Watu wenye roho mbaya ndio wanaofanikiwa maishani

WATU WENYE ROHO MBAYA NDIO WANAOFANIKIWA MAMAISHANI.

Dunia imebeba watu wa kila aina,wachapa kazi ,waviviu,wanyonyaji,majizi ,wachawi nk.
Kuna makundi ya tabia mbali mbali, kuna wapole ,wenye roho mbaya,wakali,wasamalia,wenye roho nzuri nk.
Sasa basi hapa nawazungumzia watu wenye roho mbaya,wanavyoweza ku survive na kutusua kimaisha,
Cha kwanza hili kundi huwa na shauku ya kufika mbali kimafanikio, hivyo wanapokuwa katika utafutaji huwa hawana mzaha na kitu kinaitwa pesa,

Mnaweza mkafanya nae dili,halafu dili mfanikishe ujifanye unataka kumzima,
Ohoo!!! my friend utajuta, huwa hawakubari atahakikisha unampa chake,kivyovyote vile utampa tu,
huwa hawaachi nyuma hata shilingi

Hata katika familia/ukoo hawa watu huwa wanajulika,huwa hawaangalii wewe ni nani na unaukaribu nae vipi,huwa hawabebi watu wazembe hata kidogo, na huwa hawatoi misaada kizembe, eti unakuja unasema mimi ni mtoto wa mjomba wako,nimetokea kijijini nimekuja kukusalimia,huna la maana lolote mbona utarudi mwenyewe bila kuambiwa,

Hakuna kucheka na mtu ,huwa wanapenda sana kutumia Wathesalonike 3:10 Kwa wale wavivu hawatanielewa, Kwa watu wa namna hiyo ndugu wapenda kitonga(kupe ) huwa hawakanyaji, na hubakia na maneno ya lawama tu ,

Roho mbaya hupelekea kutochezewa,kudhurumiwa,mali zako kutochezewa,kupe kukaa mbali na wewe,hata majirani hukutambua na kutoleta mazoea ya kijinga,hata mtu akija kwako anakuja na hoja inayoeleweka na si vihoja vya kipambe,

ROHO MBAYA NI KINGA ZIDI YA WANYONYAJI
Husaidia kujiimalisha kiuchumi na kufikia malengo, hukufanya kuto kuingiza bajeti zinazoibuka zisizo na msingi, sio kidogo tu flani amekumbwa na shida, unazama mfukoni na kupangua mipango uliyoiandaa, na husadia kuto sumbuliwa hovyo

LENGO NI NINI?
Lengo ni kujichimbia mizizi kiuchumi,kama ni mti basi tungesema mti wenye mizizi mirefu kwenda chini,ambao hata kimbunga kikija si rahisi kuuangusha,

Hapo sasa ndio unaweza ukabadilika kidogo na kuwa na roho nzuri,Kwa sababu mizizi yako imejichimbia chini, hata watu wakining'inia kwenye matawi yako huta anguka, utaishi vizuri na uzee wako utaumaliza vizuri bila kuwa msumbufu au ombaombaView attachment 1201404

"Ishiwa damu utapata wa kukuongeze, ukiishiwa pesa hutapata hata salamu"
Sahihi kabisa,jamaa kwenya pesa hawana mzaha,kwenye miradi yao wafamyakazi hudhurumia malipo yao au kulipwa kiduchu. Hata uwe mnyenyekevu kivip kwao mwisho wa siku utafukuzwa kama mbwa.
 
Roho mbaya haisaidii, nimewasaidia wengi sana na sasa hivi nakula matunda yake..
Hongera kama umebahatika,lakini kibongo bongo ukimsaidia mtu tegemea mbeleni kuja kuwa adui wako mkubwa
 
Ungesema wanaroho ngumu/makauzu /wazee wa maamuzi magumu sawa ila roho mbaya uko ni negative haswa.

Hatupaswi kuwa na roho mbaya kwani ni dhambi na ubaya, ukiwa na rohombaya uwezi kuwa na network ya biashara pia uwezi pata wateja wa kudumu kwakuwa watakuchukia.

Ili ufanikiwe ni vizuri kuwa na roho ngumu nanapo sema roho ngumu namaana kwamba kuna vitu yaani wewe unaweza fanya bila kuangalia jamii itakuonaje ilimradi sijambo la ubaya mfano kutomuachia mtu chenchi hata kama ni 50/=, peke yako kugoma kutoa mchango wa harusi wa jamaa yenu, unasaidia kulingana na bajeti yako,ndoa yako haina sherehe, kama ni kijana wewe unakuwa upendezi kama vijana wenzako kwenda na fashion no, usaidii ndugu bila sababu maalumu,nk
 
Ni mulemule tu
 
Back
Top Bottom