Watu Weusi We Acha Tu!

Waridi

JF-Expert Member
Mar 30, 2008
1,025
172
ASIKUDANGANYE MTU SISI WAAFRIKA(WATU WEUSI) KIBOKO!!!
Alexander mils aligundua lift ya maghorofa marefu
Richard spikes aligundua gia automatic ya magari
Joseph gammel aligundua internal combustion injini
Charles brooks aligundua fagio la barabara/mitaa
William Purvis aligundua pen ya fountain na mihuri
Lee burridge aligundua typewriter
Lovette aligundua printing mashine yenye uwezo mkubwa
Fredrick jones aligundua air conditioner/ kiyoyozi
Alice parker aligundua heating furnance
Lewis latimer aligundua taa ya umeme
Granville woods aligundua swichi ya kujizima- automatic
George Samson aligundua mashine ya kukausha nguo
John standard aligundua friji
E Bwana eeeH!!!!!!!!!!!!!!!!
Na msingi wa internet je? - Philip Emeagwali toka Nijeria!!!

Hizi figure zote nyeusi hapo sijakutajia mabingwa weusi wa karne za kale, wavumbuzi wa mahesabu na kadhalika. Watu weusi we acha tu, hivi leo marekani iko kama ilivyo kwa sababu ya figure hizo. Wakati bara la afrika linadoda, huenda sababu ni kuibiwa kwa hivi vichwa, jumlisha na brain drain ya sasa, ukiongeza na mafisadi walioko nyumbani balaa nuksi
 
One can equally come up with great achievement for any race.

Good pep talk for self esteem though, for those who need such fluff.
 
One can equally come up with great achievement for any race.

Good pep talk for self esteem though, for those who need such fluff.
Pundit,
sijamaanisha races nyingine hawana michango yao, ila
Dr Watson anayesema weusi hamna kitu, tunamdefeat kwa ushahidi huu, tena hata wenzetu wanaoamini kila kitu kafanya mzungu wapate ujumbe hapa kwamba si kweli
 
Marhaba, marhaba.

Na mimi nina maana hiyo hiyo.Uwezob wa akili maarifa hauendani na race, kwa hiyo kuna Waafrika wengi tu waliofanya kazi nzuri sana kama walivyo wazungu, wahindi, waarabu etc.

Sana sana tofauti zinatokana na sababu za mazingira, kitu ambacho kinaweza kubadili issue kutoka "Waafrika ndivyo tulivyo" kuja "maskini ndivyo tulivyo"

Jared Diamond kaongea vizuri sana katika "Guns Germs and Steel" kuhusu mambo haya.
 
Waridi
Hao wavumbuzi weusi walogundua hayo walogundua hawakufanya hivyo kwa sababu ya rangi ya ngozi yao. Naamini watu hao hao wangegundua yote hayo kama wangekuja duniani wakiwa katika race nyingine.....
 
Weusi wengi tu walishafanya maajabu ila siku zote historia hupotoshwa ama kutothaminiwa na watu ambao wao hujiona kwamba ni superior wa mwenzake.

http://www.drbencarson.com/

Ahsante sana Shomari, historia iliyopotoshwa ndio ambayo tuna wajibu wa kuirekebisha. Umefika wakati hata vitabu vya historia viache kutukuza watu wengine tu na kuacha kurecognize ushujaa na uwezo wa mtu mweusi
 
Waridi
Hao wavumbuzi weusi walogundua hayo walogundua hawakufanya hivyo kwa sababu ya rangi ya ngozi yao. Naamini watu hao hao wangegundua yote hayo kama wangekuja duniani wakiwa katika race nyingine.....

Mkuu katoto ka Mzungu,
Nakubaliana na wewe, lakini ipo haja ya kuutaja mchango huu wa watu weusi ili kudhibiti madhalilisho na uongo unaoenezwa na wabaguzi kwamba mtu mweusi ana uwezo duni kiakili akilinganishwa na watu wa rangi zingine. Uongo huu umeenezwa kwa muda mrefu kiasi kwamba wapo wenzetu wanaoamini kwamba kila uvumbuzi wa maana kafanya mzungu, kwa taarifa hii wajue kwamba si kweli.
 
