Watu wenye ajira tunaomba mtusaidie sisi ambao hatuna ajira

Mkuu mimi mwenyewe nilianza sina chochote kama yeye, tena yeye ana bahati ana hela ya bundle na smart phone anaingia JF ila niliweza

Ni kweli anaweza akakosa hiyo laki moja ya mtaji lakini ana simu ya laki nne, tatizo letu vijana ni hadi umwambie hii ni hela ya mtaji ndio anaanza hatuwezi jiongeza kabisa

Kujiajiri ni vita ambayo unatakiwa ujikane mwenyewe (kwa sisi ambao kwenye familia zetu ndio tunatoboa horizon),unaweza kaa mwaka mzima hujapata project wala nini, unasonga mbele .

Kwa hiyo [HASHTAG]#christelly[/HASHTAG] naelewa jamaa anapitia nini. Kama mimi nilifanikiwa na yeye atafanikiwa tu, ajipe moyo
sijawahi kutumia simu ya laki nne, simu ninayotumia ilinunuliwa kwa shilingi elfu tisini, ni Itel mkuu.
 
Unatangaza kitu baada ya kufanya utafiti na kufanikiwa la sivyo ni ukurupukaji. Kwa mtindo huo nani akuajiri ili uje uharibu sifa ya shule yako. Tafakari kwanza
asante mkuu, ubarikiwe sana. ukitaka kujua siri ya mtungi uliza kata. kuna watu tunalaumiwa na kuhukumiwa isivyostahili. Aliyeshiba hamjui mwenye njaa. Mungu aendelee kukujalia maisha mazuri, na kama inampendeza nami niendelee kuangaika
 
Baada ya kumaliza masomo ya ualimu shule ya msingi (sanaa)mwaka 2014 nilikaa kama miezi sita bila kusikia chochote kuhusu ajira,ndipo nilipoamua kuanzisha chekechea za mtaani yaani,nikakodi nyumba(hapa nilipo vyumba siyo bei ghali)nilianza na mtoto mmoja wa nyumbani na kwa sasa nina kama watoto 85 hv na bado nimefungua tena kuna watoto kama 28 hv japo hvyo vituo havijasajiriwa lkn naendesha kigumu na maisha yanaenda najua changamoto ipo imagine umemaliza chuo kikuu harafu uanze kuruka ruka na watoto wa miaka 4,5,6 mpk uamzi utoke moyoni.Je mazingira uliyopo kazi kama hii inaweza kufanyika.Kwa hayo machache yanatosha kwa maelezo zaid utanitafta.
 
kwa mazingira niliyopo kazi hii haiwezi kufanyika. nursery schools zipo za kutosha. pia nilishawahi kutangaza tuition wala sikuambulia kitu. asante kwa ushauri
 
Daah!! Alafu ukisema wanakuita mpiga dili... acha nikae kimya tu...hata sisi tunapitia huko mkuu pole sana!!
 
kwa mazingira niliyopo kazi hii haiwezi kufanyika. nursery schools zipo za kutosha. pia nilishawahi kutangaza tuition wala sikuambulia kitu. asante kwa ushauri
Mkuu kwa nini hutaki kutoka Dar uzitafte fursa mikoani???na umeshasema huko siyo kwenu umeenda kwenye interview hebu fanya mchakato wa kurudi mkoa then utazame fursa za vijijini kama kilimo kisha baada ya miezi 4 urudi kutupa mrejesho.Mm nilikuwa na hali ngumu kuliko unavyofikiria ila vichekechea vyangu vimenipa nguvu ya kufanya vitu vingi sana ikiwemo kilimo na projects zingine.
 
Daah!! Alafu ukisema wanakuita mpiga dili... acha nikae kimya tu...hata sisi tunapitia huko mkuu pole sana!!
asante sana. Kama Mungu ni wa wote nasi ipo siku yetu tu. Tushikamane, tunaoujua ukweli tuendelee kuamini ukweli wetu huo, siku zote aliyeshiba hamjui mwenye njaa, wanatengeneza matatizo kisha siye ndio tunaitwa matatizo, anyway Mungu ndiye mlipaji.
 
Ajira nchi zilianza kuwa tatizo tangia mwaka 1993. Tulitoka UDSM tukaweweseka na bahasha za KAKI . KUNA WALIOKUFA ILA wengine bado typo mpaka Leo tuna shughuli za hapa na pale. KIJANA OMBA UZIMA HAYA YATAPITA.
 
Mkuu kwa nini hutaki kutoka Dar uzitafte fursa mikoani???na umeshasema huko siyo kwenu umeenda kwenye interview hebu fanya mchakato wa kurudi mkoa then utazame fursa za vijijini kama kilimo kisha baada ya miezi 4 urudi kutupa mrejesho.Mm nilikuwa na hali ngumu kuliko unavyofikiria ila vichekechea vyangu vimenipa nguvu ya kufanya vitu vingi sana ikiwemo kilimo na projects zingine.
kaka Only God knows. huko unakoita vijijini hali ndio mbaya zaidi. kwa wanaotoka vijijini wataleta ushuhuda. Mimi sitaki kumlaumu mtu yeyote kwa wakati mugumu ninaopitia, ninachohitaji nikushikwa mkono, hata nisiposhikwa mkono mimi, basi vijana wengine wanaopitia wakati mgumu kama mimi.
 
Ajira nchi zilianza kuwa tatizo tangia mwaka 1993. Tulitoka UDSM tukaweweseka na bahasha za KAKI . KUNA WALIOKUFA ILA wengine bado typo mpaka Leo tuna shughuli za hapa na pale. KIJANA OMBA UZIMA HAYA YATAPITA.
asante
 
Kijana naelewa sana concern yako, lakini katika hali yako hii ya kutokuwa na ajira, hebu angalia advantage ya wewe kutokuwa na ajira. Lakini katika kitu kitakachokufanya ufe maskini ni ajira.

Nakushauri kwa hali yeyote ngumu itakavyokuwa najua ni vigumu sana, jiajiri . Mungu atakubariki tu, anza kufanya kitu, Mungu huwa habariki patupu. Utafanikiwa tu, tena utashukuru kwa kutokuajiriwa
Mkuu samahani kama ntakukwaza lakini inategemea sana. kwa hiyo usimpotoshe kijana, sisi wengi tuliotoka familia duni inabidi tuajiriwe kwanza halafu ndio tujiajiri sasa. Watu wameajiriwa huku na wanapiga hela vibaya. My assistant ofisini kwangu hajafika hata form four, ila anafanya kazi vizuri sana. mimi nilipoajiriwa nilimkuta na ni muaminifu sana. salary yake ni above 1M kutoka hapa ofisin na amejenga, ana familia yake nzuri tu, ana biashara zake big time. sio eti kila ukiajiriwa hutofanikiwa.
 
Najua hali unayopitia ndugu. Maisha ni katili sana na binadamu hawana wema. Labda kama ungekuwa unatafuta pesa ya kunywa bia au umekamatwa kwa kutukana wanasiasa ungechangiwa. Kaza roho, kuwa na subra na jaribu mambo madogo madogo.
- Nipo kwenye hali ngumu labda hata kuliko yako, naishi kwa nguvu ya Tumaini na Subra tu. Sina thamani yoyote kwa sasa, natengwa na watu kila siku. Nikibahatika kupata Lunch nakosa uhakika nitakula tena lini.
- Nimetafuta kazi viwandani, madukani, kutembeza bidhaa barabarani bila mafanikio. Nina idea yangu nzuri sana ya biashara nimejaribu kuipitch kwa watu lakini hawaniamini.Nimetafuta mkopo Tsh 300,000 hakuna aliyenipa kumbuka Hauko peke yako katika hali hiyo, kuwa mvumilivu ni MAPITO tu yanapita. FINALLY YOU WILL LIGHT AT THE END OF THE TUNNEL !!
Aiseee. vijana mnaandika kwa hisia sana mpaka tunapata huruma. Poleni wandugu
 
Back
Top Bottom