Watu wenye silaha washambulia eneo la watalii Mali

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Vyombo vya Usalama nchini Mali vinasema vimeokoa zaidi ya wageni thelathini kutoka katika kituo kimoja cha Utalii, kilichokuwa kikishambuliwa na watu waliokuwa na silaha.

Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Salif Traore amethibitisha kuuawa kwa watu wawili, baada ya watu wanaohisiwa kuwa ni wapiganaji wenye itikadi kali kushambulia eneo hilo la starehe la Le Campement Kangaba lililoko nje ya mji mkuu wa nchi hiyo Bamako.

Kwa mujibu wa Waziri huyo wa Usalama, mmoja wa washambuliaji hao alifanikiwa kutoroka, baada ya kujeruhiwa, huku akiacha bunduki na chupa zilizokuwa na vifaa vya milipuko. Aidha amesema watu wawili akiwemo raia mmoja pia walijeruhiwa. Majeshi ya Mali na Ufaransa yalifika katika eneo la tukio.

Kituo hicho cha utalii ni maarufu nyakati za juma la wiki na kuwa kivutio kwa raia wa Mali wenye uwezo na wale wa kigeni wanaoishi Bamako.

Mapema mwezi huu, Ubalozi wa Marekani mjini Bamako ulionya uwezekano wa kutokea mashambulizi katika siku za baadaye katika majengo ya wanadiplomasia wa magharibi na maeneo mengine katika mji wa Bamako ambako raia wa nchi za magharibi wanapenda kwenda.

Wapiganaji wa Kiislamu wameendelea kufanya mashambulizi nchini Mali licha ya kupoteza maeneo yao wanayoyashikilia wakati wa uvamizi uliofanywa na majeshi ya muungano yaliyokuwa yakiongozwa na Ufaransa mwaka 2003.


Chanzo; bbc swahili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom