Watu wenye umri mrefu duniani wapatikana Japan

Chibudee

JF-Expert Member
Dec 28, 2016
1,775
2,397
Mtandao maarufu wa kutunza rekodi duniani "Guiness World Records" umemtaja na kumkabidhi cheti bwana Chitetsu Watanabe kutoka Niigata Japan, kama ndiyo mwanaume mwenye umri mrefu zaidi duniani akiwa na miaka 112.

Bibi Kane Tanaka na Babu Chitetsu Watanabe, waliovunja rekodi ya kuwa na umri mrefu zaidi Japan

Babu huyo Chitetsu Watanabe ni mtoto wa kwanza kati ya watoto 8 kutoka kwa Baba yake na Mama yake na amezaliwa Machi 5, 1907.

Kwa mujibu wa mtandao huo umempongeza mzee huyo kuwa mwanaume mwenye umri mrefu duniani kwa sasa, mwenyewe amesema siri iliyomfanya kufikia umri huo ni kutokuwa na hasira bali kuendelea kuwa na tabasamu usoni mwake.

Historia yake inaonesha mzee huyo alikuwa ni mwanajeshi na amepigana vita ya mwaka 1944, kisha akaastaafu na sasa anajishughulisha na kilimo.

Aidha kutokea hukohuko nchini Japan bibi wa miaka 117 Kane Tanaka, amekabidhiwa cheti kutoka mtandao huo wa rekodi kwa kuwa mwanamke mwenye umri mrefu zaidi duniani.

20200213_104139.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NATAMANI SANA NA MIMI NIJE KUFIKIA UMRI KAMA WAO, HONGERA SANA KWAO BABU NA BIBI

inategemea na umbo lako mkuu, watu wafupi huwa naona hawazeeki haraka kama warefu. japo kwa binafsi yangu kiukweli umri wa kuzidi 90 sitamani kufika
 
inategemea na umbo lako mkuu, watu wafupi huwa naona hawazeeki haraka kama warefu. japo kwa binafsi yangu kiukweli umri wa kuzidi 90 sitamani kufika
Kwanini mkuu hautaki kujionea mengi yajayo ya dunia hii? Ile pia ni mojawapo ya baraka
 
NATAMANI SANA NA MIMI NIJE KUFIKIA UMRI KAMA WAO, HONGERA SANA KWAO BABU NA BIBI
... hayo sio mambo ya kutamani wala kuomba bali ni baraka tu kutoka kwa Mungu. Mungu akipenda atakupa lakini sio wewe kuwa na tamaa ya kukipata - baraka mtu hupewa bila kustahili.

"Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani, akamwambia, Omba utakalo nikupe. Sulemani akamwambia Mungu, Umemfanyia baba yangu Daudi fadhili kuu, nawe umenimilikisha mimi badala yake. Basi sasa, Ee BWANA Mungu, na limyakinie baba yangu Daudi neno lako; maana umenitawaza niwe mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya nchi. Basi sasa nipe hekima na maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi? Naye Mungu akamwambia Sulemani, Kwa sababu neno hili lilikuwamo moyoni mwako, wala hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu, wala maisha za wakuchukiao, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; bali umejitakia hekima na maarifa, ...."
 
Kwanini mkuu hautaki kujionea mengi yajayo ya dunia hii? Ile pia ni mojawapo ya baraka

umri ukashaenda sana huwa ni taabu kwa watu wengine (unless uwe na presa za kutosha) na mbaya zaidi unakuta hata age mates wengi washafariki.

kilichonihudhunisha zaidi ni kuwaona wazee wakizika watoto wao huku wao wakiwa hai, huwa ni mateso sana
 
N
... hayo sio mambo ya kutamani wala kuomba bali ni baraka tu kutoka kwa Mungu. Mungu akipenda atakupa lakini sio wewe kuwa na tamaa ya kukipata - baraka mtu hupewa bila kustahili.

"Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani, akamwambia, Omba utakalo nikupe. Sulemani akamwambia Mungu, Umemfanyia baba yangu Daudi fadhili kuu, nawe umenimilikisha mimi badala yake. Basi sasa, Ee BWANA Mungu, na limyakinie baba yangu Daudi neno lako; maana umenitawaza niwe mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya nchi. Basi sasa nipe hekima na maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi? Naye Mungu akamwambia Sulemani, Kwa sababu neno hili lilikuwamo moyoni mwako, wala hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu, wala maisha za wakuchukiao, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; bali umejitakia hekima na maarifa, ...."
NI KWELI MKUU NI BARAKA ZAKE MUUMBA JAMBO BINADAMU HULKA YETU NI KUTAMANI
 
N
NI KWELI MKUU NI BARAKA ZAKE MUUMBA JAMBO BUNADAMU HULKA YETU NI KUTAMANI
... ya nini kutamani kitu ambacho hata ujisumbue vipi huwezi kujiongezea yodi moja wala nukta moja? Mali, elimu, n.k. waweza kujihangaisha kwa bidii zako ukafanikiwa kufika mahali fulani lakini sio UHAI Mkuu. Huo uko ndani ya mamlaka yake mwenyewe aliyekupa na anao uwezo wa kuutwaa muda apendao. "Bwana alitoa na Bwana ametwaa; JINA lake lihimidiwe". AMEN; andiko hilo linazungumzia UHAI.
 
NATAMANI SANA NA MIMI NIJE KUFIKIA UMRI KAMA WAO, HONGERA SANA KWAO BABU NA BIBI
Issue hapo ni kukwepa mishale,maana dunia ya leo yenye vyombo vya usafiri kama bodaboda,gari ndogo,mabasi,malori,ndege,meli yaani vyote vikukose,inakuja magonjwa kama malaria,typhoid,ukimwi,cancer,pressure,kisukari n.k vyote vikukose,hapo bado kuna majanga kama matetemeko,mafuriko,vimbunga n.k.kwakweli ukifika umri huo ni jambo la kumshukuru sana Mungu kwa neema zake na wala haitakuwa kwa ujanja wetu...
 
inategemea na umbo lako mkuu, watu wafupi huwa naona hawazeeki haraka kama warefu. japo kwa binafsi yangu kiukweli umri wa kuzidi 90 sitamani kufika
Sio kweli Japan wanakula sana samaki, hawali redmeat na vyakula vyao vingi vya kuchemsha na vegetarian
 
Back
Top Bottom