Swali: Mbona hao watu weusi hawavumbui vitu vitakavyoifanya Afrika iondokane na umaskini na ufukara..?

Brain drain inaondoa human resource ya maana katika bara la afrika, usidhani yanaibiwa madini tu. wakishaondoka hao vipanga wetu kwenda kufanya mavituzi huko nje, nyumbani kunabaki wasanii na mafisadi wakishikilia madaraka na kuudumisha umaskini.
 
sasa hao vipanga mbona wasibaki home kuendeleza bara lao?Africa sijui kuna nini?haiwezekani nchi zote zikawa na mabaya yanayofanana?kidogo south AFRICA nako ni kwa sababu wazungu walikaa muda mrefu!kweli waafrica tuna matatizo!
 
Swali: Mbona hao watu weusi hawavumbui vitu vitakavyoifanya Afrika iondokane na umaskini na ufukara..?
Hivi wewe kumbe bado unaishi? ina maana kifo chako ilikuwa ni uvumi tu?
ahh kweli tatizo bado lipo..........
 
ukikaa ukafikiria na kuanza kuandika mafanikio ya mtu kwa kuangalia ngozi yake, ukaa tena na kufikria ukaanza kuandika mafanikio ya mtu au watu kwa ukabila wao, na hujachoka ukakaa tena na kufikria ukaanza kuandika mafanikio ya watu au mtu kwa udini wake jibu ni rahisI NALO NI-WEWE NI MMOJA WA WATU WANAOFIKIRI KIBAGUZI! NA WEWE NI MBAGUZI KWA NJANJA ZOTE.
 
Mkuu Mwakimbi,
Tuhuma zako si za kweli. Mtu anayeamua kuleta ushahidi kwamba mtu mweusi naye yumo katika uvumbuzi, ni mpinzani wa ubaguzi anaofanyiwa mtu mweusi kwa kudhalilishwa kwamba yeye ana akili duni as compared to races nyingine. Ushahidi unaotolewa hapa watosha kuwaziba midomo watu kama Dr.Watson wanaodai watu weusi ni duni.
 
Ukiangalia historia ya dunia sio miaka 500 iliyopita, kama 2000 iliyopita, race ya mweupe ni ya mwisho kustaarabika weusi walikuwa wa kwanza

1)Chunguza alphabet tunayoitumia sasa hivi source yake ni wapi?Ni waafrika wa egypt.
2)Oldest standing stone building in the world ipo wapi? afrika(ilijengwa 3000 bc)
3)Calendar tunayoitumia sasa hivi ilianzia wapi? Afrika.
4)Mzungu i.e wagiriki walichukua teknologia hii na kuiendeleza,lakini SOURCE kubwa ni waafrika.(soma aristotle,herodotus, sikiliza,wanasemaje kuhusu walipotoa elimu yao)
 
Hizo ni blah blah tu....hakuna lolote
 
Hizo ni blah blah tu....hakuna lolote

000-106-01-ruckus-front2-.jpg

Uncle Ruckus from "The Boondocks"
 
Swali: Mbona hao watu weusi hawavumbui vitu vitakavyoifanya Afrika iondokane na umaskini na ufukara..?

...Naam, kama Ethiopia! mimi hawa watu nishaanza kuwachoka, kila mwaka wao tu ndio wanakufa njaa afrika? Rais na watawala wao hawana hata haya?

mfano; How many times ( since 1985) kina Bono na Geldof waje na ideas za Live Aid, Sports Relief funds? Misaada inayotolewa inapotelea wapi!???

Hatuna raha, kila mwaka kwenye TV sura zao tu zimejaa manzi, na makamasi, tunaulizwa, Afrika ndivyo mlivyo?

Haya leo mmarekani katoa msaada wa $ 70m. Mwakani utawaona tena na mikamasi yao,...

...shame!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom