Watu wengi hawaelewi maana ya mbuzi wa kafara, hata kwenye siasa inatokea

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
279
480
Utoaji wa kafara ni sawala la kiasili tangia jadi na jadi, limekuwa likifanyika katika kila aina ya jambo linapoanzishwa au kipindi kipya, hakuna jambo lolote linaanzishwaga bila kafara. Hata ukianzisha biashara unaanza kuzika mtaji kwanza, Hata huku kwetu kanisani tunazo aina zetu za kafara pia.

Mbuzi wa kafara anaweza kupatikana kwa njia nyingi, ikuwemo kujadiliana, mchakato, kisiri au kesi na kushitakiwa lakini lazima mbuzi wa kafara achinjwe hili muzimu upokee na mambo yaendelee. Haya ni mambo ya kawaida kabisa katika jamii yeyote ile kafara utolewa za aina tofauti tofauti, na zimekuwa zikikubarika katika jamiizote, lakini tatizo linakuja tu akichukuliwa mbuzi wenu kutolewa kafara hapo inakuwa shida.

Katika siasa tumeshuhudia mbuzi wengi katika nyakati tofauti wakitolewa sadaka, lakini tuliona kundi lililomtoa huyo mbuzi au mbuzi mwenyewe walilalamika lakini wale walio kuja kumla mbuzi ilikuwa furaha na vicheko. Kuna mbuzi waliwai tolewa katika chama tawala wengi tu, na kunawatu walifurahi na wengine kununa. Kun ambuzi walitolewa kafara kutoka vyama vya upinzani pia wengi tu, na wengine walifurahi na wengine kununa.

Kwahiyo hii tabia ya kuto kafara ipo na aijaanza leo na haijakatazwa wala hajawai mtu au kikundi chochote kusema ikomeshwe isipokuwa upande unaotolewa mbuzi wa kafara unanunaga lakini mambo yanaendeleaga.

Sasa leo tupo katika mchakato wa kupata mbuzi wa kafara kule kwa Pilatoz lakini malalamiko yanazidi kuwa mengi utadhani ni jambo jipya. Na ikumbukwe kuwa maranyingi mbuzi wa kafara huwa anatolewa mwanzoni mwa kipindi na si katikati au mwisho. Na hakunaga mbuzi anayejua kuwa atatolewa kafara, tatizo akijua kuwa ni yeye au kunadalili kama za kutolewa sadaka hapo macho yaana amza kumtoka kama fundi saa au hilo kundi linaanza kulalamika.

Na jambo la ajabu na kushanga katika utoaji wa kafara huwa mbuzi wa kafara akichaguliwa tu abadilishwi na mwisho wa siku analiwa kama kawaida na kazi inaendelea. Mi nadhani kuna haja ya kujiandaa kisaikolojia kwani inaaminika shughuli haita weza kuendelea mpaka kafara itolewe, hivyo nachokiona hapa hii kafara tukubali au tukatae lazima ifanyike kama ilivyo desturi na mambo mengine yataendelea kama kawaida.

Nahizi kafara ni zaajabu sana huwa zinakujaga kubadilika wakati mwingine na kuleta matokea chanya kama Nelson alitolewa kafara na Bota lakini baadae kibao kilibadilika baada ya mamiaka, kumbe kafara inaitaji uvumilivu inaletaga majibu yake baadaye.

Kama unaelewa changia, mtoto wa mchungaji nimewasilisha.
 
Wacheni Waziri wa watu alale salama. Ni muda wake umefika hakuna ujanja. Mnazoza Sana!
 
Najua pia kule kwenye misafara ya baharini au ziwani chombo kikianza kwenda mlama kutokana na hali ya hewa kuchafuka ghafla nahodha na wasaidizi wake huanza kutosa mizigo baharini au ziwani lakini hali isipokoma basi wataanza kuangaliana wenyewe kwa wenyewe kama kuna anaye sababisha nuksi basi lazima atoswe ili safari iendelee salama.
 
Back
Top Bottom