Golden Age
JF-Expert Member
- Mar 9, 2017
- 203
- 45
DRUGS WON - KRS ONE
Ukisikiliza album ya mkongwe KRS One inayokwenda kwa jina la " now hear this " ambayo aliitoa rasmi mwaka juzi mwishoni basi utakutana na ngoma moja inaitwa " drugs won " ambapo humo ndani Krs One ameichana serikali ya Marekani waziwazi kabisa kwamba imeshindwa kutokomeza na kukomesha biashara ya madawa kulevya, yaani kwamba viongozi wa serikali ya Marekani wameshindwa kutimiza ile ahadi waliyoahidi kwamba watatokomeza na kufutilia mbali kabisa biashara ya madawa ndani ya Amerika.
Kwa hiyo hebu tuangalie legendary Krs One anasemaje humo ndani.Krs One anachana akisema " cops ain't selling while rocking your melon?/ cop cars smelling like Cali blue dream.../.Hapa Krs One anatuweka wazi kwamba maofisa polisi wa Marekani ni watumiaji wakubwa wa bangi, lakini wamekua wakiwakamata na kuwatesa raia wote wa kawaida ambao wanajihusisha na uuzaji pamoja na utumiaji wa bangi.Hili suala la kuhalalisha matumizi ya bangi limekua na mijadala mirefu sana.....katika baadhi ya majimbo ya Marekani matumizi ya bangi yamehalalishwa na kwamba hakuna hukumu ya adhabu kwa yeyote yule anaejihusisha na matumizi ya bangi,. Israel nao wapi katika mchakato wa kuhalalisha matumizi ya bangi.
Tukija hapa Bongo kuhusu suala la askari polisi kutumia mmea kwa kweli sitaki kuliongelea,sitaki kuingia katika mvutano na vyombo vya usalama.Suala la uhalalishwaji wa matumizi ya bangi ni pana mno na tutakuja kulijadili siku nyingine.
Krs One anaendelea kuchana akisema "government are selling it, every day one ton/ they declared a war on drugs but drugs won....." anachana tena akisema " don't you think these politicians ain't selling.... ".Hapa Krs One anaishtumu serikali ya Marekani kwamba inahusika katika kufanya biashara ya madawa na kwamba wanachokifanya ni unafiki tu lakini ukweli ni kwamba wako ndio wauzaji wakuu wa madawa pale Marekani, Hapa Krs One anawaongelea CIA,CIA ndo wauzaji wakubwa wa madawa pale Marekani na ushahidi upo wa kutosha.
Miaka kadhaa iliyopita mkuu wa kitengo cha kuzuia biashara ya madawa ya kulevya alijitoa ufahamu,na akaithibitishia dunia kwamba CIA ndo wauzaji wakuu wa madawaya kulevya ambapo alisikika akisema " a ton of cocaine was smuggled into the united States of America by Venezuelan national guard in cooperation with CIA".
Pia kuna ripoti nyingi sana ambazo zimekua zikithibitisha kwamba serikali ya Marekani imekua ikijihusisha na biashara ya madawa ya kulevya,moja ya ripoti ilikuwa ikisomeka "americans themselves admit that drugs are often transported out of Afghanistan brings them about 50 million dollars a year which covers the expenses tied to keeping their troops there....they don't have any planned military action to eliminate Mujahedeen....".
Tone deff nae katika wimbo wa Peruvian Cocaine alisikika akichina " the CIA conducts the flow for these young hustlers who lust for dough..." Hapa tunaona Tone deff nae ameweka wazi kwamba CIA ni wauzaji wa madawa,Diabolic nae amewahi kuiongolea hii ishu ambapo alisikika akichana " the central intelligence agency takes a weight faithfully/ the finest type of China white and cocaine you will see......"
Pia kuna mwandishi wa habari aliyekua akijulikana kwa jina la Garry Webb,yeye aliandika kitabu ambacho ndani yake alielezea kwa urefu sana jinsi mtandao mzima wa CIA unavyoingiza na kuuza madawa Amerika,na hii ikazua taharuki kubwa pale Marekani.... kwa sababu Garry Webb akawa kama ameivua nguo serikali ya Marekani,Miaka kadhaa baade Garry Webb aliuawa na inaaminika kwamba CIA ndio waliomuua.
Garry Webb kabla ya kifo chake alisisitiza kwamba daima atasimamia ukweli katika kuelezea uchafu wote unaofanywa na serikali ya marekani ambapo alinukuliwa akisema " aunthetic journalism is telling people something that the government does not them want to know... " Pia juzi tu hapa kuna ndege ilipata ajali mpakani mwa Marekani na Mexico na katika harakati za uokoaji ile ndege.....itaendelea
Muendelezo utapatikana katika kitabu cha HipHop na Maisha ambacho kitatoka hivi karibuni na unaweza ukaweka oda yako kupitia namba 0713560346/0743959819