Wildlifer
JF-Expert Member
- May 12, 2021
- 1,883
- 5,186
1. MUHAMMAD (a.i.j.y/p.b.u.h/s.a.w)
Huyu ni mtume wa Mungu katika imani ya Dini ya Kiislam. Ndiye aliyeteremshiwa kitabu cha Quran Tukufu na kuasisi Dini ya Uislam. Matendo yake, maisha yake, mafundisho yake yamekuwa na ushawishi mkubwa na kuitengeneza dunia kuwa hivi ilivyo leo.
Ushawishi:
Wafuasi
—Muhammad anawafuasi takribani Bilioni 1.8 (mwaka 2018) takribani asilimia 25 ya watu wote duniani, ambao ni waumini wa dini ya kiislam.
Mtindo wa maisha
—Wapo watu (Mamilioni) wanaofuata mtindo wa mavazi wa Mtume Muhammad wa kuvaa suruali zisizovuka kifundo cha mguu, wapo wanaofuga ndevu na kuzinakshi kama alivyofanya yeye. Kwa ujumla, kundi hili la watu huyaigiza matendo ya Mtume Muhammad.
Vikundi vya kianaharakati
—Leo dunia inashuhudia vikundi vingi vyenye harakati ambazo zinatokana na mafunzo ya Mtume Muhammad katika maisha yake au Quran. Vikundi/harakati kama Al Qaeda, ISIS n.k.
Serikali
—Kupitia mafunzo yanayohimiza Uislam kushika hatamu ya mifumo yote ya maisha, leo dunia ina nchi 57 ambazo uislam ndio dini yao rasmi na mfumo wa uongozi. ⅓ ya serikali zote duniani, zimetokana na ideas za Mtume Muhammad. Brilliance!
Uchumi
—Kusanyiko kama la Hijja, hukusanya watu Milioni 2.5 kwa mwaka kutoka kila sehemu ya ulimwengu.
Kwa ujumla, mafunzo ya Mtume Muhammad yametumiwa na Mamilioni ya watu duniani, katika namna zote mbili (amani na vurugu).
YESU KRISTO.
Kama alivyo Mtume Muhammad, Yesu ndiye kinara wa dini ya Ukristo.
Ushawishi wake:
Wafuasi
—Takribani asilimia 32 [2.3 Bilioni] ya watu duniani ni wafuasi wa mafundisho na maisha ya Yesu Kristo. Hivyo; Muhammad na Yesu, wanaushawishi kwa zaidi ya Nusu ya watu wote duniani.
Serikali
—Kati ya serikali zote 195 duniani, Serikali 13 Ukristo ndio imani kuu ya nchi zao.
Vikundi vya kianaharakati
—Vipo vikundi ambavyo harakati zao (aidha za amani au vurugu), zinatokana na fikra au mafunzo ya Yesu Kristo kutoka kwenye Biblia. Vikundi kama Ku Klax Klan, Arm of God, au Lord Resistance Army vimekuwa na harakati ambazo zimechochewa na mafunzo hayo.
Uchumi
—Waumini wa Ukristo wamekuwa wakifanya ziara kutembelea maeneo mbalimbali ambayo yamesukumwa na mafunzo ya Ukristo. Maeneo kama Jerusalem, Roma, Nidaros, Santiago de Compostela n.k! Hutembelewa na mamia ya waumini hivyo kuwa sehemu ya uchumi wa dunia kwenye sekta ya utalii kwa vitu kama usafiri na mahoteli n.k
Yakadiriwa watu zaidi ya Milioni 1 (kwa miaka kumi-2007 hadi 2018), wameuwa kwa visa vya Ugaidi wa Kiislam na kikristo duniani.
KARL MARX
Huyu alikuwa ni mjerumani, aliyezaliwa nchini humo mwaka 1818 na kufariki London mwaka 1883. Huyu alikuwa ni mwanafalsafa wa kikomunist na mkosoaji mkubwa wa Ubepari. Watu mashuhuri kwenye historia kama Lenin, Stalin, Che Guevara, Mao, Nyerere, Sankara, Allende, Castro, Chavez n.k wote hawa msingi wao ni Karl Marx.
Katika maisha yake, Karl Marx alitoa kazi mbili ambazo zimeutengeneza ulimwengu kuwa hivi ulivyo sasa. Das Kapital—ambayo iliukosia mfumo wa Ubepari, na Communist Manifesto—ambayo ilieleza ni kwa vipi serikali ya kikomunist inapaswa iwe.
Ushawishi:
Mapinduzi
—Takribani miaka 70 toka Ilani ya wakomunist ichapishwe, Mawazo hayo yaliwekwa kwenye vitendo na warusi chini ya Vladimir Lenin na kufanya mapinduzi mwaka 1917 na kuweka serikali ya kikomunist. Serikali hii ndio ikawa moto wa nyika na kuanza kusambaza imani hii maeneo mengine, na kuziteka nchi jumla 14 kama Russia, Ukraine, Georgia, Belorussia, Uzbekistan, Armenia, Azerbaijan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Moldova, Turkmenistan, Tajikistan, Latvia toka 1922 hadi kuanguka kwake mwaka 1991. Uwepo wa Soviet/marxism , ulizaa mapinduzi kwenye nyingi kama Congo, Cuba, China, Zanzibar, Bolivia, Brazil, Chile n.k
Vikundi vya kianaharakati
—Historia imeonyesha kuwa mawazo yamekuwa ni jambo hatari kuliko Silaha. Ideas ndio huwapa sababu ya watu kufyatua risasi. Ideas za Marxism, zilihamasisha matumizi ya vurugu katika kuifikia nchi ya kikomunist. Kutokana na mawazo hayo, dunia imeshuhudia vikundi kama 19 May Communist Organization Sandinistas, Shining Path, 19th of April Movement, na Revolutionary Armed Forces of Colombia (FARC). Vikundi hivi vimeendesha vurugu na mauji makubwa sana ulimwenguni. Yakadiriwa watu Milioni 100 hadi sasa wameuawa kutokana na ushawishi wa fikra za Karl Marx.