Watu Wote: Filamu ya Kenya yashinda tuzo ya Oscars

Bishop Hiluka

JF-Expert Member
Aug 12, 2011
7,140
14,678
_97824380_0022449.jpg

Filamu kuhusu shambulizi la kigaidi la Alshabaab nchini Kenya ambapo watu 28 waliuawa ndani ya basi eneo la Mandera mwaka 2014 imeshinda tuzo la Oscars kitengo cha wanafunzi.

Filamu hiyo pia itawania tuzo kuu za Oscars kitengo cha filamu fupi mwaka ujao. Ni filamu ya kwanza kutoka Kenya kushinda tuzo hiyo.

Filamu hiyo inayoeleza hadithi ya Kenya, kuhusu Wakenya na inashirikisha waigizaji wa Kenya, inasimulia shambulio hilo la mwaka 2014 kaskazini mwa Kenya, ambapo maudhui ya uadui wa kidini kati ya wakristo na waislamu yanaangaziwa.

Tuzo hiyo itatolewa tarehe 12 Oktoba, katika ukumbi wa Samuel Goldwyn Theater, Beverly Hills, Los Angales Marekani. Ni mara ya kwanza ambapo filamu ya kenya imeteuliwa kuwania tuzo ya Oscars.

"Kenya sasa imepanda ngazi. Tunaongoza katika kueleza ulimwengu hadithi za Afrika" Matrid Nyaga, mwandaaji wa filamu hiyo ameambia BBC.

Katika shambulizi hilo, Waislamu walikataa kujitenga na Wakristo walipoamriwa kufanya hivyo na magaidi wa Alshabaab kutoka Somalia.

"Ni hadithi kuhusu Kenya na undugu wa Wakenya, na inaonyesha njia mwafaka ya kukabiliana na ugaidi kote Ulimwenguni"

Filamu hiyo iliyoundwa kwa ushirikiano wa wanafunzi wa Ujerumani na watengenezaji filamu wa Kenya inalenga kuwakumbuka mashujaa wa shambulizi hilo.

"Nina furaha kubwa! Cha kufurahisha ni kwamba filamu hii imetengenezwa kwa ushirikiano wa Wakenya. Sisi wote tulishirikiana kufanikisha ndoto hii" Tobias Rosen, mwandaaji wa filamu hiyo kutoka Ujerumani ameambia BBC.

Filamu itaonyeshwa Kenya kabla ya mwisho wa mwaka huu. Kwa kipindi cha Zaidi ya miongo miwili, Kenya imekuwa ikishambuliwa na magaidi wa Alshabaab. Mwaka 2015, wanafunzi zaidi ya 147 waliuwawa na Alshabaab katika chuo kikuu cha Garissa kaskazini mwa Kenya.

SOURCE: BBC

HONGERA SANA MAJIRANI. Ninavyowajua, mtaitumia hii opportunity kufanya mambo makubwa sana, wakati sisi tukiendelea kupiga domo...
 
View attachment 589312

Ile filam ya mapanki ilikomea wapi?

Heri nasi watz itutoe kimasomaso
 
Back
Top Bottom