Watu Weusi Tuna Akili Ndogo?

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Padri Karugendo: Watu Weusi Tuna Akili Ndogo?

JAMES Watson, mwanasayansi maarufu sana duniani na mshindi wa nishani ya Nobel katika tiba mwaka 1962, ameleta mjadala mkubwa baada ya kudai kwamba mtu mweusi ana akili ndogo kuliko mtu mweupe. Kauli yake hiyo imeshikiwa bango na wapinzani wa ubaguzi wa rangi kwa kuwa inamdhalilisha mtu mweusi.

Huyu si mtu wa kwanza kusema hivyo, tofauti ni kwamba yeye ameisemea kisayansi zaidi. Siku za nyuma waziri mkuu mmoja wa Japan alipata kusema maneno kama hayo kwamba anatilia shaka uwezo wa mtu mweusi. Waziri mwingine wa Japan na yeye alishanukuliwa kusema hivyo hivyo. Wote baadaye waliomba radhi lakini ujumbe ulifika.

Chika Onyeani katika kitabu chake cha Capitalist Nigger naye anashangaa ni kwa nini Mwafrika atukanwe namna hiyo na mawaziri wa Japan lakini bado waendelee kununua bidhaa toka Japan. Anaelezea pia kwamba jamii yote ya watu weusi inafanana kwa kiasi kikubwa.

Kwa mfano ukikutana na Mmarekani mweusi aliyezaliwa na kukulia Marekani au Carribean au Afrika kwenyewe, bado wana tabia zile zile ambazo zinatia shaka kama kweli akili za Waafrika si ndogo kwa kiasi fulani.

Ukianza kuangalia matokeo mbalimbali yanayotokea Afrika, kuanzia enzi za miaka ya nyuma, unaanza kuwa na wasiwasi kuhusu hali na uelewa wa mtu mweusi. Historia inatuambia kwamba, hadi karne ya 16 kiwango cha maendeleo kati ya Ulaya na Afrika kilikuwa sawa.

Tunaambiwa pia kwamba miaka ya 1960 baadhi ya nchi za Kiafrika zilikuwa mbele kimaendeleo au katika usawa mmoja na nchi za Asia ambazo leo ziko mbali kimaendeleo. Bado unajiuliza ni wapi kwenye matatizo? Kwa nini Waafrika waachwe nyuma kila leo?

Inavyoelekea ni kwamba bara la Afrika linakuwa kama kigezo kizuri cha kupima maendeleo na mabara mengine. Ripoti za umasikini duniani zinaonyesha kwamba umasikini duniani umepungua kwa kiasi kikubwa lakini kwa Afrika unaonyesha kuongezeka. Mbaya zaidi hakuna ishara ya watu hao kutoka katika utando huo wa umasikini walikonasa kabisa.

Idadi ya watu waliopungua umasikini kidunia unatokana na kukua kwa uchumi wa China na India, nchi zenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani. Kwa hivyo, uwezo wao wa kupunguzia watu wao umasikini unachangia takwimu za kidunia zionekane nzuri lakini kwa Afrika hakuna mabadiliko mazuri.

Ukipima baadhi ya kauli za hawa tunaowaita wabaguzi utagundua kuna ujumbe wanawasilisha. Kama tukichukulia Tanzania kama mwakilishi wa Waafrika, tunaweza tukajadili baadhi ya hoja na kujipima ni kweli tuna akili ndogo kijenetiki au mazingira yetu yanatufanya tuwe na uwezo mdogo wa kutumia akili zetu au tujiulize ni wapi tumeteleza?

Tanzania hii ina rasilimali nyingi sana lakini bado hatujaweza kufika popote pa maana. Tunasaini mikataba ya hovyo kabisa ambayo inampa mgeni mamlaka ya kuchukua rasilimali jinsi anavyotaka huku wenyeji tukibaki hoi kabisa. Tuna mapori ya kutosha na mito na maziwa ya kutosha lakini bado tunaagiza chakula nje ya nchi.

Tuna watu wanajilundikia mabilioni ya fedha benki huku watu wa kijijini kwake hawana maji ya kunywa. Kuna watu wananunua samani za mabilioni ya Shilingi kwenye nyumba walizojengewa na Serikali wakati ambapo Shule ya Sekondari ya Azania, iliyopo katikati ya jiji kuu la nchi, ina wastani wa tundu moja la choo kwa wanafunzi 300!

Shule karibu zote mpya zilizojengwa, kuanzia za msingi hadi za sekondari, zina uhaba mkubwa wa vyoo. Hivi ni vitu vya msingi kabisa lakini bado hatujaweza kuvitatua.

Bado tunazipa likizo ya kodi kampuni kubwa huku tukifuatilia vikodi vidogo vidogo vya wafanyabiashara wadogo au hata wachuuzi. Kampuni kubwa zinaruhusiwa kubeba hasara na kuipeleka kwenye mahesabu ya mwaka ujao kwa miaka kadhaa lakini hiyo hiyo kampuni inayopata hasara inaendelea kufanya biashara!

Sasa hivi tunasifiwa kwa kuweza kufuatilia kodi kwenye biashara ndogo ndogo huku tukiwa hatujafanya lolote la maana kwenye kodi za makampuni makubwa. Uwezo wa Serikali wa ukusanyaji hupimwa na kuongezeka kwa kodi za makampuni makubwa (Corporate Tax) na si kuongezeka kwa kodi za mapato zinazotokana na kuajiri watu wachache.

Ni lazima tukae chini tujiulize: Kunani katika akili zetu? Tunavuna madini ya Tanzanite lakini hatuwezi kuyauza. Tunasema tuna mafuta lakini tukitaka kuyachimba tunamwita Mzungu, japokuwa tumekuwa tukizalisha wahandisi na wanajiolojia kila mwaka. Lazima tujiulize kama elimu yetu ina mushkeli au la!

Sasa hivi tunajigamba kuwa na vyuo vikuu karibia 30 lakini bado tunaagiza vijiti vya kuchokonolea meno kutoka Malaysia. Ni lazima tujiulize tulipoteleza. Ni lazima wakati mwingine tujiulize kama kweli hatuna mushkeli kwenye akili zetu.

Maamuzi yenye maslahi ya taifa yanachukua muda mrefu kuchukuliwa. Wananchi wamekuwa wakipigia kelele suala la Richmond lakini imechukua miezi kadhaa kuchukua uamuzi wa kulichunguza. Kampuni iliyoshindwa kazi.

Katika hali ya kawaida, ilibidi maamuzi ya haraka yachukuliwe na taarifa ipatikane ili wananchi waondoe hisia mbovu. Wapi? Imechukua miezi ndio maamuzi yanatoka. Ni dhahiri mazingira haya yataifanya hata taarifa yake itiliwe shaka.

Maamuzi yenye maslahi ya taifa yanatakiwa yachukuliwe mapema ili kusafisha hisia mbovu. Wenzetu wanaosemwa kuwa na akili kuzidi sisi leo wameweza kushughulikia mambo yenye maslahi ya taifa na kuondoa umimi kwanza. Ni lazima tujitathimini na kujiuliza kama kweli tuko sawa na wengine.

Kwenye makala yangu ya juma lililopita, nilitoa hoja kwamba tunajipima kwa viongozi wetu.Katika hali ya kawaida kiongozi wa watu maskini ni lazima aishi maisha yanayofanana na watu wake; maisha ya kimaskini. Lakini kama kiongozi wa watu maskini anaishi kwenye utajiri unaopindukia, ni lazima kuna kasoro.

Magari zaidi ya 30 yenye thamani ya Shilingi milioni 60 kila mmoja, kupita katika vijiji vya watu maskini kwa kisingizio cha kukagua maendeleo, ni jambo la kuleta mashaka kama kweli hatujateleza mahali au kuzua wasiwasi juu ya ubora wa akili zetu.

Viongozi wetu wanapokwenda kuomba pesa kule nchi za nje, wanafikia na kuishi kwenye mahoteli ya kitalii. Kwa nini akili zetu zisitiliwe shaka? Kiongozi wa watu maskini, anayekwenda kuomba misaada ya watu maskini, anafikia hoteli ya kitalii!

Yamekuwepo malalamiko ya chini chini ambayo kwa namna fulani ni matusi, kwamba wale wanaotoa pesa wakija kuzifuatilia, wanasafiri kwa usafiri wa kawaida. Kama ni ndege wanapanda daraja la tatu, lakini viongozi wetu wanasafiri daraja la kwanza!

Ipo mifano mingi inayoonyesha dalili nyingi za kuwafanya wenzetu wawe na mashaka juu ya ubora wa akili zetu. Mheshimiwa Ndesamburo, juzi, bungeni, alitoa ushuhuda kwamba asilimia 98 ya watu walio na simu za viganjani wanazitumia kutongoza wanawake, kuzungumza umbea, kutuma ujumbe wa mapenzi na kupanga mipango ya ujambazi. Labda asilimia mbili ndio wanatumia simu kwa mipango ya biashara na maendeleo.

Hili ni jambo la kushangaza kwani Tanzania ni kati ya nchi zinazosifika Afrika kwa kuingiza kwa wingi simu za viganjani na makampuni ya simu hizi yanapata faida kupindukia.

Siku za karibuni Benki ya Dunia ilitoa taarifa ya mamilioni ya dola zilizotolewa barani Afrika kwa ajili ya kukuza kilimo lakini wanashangaa na kujiuliza; mbona mapinduzi ya kilimo kwa bara la Afrika hayajafanikiwa kama ilivyotokea Asia?

Najua vyombo hivi navyo vina unafiki wa kutosha kwa sababu wanatumia nchi masikini kujineemesha pia. Lakini cha kujiuliza mbona fedha za namna hiyo zimefanya mapinduzi sehemu nyingine? Kwa nini zisifanye mapinduzi Afrika? Kwa nini tukubali kutumiwa kama nguruwe wa majaribio na sisi tusifaidi kama nchi nyingine?

Tunapaswa kujitathmini hapa. Mara nyingi sana wanaharakati wanaopingana na misaada ya nje huwalaumu watoaji kwamba wanakuja na misaada yao kuja kuitumia huku kwetu wakijineemesha wenyewe. Mimi huwa nauliza kama umeona msaada hautafaidisha taifa kwa nini uukubali?

Kwa hivyo tunawalaumu pia wanaopokea misaada isiyo na tija. Lakini wanaopokea wanaangalia maslahi yao binafsi kwamba watafaidi wao na si taifa. Wenzetu wa Asia wanawarudishia wataalamu wa Benki ya Dunia na IMF fedha zao kama wakigundua hazitakuwa na manufaa, na ndio maana kuna ushahidi wa kitaaluma kwamba mikopo na misaada mingine imeweza kusaidia sana kuleta mapinduzi Asia. Sisi bado tunalia. Tujiulize tatizo lilipo.

Tutalaani wabaguzi hawa, tutashika mabango na kuandamana lakini kabla ya kwenda tujiulize sababu ya kukwama kwetu. Tusikimbilie kulaumu Wazungu kama chanzo cha matatizo yetu.

Kuna wale rafiki zangu wanaolaani ukoloni na ukoloni mamboleo. Malaysia na Ghana zilikuwa zote koloni la Uingereza na zilipata Uhuru mwaka mmoja (1957). Wamalaysia walikuwa wanakwenda Ghana kujifunza kilimo cha mawese. Leo hii Ghana inajifunza kila kitu toka Malaysia kikiwemo kilimo cha mawese!

Tanzania ni mika 46 ya Uhuru sasa. Tuache kuendelea kulia na kulalamikia ukoloni. Sisemi haukuleta madhara lakini tutalia mpaka lini? Tunachukua hatua gani za kuondoa hayo makovu? Au hatua zenyewe ni hizo za kuwaita tena wakoloni waje kuwekeza kwa kuwasamehe kodi?

Hawakatai kuja. Watakuja watatula halafu watatutukana. Hawasemi hadharani lakini wanasemea chinichini kwamba hawa Waafrika ni wajinga.

Wazungu wengi wanaobishana na kauli ya Watson si kwamba wanasikitika sana. Wanaonyesha usoni kwamba wamechukia lakini moyoni wanasema ni kweli hawa wana ujinga wao mkubwa. Wanatutetea ili waendelee kutuvuna. Hawataki tukae chini na kujitathmini tulipoenda mrama.

Nachukia sana kuitwa kiumbe dhaifu hasa kiakili. Nachukia kwa sababu naupenda Uafrika na weusi wangu. Nawapenda Waafrika wenzangu. Nachukia sana wanapoambiwa kwamba wana ubongo dhaifu. Lakini nahisi kuna mahali kama watu weusi tumeteleza.

Kuna ushaidi unaoonyesha kwamba tumefanya mambo ambayo akili zetu zinatakiwa zihojiwe. Kama mtu anaiba mabilioni ya fedha za umma kwenye nchi masikini na kuyaweka Ulaya au kuwekeza mahali popote, huku kukiwa na wananchi wanaokufa kwa kukosa dawa ya Malaria, basi, tuna ulazima wa kujiuliza tuliko na kasoro.

Kama viongozi wanawaibia wanachi wao waliowachagua kuwawakilisha bila aibu yoyote inabidi tuhoji akili zetu. Kama wananchi nao wanaridhika na hila za viongozi wao bila kuchukua hatua madhubuti, basi tuhoji akili zetu.

Kama kijenetiki tuna akili ndogo, basi, hatuna cha kufanya labda ufanyike utaratibu wa kutuunganisha kijenetiki na hao wenye akili zaidi. Kama akili ndogo zinatokana na kukataa kutumia uwezo tuliopewa basi tunaweza kujirekebisha.

Hata kama Watson ataomba radhi kama wale mawaziri wa Japan walivyofanya, atakuwa ameshapeleka ujumbe mzito wa watu weusi kujichunguza! Ujumbe huu ni mzito kwa taifa letu la Tanzania.
 
Hilo hata kaburu Botha alisha wahi sema muda mrefu Sana na ndo ukweli wenyewe akili zetu niza hovyo Sana.

Leo hii mwafrika yuko bize kujadili Yesu alikuwa Mwafrika sijui agundue kitu gani kwamba Yesu alikuwa Mwafrika sijui itasaidia Nini?

Tanzania mpaka Sasa tuna miaka 60 ya Uhuru lakini tunasaidiwa pesa na wazungu kwa ajili ya kujenga matundu ya vyoo mashuleni na wakati huo huo serikali kupitia viongozi wake wanatumia 500m kununua v8 Sasa huu si uzwazwa.

Unaweka bajeti tatribani bilioni moja na kitu ili kukimbiza Mwenge wa Uhuru badala ya pesa hizo kutumika kupeleka maji vijijji au kujenga vituo vya afya huu si ujinga.

Wasomi wasio jua thamani ya taalumu zao wako Afrika mfano ni hapa Tanzania kipindi Cha Corona madaktari bingwa wa hospital ya taifa Muhimbili kukubali kujenga mtambo wa kupinga nyungu

Angalia mipango miji yetu yaani vitu hovyo hovyo kabisa,kuweka system tu za maji taka na maji Safi hatuwezi.

Wakoloni walipo ondoka Afrika waliacha viwanda,mashamba,huduma za kijamii na uchumi katika hali nzuri walipo ingia waafrika wakoloni wapya na sera zao Mara ujamaaa waliharibu kila kitu.

Wakuu endeleeni

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mbona hujasema tunatumia gharama kubwa na mda mwingi kuabudu Mungu wa kizungu na Kiarabu huku tukiambiwa tuna laana za mababu majina yao na tamaduni zao hatupaswi kuzifuata Tena, Ili tusalimike tunabidi tutumie mafuta na maji ya upako tunachangishana mamilion kujenga kanisa wakati mtaani hatuna maji safi Wala, huduma nzuri za afya na elimu WAAFRIKA TUNAUMWA
 
Huu ni ukweli mchungu sana na kwa sababu hiyo akitokea kiongozi mwenye maono au uwezo mkubwa atapata upinzani mkubwa sana na kuitwa majina yote mabaya kwa kuwa annaongoza kundi kubwa la watu wenye uwezo duni.
Binafsi huwa na tafsiri yangu kuhusu mtu mwenye akili kubwa au nyingi. Naamini akili kubwa mtu anazaliwa nayo na hii ni zawadi kutoka kwa Mungu na wala sio kwamba kuwa na Elimu kubwa ni kuwa na akili nyingi. Elimu inakwenda kuongeza maarifa kiasi kwenye akili ambayo mtu tayari amezaliwa nayo .

Ndio maana Kama ni wasomi wakubwa Afrika wapo lakini bado matatizo chungu nzima yamejaa na yanawasumbua wananchi lakini wasomi hawayatatui na hata miongoni mwa hao wasomi wakiwepo wenye akili kubwa na kutaka kuyatatua matatizo hayo, kunamifumo inayosimamiwa na watu wengine inakwamisha.

Huu uzi umeanika ukweli mtupu kuhusu dhna ya mtu mweusi hasa muafrika. Ukikutana na muafrika aliyeishi na mzungu kidogo utagundua kuwa yeye anauwezo mkubwa kidogo na ustaarabu wa kufanya mambo. Kuna waafrika wengine wenye uwezo mkubwa na ustaarabu na hawajawahi kuishi na mzungu, inafika wakati watu wanampachika jina kuwa fulani yule ni mzungu hii inatokana na jinsi anavyobehave.

Mimi huwa nashangaa sana muafrika kusema kuwa anabaguliwa na jamii nyingine kuwa ana uwezo mdogo. Ikiwa tuna ardhi nzuri mvua za kutosha mito ya kutosha mabonde halafu tunalalamika njaa hivi hapo hata kabla mtu hajakuambia hauna akili inapaswa mwenyewe ugundue hilo.

Niseme wazi wazungu huwa wanashanga sana kuona kuna mtu mwenye uwezo mkubwa yupo Afrika au ni mtu mweusi na akitokea mtu kama huyo wao hawawezi kumpenda hasa akiwa anatishia maslahi yao.
 
Mwenda zake mara kwa mara alionyesha wazi kukerwa na hawa tunaowaita wazungu. Alikerwa zaidi na unafiki wao juu ya waafrika. Aliwahi kusema; wazungu utajiri (mali) zao chanzo chake ni Afrika, na mpaka leo hii bado wanavuna baadhi ya sehemu.

Aliendelea kusema, linapokuja suala la kutoa misaada; wanatoa misaada na masimango juu, wanakupa msaada huku wanasema ''this country is very poor'', ilhali hicho wanachokupa wamekitoa kwako, na utakilipa na riba juu.

Ni kweli inafikirisha sana ukijiuliza swali; kwamba hawa wenzetu (weupe) walituzidi vipi ilhali duniani tulikuja wakati mmoja? Je, ni kweli Mungu aliwapendelea wao kwa kuwapa akili nyingi kuliko sisi weusi?

Hapana, Mungu sio binadamu (wengine wanasema Mungu sio Athumani), na kwa hivi hana upendeleo, alitupatia wote akili sawa.

Umeongelea mazingira, hilo ndio jambo lililopelekea hawa wenzetu kutuzidi akili. Walikuwa hawana namna ya kuendesha maisha yao kwa maana ya rasilimali asilia, sasa wangefanyeje? Wafe njaa? Lazima wachekeche akili ili waweze kuishi (survive). Ndipo linakuja suala la mazingira kubadilisha akili ya binadamu.

Utafiti unaonyesha kuwa, mnyama Twiga, wa mwanzo kabisa alizaliwa na shingo ya kawaida kama wanyama wengine, yaani shingo fupi. Lakini mahali hapo alipozaliwa palitokea majanga, majani yaliyoota chini yaliungua na hivyo kubaki majani ya juu kwenye miti mirefu. Ndipo mnyama Twiga akaanza taratibu kunyoosha (stretch) shingo yake kuelekea juu ya mti akitafuta namna ya kupata majani ili ale.

Ni kwa mazingira haya, shingo ya Twiga ikarefuka, na kubadili moja kwa moja genetic yake mpaka leo hii. Kwa kuwa alibadili genetic, basi hata watoto aliowazaa wakawa kama yeye, yaani wenye shingo ndefu.

Wazungu nao walibadili genetic baada ya kuwa subjected katika mazingira magumu, na kwa hivyo vizazi vyao vyote vitaendelea kuwa hivyo, kwa kuwa hiyo ni 'genetic'.

Labda na sisi (watu weusi) mpaka tutakapokutana na mazingira magumu ndio tutabadili genetic na kuwa wenye akili, lakini kwa sasa bado sana.
 
Watu weusi wana matatizo ns ujinga wa asili.

Hatuwezi na hatutaweza kuwa juu ya race yoyote hapa duniani. Sisi ni watumwa wao milele

Hata hapa nchini kwetu katika ardhi yetu watu weusi ni watumwa kwenye viwanda na makampuni ya Wazungu, Waarabu na Wahindi na wanalipwa mishahara ya hovyo

Ndani ya ardhi yetu Dada zetu ndio wanatawaza mavi ya watoto wa kiasia na kiarabu na kulipwa hela ndogo sana

Hatupendani, tunauana wenyewe

Tuna laana ya asili na itadumu hivyo.
 
Ukitaka kujua sisi hatuna akili angalia yafuatayo
1) angalia ushaghala bagala pale stand ya mkoani mbezi
2)angalia maamuzi wa wakuu wetu yalivyo
3) mtu anasimama barabarani / kituo Cha basi anapiga debe wakati Kila aliepo kituoni anajua anapokwenda
Mfano ni mingi
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom