kitu kimetokea leo leo na vifo vyote vimetokea leo. Daah! Kwa kweli nili panic sana.

Ila tusubiri majibu kutoka wizarani nadhani kutakuwa na mwongozo thabit

Ila kwa kweli sio jambo la Kubeza wala kulifanyia mzaha ndugu zangu, Tumuombe mungu maana kama ni kweli hii issue ni hatari
 
Naomba kujua kama ugali wa dona unaliwa sana pande hizo, baada ya hapo zichukuliwe sampuli za mahindi yaliyohifadhiwa kwa ajili ya chakula cha familia zipelekwe kupimwa kiwango cha sumu kuvu aina ya aflatoksini pale TBS mbali na vipimo na uchunguzi mwingine utakaofanyika, wabeja sana...
 
TUWE MAKINI SANA NA HAWA MABEBERU.TENA MBAYA ZAIDI TUMEKATAA CHANJO NA BILL GATES ALISEMA KUNA JANGA LITAKUJA BAYA ZAIDI HATUJUI LITAANZIA NCHI GANI.
Umebana pua "tuwe makini na mabeberu..." huku masaa 24 uko bize na smartphone yao, je hawawezi kukuwekea radiation or anything to harm you as you daily claims??
 
Daah huko kuna washkaji zangu kibao sijui kama hata wamechukua tahadhari
 
Nani kakuambia hakipo? Ubaya wa nyakati hizi ni kwamba sirikali yetu haitaki kuwa wazi.

Au umesahau Mwele alifanywaje baada ya kusema Tanzania kuna Zika virus? Sasa huyo Mwele ndiyo alikuwa hiko kitengo.
Sidhani Kama kikosi cha emergency nachozungumzia Mimi hata maabara yao inakua mobile au unazungumzia hiyo ya kutuma sample daslm harafu unasema emergency? hapo vitu vingi mno vinatakiwa ili kulinda afya za Watanzania wenzetu...
 
Mganga mkuu alitoa taarifa ngazi za juu baada ya kupata taarifa kutoka kwa diwani.Kwa nini afukuzwe kazi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom